Kabla ya Ikulu Makombe 5 ya Yanga yatua mjengoni SportPesa@tzsportpesaShukrani kwa mdhamini wetu mkuu @tzsportpesa
  • Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa, GSM watajwa kusuka mpango hatari wa ubingwa.
  • SportPesa na Yanga wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8.
  • SportPesa ambao ni wadhamini wakuu wa Yanga kupitia mkataba huo wameipa Yanga jeuri kusaini mastaa wakubwa kama Pacome wakiichangia Bilioni 17.

Mara baada ya mechi ya ushindi ya Yanga SC 2-0 Simba SC na wananchi kutangaza ubingwa wao wanne mfululizo wa Ligi Kuu Bara, Uongozi wa Yanga umezishukuru taasisi mbalimbali zilizochangia mafanikio hayo, huku jina la SportPesa likitajwa kwa herufi kubwa kutokana mchango mkubwa wa kifedha walioipa Yanga.

Kwanini Yanga waishukuru SportPesa?

Mkataba Yanga SC na SportPesa
Mkataba Yanga SC na SportPesa

SportPesa na Yanga wamekuwa na mahusiano ya muda mrefu yanayokaribia kufikia miaka 8, ambayo inagawanyika katika vipindi viwili. Mkataba wa kwanza wa SportPesa na Yanga ulikuwa wa miaka mitano ambao ulimalizika mwaka 2022 ukiwa na thamani ya Bilioni 5.2

Mwaka 2022 SporPesa na Yanga ziliingia mkataba mwingine wa miaka mitatu wenye thamani ya Bilioni 12.33, ambapo kwenye kila msimu Yanga wamekuwa wakivuna kiasi cha Shilingi Bilioni 4 ambazo zimekuwa zikitumika kwa maendeleo ya timu hiyo.

SOMA HII PIA: Mwamuzi Yanga SC vs Simba SC balaa! kuna kadi nyekundu leo?

SportPesa yaipa Yanga jeuri usajili wa Aziz Ki, Pacome

Kufuatia mzigo huo mzito wa Pesa ambao Yanga wamekuwa wakiuvuta kutoka SportPesa, Wananchi wamekuwa na jeuri ya kushusha wachezaji bora kama Aziz Ki na Zouzoua Pacome. ambao wameifanya timu hiyo kutawala soka la Tanzania kwa misimu minne mfuluizo.

Pacome aiteka shoo mbele ya Simba kwa mkapa Jumatano

Pacome vs Simba SC
Pacome vs Simba SC

Pacome mbele ya Simba SC jana Jumatano alikuwa kwenye siku bora kazini, mguu wake wa kulia ukihusika kwenye mabao yote mawili, alitoa pasi ya bao kwa Clement Mzize na kufunga bao la Penalti mbele ya Simba SC.

Hizi ni alama nyingine tatu muhimu kwa Yanga mbele ya Simba msimu huu, ikumbukwe kwamba mzunguko wa kwanza Simba SC ilipoteza mbele ya Yanga SC. Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 0-1 Yanga SC.

Walioamua mchezo wa jana Yanga SC 2-0 Simba SC

Pacome Zouzoua

Ni kiungo wa kimataifa wa Ivory Coasta, Pacome Zouzoua ndiye aliandika bao la kwanza dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati. Penati hiyo ilisababishwa na kipa wa Simba SC, Moussa Camara kwenye harakati za kuokoa hatari.

Matokeo hayo yamemfanya Pacome sasa kufikisha mabao 12 ndani ya ligi huku pia Pasi za mabao ambazo anazo ni 9, hivyo kahusika kwenye mabao 21 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC. Kinara ni Jean Ahoua wa Simba SC mwenye mabao 16 na pasi 9 za mabao.

Clement Mzize

Mshambuliaji kinda wa Yanga, Clement Mzize aipigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la Simba dakika ya 87, baada ya kupachika bao la pili. Mzize alianza benchi alichukua nafasi ya Prince Dube. Bao hilo linamfanya afikishe mabao 14 akiwa ni mzawa mwenye mabao mengi.

Washambuliaji Yanga SC wauwasha moto

Mzizeeeeeee⚽️
Mzizeeeeeee

Yanga SC safu yao ya ushambuliaji imekuwa na balaa ambapo kwenye mechi tatu imefunga jumla ya mabao 12. Mechi hizo ni dhidi ya Tanzania Prisons 0-5 Yanga SC, Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji na Yanga 2-0 Simba SC. Huku ukuta wao ukigoma kuruhusu bao.

Ikumbukwe kuwa Yanga SC ndio timu namba moja kwa timu iliyofunga mabao mengi. Jumla ni mabao 83 imefunga. Timu namba mbili ni Simba SC ambayo imefunga mabao 69. Kinara wa utupiaji kwa Simba SC ni Ahoua.

Kikosi cha Yanga SC kilichoanza dhidi ya Simba SC

Djigui Diarra, Israel Mwenda, Boka, Ibrahim Bacca, Dickson Job, Khalid Aucho, Maxi Nzengeli, Prince Dube, Pacome, Mudathir Yahya, Duke Abuya.

Simba SC kikosi kilichoanza dhidi ya Yanga SC

Moussa Camara, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen Zimbwe Jr, Chamou Karaboue, Che Malone, Kagoma, Ellie Mpanzu, Fabrince Ngoma, Steven Mukwala, Jean Ahoua na Joshua Mutale

Waamuzi

Yanga SC 2-0 Simba SC: SportPesa
Mwamuzi Yanga vs Simba

Mechi hiyo ilisimamiwa na waamuzi kutoka mataifa matatu ambayo ni Tanzania, Misri na Somalia. MisriMwamuzi wa kati kutoka Misri, Amin Omar, msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal na msaidizi namba mbili ni Samir Gamal Saad.

Historia imeandikwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumatano, Juni 25 2025. Yanga SC ambao ni wenyeji wa Simba SC katika mchezo mkubwa wa Kariakoo Dabi. Ni matukio makubwa mawili yalikuwa yanasubiliwa mshindi na bingwa.

Jambo jingine la kihistoria ni kuwa katika mchezo huu ni matumizi ya waamuzi wa kigeni ambapo jopo zima la waamuzi watakaosimamia mchezo wanatokea nje ya Tanzania likiongozwa na waamuzi wanne wa Misri na mmoja wa Somalia huku Kamishina wa mechi akitokea Tanga.

Kadi za njano zimetembea

Mwamuzi wa derby, Amin Omar kwenye utoaji wa kadi amekuwa na rekodi za hatari ambapo akiwa amechezesha jumla ya mechi (240), kwenye hizo mechi ametoa kadi za njano (826), ametoa jumla ya kadi nyekundu (47).

Katika mchezo wa jana mchezaji wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano alikuwa ni Pacome. Pacome alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 21 ya mchezo. Hivyo anaingia kwenye rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano Kariakoo Dabi mzunguko wa pili.

Shinda Bilioni ya SportPesa Supa Jackpot

Unaweza kuwa mshindi ajaye wa zaidi ya Bilioni inayotolewa na SportPesa kwa kubonyeza sasa picha hii chini.

Hitimisho

Hatimaye msimu wa Ligi Kuu Bara umefikia tamati kwa Yanga kushinda ubingwa, huku Wananchi wakiishukuru SportPesa mdhamini kuu namfadhili wao, Ghalib Said Mohammed (GSM), huku Yanga pia wakiandika historia ya kupoteza mara moja tu, kati ya makutano 10.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.