- Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imebainisha kuwa msimu wa 2025/26 unatarajiwa kuanza rasmi Septemba 17 2025 kwa mechi mbili za ufunguzi.
- Kariakoo Dabi mzunguko wa kwanza Yanga SC itakuwa nyumbani kuwakaribisha watani zao wa jadi Simba SC Uwanja wa Mkapa.
- Hatuchezi, tunacheza dawa yapatikana, kanuni mpya kwa timu ambayo haitafika uwanjani yabainishwa.
Ratiba ya mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC ipo wazi. Msimu mpya wa 2025/26 unatarajiwa kuanza Septemba 17 2025. Ikumbukwe kwamba mabingwa watetezi wa taji la ligi ni Yanga SC inayodhaminiwa na kampuni ya SportPesa.
Muda wakushinda mamilioni sasa na Kindege cha SportPesa
Kila siku kuna mgao kwa marubani wanaopaisha Kindege cha SportPesa.Muda ni sasa cheza Aviator upate mgao wako.

Ratiba ya Ligi Kuu Bara Tanzania Bara ya NBC

Soma hii: Ligi Kuu ya Tanzania 2024/25: Muhtasari wa Msimu – SportPesa Tanzania
Mapema Agosti 29 2025, ratiba ya ligi ya NBC ilikuwa wazi. Kwa mujibu wa Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, (TPLB), Ibrahim Mwayela ameitaja ratiba hiyo. Amebainisha kuwa mechi zote za raundi ya mwisho zitachezwa muda mmoja. Aliongeza kuwa Kariakoo Dabi ya kwanza itachezwa Desemba 13 2025 mwenyeji atakuwa Yanga SC.
“Katika ligi hiyo ufunguzi itakuwa ni Septemba 17. Mechi za ufunguzi zitakuwa ni KMC FC itacheza dhidi ya Dodoma Jiji FC Uwanja wa KMC Complex. Coastal Union dhidi ya Tanzania Prisons, Mkwakwani Tanga.
“Tunategemea ratiba yetu kwamba mechi za mwisho raundi ya 30 itakuwa Mei 30. Kwa maana ya ratiba zetu siku hiyo mechi zote zitachezwa muda mmoja. Tunaamini kwamba timu zimejiandaa na ligi itakuwa na ushindani,” amesema.
Uwanja wa nyumbani kwa Simba SC na Yanga SC 2025/26

Soma hii: Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Watani wa jadi Simba SC na Yanga SC, 2024/25 walikuwa wanautumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani. Itakuwa tofauti msimu wa 2025/26 uongozi wa Yanga SC utautumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wa nyumbani. Simba SC itabaki Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani.
Hii hapa ratiba ya mechi za Dabi 2025/26
Kariakoo Dabi

Soma hii: Kariakoo Dabi kuna vita nyingine kwa wachezaji
Watani wa jadi Yanga SC na Simba SC kuna dakika 180 ndani ya ligi wakiwa na Dabi ya Kariakoo. Mchezo wa raundi ya kwanza unatarajiwa kuchezwa Desemba 13, 2025. Yanga SC atakuwa mwenyeji Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wa pili wa Kariakoo Dabi unatarajiwa kuchezwa April 04, 2026. Mzunguko wa pili ni Simba SC atakuwa nyumbani. Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Dar Dabi
Azam FC vs Yanga SC, mchezo wa kwanza ratiba yake itapangwa. Ni Azam FC watakuwa nyumbani na mchezo utachezwa Uwanja wa Azam Complex. Mzunguko wa pili unatarajiwa kuchezwa Mei 14 2026, Uwanja wa Mkapa muda utapangwa.
Mzizima Dabi
Hii huwakutanisha Simba SC vs Azam FC. Novemba 2 2025 mchezo wa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kuchezwa. Muda wa mchezo utapangwa ambapo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, Simba SC itakuwa nyumbani.
Mzunguko wa pili muda na tarehe utapangwa. Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex. Wababe hawa watakutana kukamilisha ngwe ya pili.
Mbeya Dabi
Kuna timu mbili zenye ushindani mkubwa kutoka Nyanda za Juu Kusini, Mbeya. Ni Tanzania Prisons na Mbeya City. Oktoba 21 2025 itakuwa ni Mbeya City vs Tanzania Prisons na Machi 18 2026 itakuwa Tanzania Prisons vs Mbeya City, zote zitachezwa Uwanja wa Sokoine.
Kanuni kwa timu ambayo haitafika uwanjani

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC ni Juni 25 2025 sio Juni 15 2025
Msimu wa 2024/25 ulikuwa na matukio mengi mazuri na magumu. Miongoni mwa mvutano mkubwa ilikuwa mchezo wa mzunguko wa pili wa Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC. Mwisho wababe hawa walikutana na ushindi ulikuwa kwa Yanga SC ambao ni mabingwa watetezi.
Kutokana na mvutano huo kwa kila timu kuvutia upande wake. Sakata ambalo lilianza Machi 8 2025 kwa Simba SC kugomea mechi na Yanga SC kufika uwanjani. Hata ilipopangwa tarehe nyingine na TPLB, Yanga SC waligomea mazima. Kutokana na hilo, kanuni mpya imetungwa.
Ni Kanuni ya 31, kutofika uwanjani inasema hivi:- Timu yoyote itakayokosa kufika uwanjani bila ya sababu za msingi zinazokubalika kwa TPLB au mchezo usifanyike itakabiliwa na adhabu ya kupoteza mchezo huo na timu pinzani itapewa ushindi wa pointi tatu na magoli matatu.
31 (1.2). Lakini pia timu kutozwa faini isiyopungua shilingi milioni hamsini (50,000,000/-) ambapo 50% ya faini itachukuliwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania na 50% italipwa kwa timu.
31 (4.1). Timu Kupokwa alama 3 katika msimamo wa Ligi pamoja na Mwenyekiti au Rais wa Klabu kufungiwa kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi mitano.
Hitimisho
Kutoka kwa ratiba ya ligi ya NBC 2025/26 ni mwanzo kuanza kusaka bingwa mpya mwingine.Ligi ya Tanzania ni namba tano kwa ubora Afrika ushindani wake ni mkubwa. Yanga SC ni mabingwa mara 30 wanaingia kwenye kibarua cha kutetea taji lao kwa mara nyingine tena.


