Ali Kamwe Ofisa HabariAli Kamwe Ofisa Habari
  • Yanga SC vs Simba SC ni Juni 25 2025 sio Juni 15 2025, ngoma imegeuka juu chini, Yanga SC wakubali kucheza mchezo ujao.
  • Simba SC ngoma nzito walitarajia kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa Juni 14 2025 kuwakabili Yanga SC.
  • Wimbo wa hatuchezi kugota mwisho kwa watani hao wa jadi katika msako wa pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.

Yanga SC vs Simba SC ni Juni 25 2025 na sio Juni 15 2025 baada ya mchezo huo namba 184 kupelekwa mbele na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB). Watani hao wa jadi wanatarajiwa kukutana kwenye mzunguko wa pili katika msako wa pointi tatu muhimu. Kuchezwa kwa mchezo huo wimbo wa hatuchezi utakuwa umegota mwisho msimu wa 2024/25.

Yanga vs Simba Juni 15
Yanga vs Simba Juni 15 2025 imeota mbawa.

Taarifa iliyotolewa na TPLB Juni 13 2025 na TPLB imeeleza imeusogeza mbele mchezo huo wa watani wa jadi mpaka Juni 25 2025. Taarifa hiyo imeeleza namba hii: “Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) imeusogeza mbele mchezo wa NBC namba 184 kati ya Yanga SC uliotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 mpaka Juni 25 2025, saa 11:00 jioni bodi inawatakia maandalizi mema.”

Taarifa muhimu kuhusu mechi ya Juni 15 imegeuka

image

Licha ya Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) Karim Boimanda kupitia Azam TV Juni 12 2025 kuweka wazi kuwa maandalizi kuelekea mchezo wa Kariakoo Dabi uliotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 yapo vizuri na kuna taarifa nyeti na muhimu zitatolewa muda wowote kuanzia sasa ngoma imegeuka.

Boimanda alibainisha kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yanaendelea vizuri kutokana na ukubwa wa mchezo ambao unatoa taswira ya ligi ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika. Hivyo kila kitu kinakwenda sawa.

“Maandalizi yapo vizuri lakini pia ni vizuri nikitoa taarifa kuwa kuna baadhi ya taarifa nyeti na muhimu kwa ajili ya mchezo huo zitatolewa muda wowote kuanzia sasa hivyo zitakuwa zinakwenda kutamatisha kuhusu maandalizi ya mchezo nadhani wadau wanapaswa kusubiri kusikia kutoka bodi ya ligi kusikia kuhusunia na mchezo huo.

“Tumekuwa tukisisitiza kuwa maandalizi yanaendelea. Tunaamini kwamba wadau wengine zikiwemo hizo timu mbili Yanga SC na Simba SC wanaendelea na maandalizi mchezo ambao ni mkubwa mchezo namba 184 ambao ni kioo cha ligi yetu mchezo ambao umekuwa ukivuta hisia za watu wengi.

Karim Boimanda
Karim Boimanda, Ofisa Habari TPLB.

Isome hii:Yanga SC vs Simba SC taarifa muhimu kuhusu waamuzi wa mchezo Juni 15 2025 viingilio kutolewa

“Kuna baadhi ya taarifa muhimu zitatolewa muda mfupi kuanzia sasa zinatarajiwa kutolewa hivi karibuni ikiwa ni kama vile maofisa wa mchezo, kwa maana ya waamuzi, viingilio masuala ya uuzwaji wa tiketi zitatolewa hivi karibuni.” Alisema Boimanda.

Simba SC walichungulia mbali kumbe

Simba SC ni kama walichungulia mbali kwa kujua kwamba pengeni mchezo huo utabadilishwa tarehe. Jambo hilo lilitimia licha ya taarifa yao kueleza kuwa hawatakuwa tayari kwa mchezo wa tarehe nyingine. Baada ya tarehe mpya kupangwa, uongozi wa Simba SC umechunia jambo hilo kwa muda.

Isome taarifa ya Simba SC, Juni 12 2025: “Klabu ya Simba inautaarifu Umma, wanachama na wapenzi wake kuwa itaingia uwanjani siku ya Jumapili Juni 15, 2025 kushiriki mchezo namba 184 kama ilivyopangwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania.

Kocha Simba Fadlu
Kocha Mkuu wa Simba SC, Fadlu Davids. Source: Simba SC.

Isome hii:Hatuchezi ya Yanga SC imehamia Simba SC kuelekea Juni 15, Mambo yazidi kuharibika

“Mabadiliko yoyote ya kujaribu kuahirisha mchezo huo ni batili na kinyume na taratibu za uendeshaji wa mpira wa miguu. Kwa msingi huo, Klabu ya Simba haitashiriki mchezo wowote wa namba 184 isipokuwa ule uliopangwa kuchezwa siku ya Junapili Juni 15 2025. Tunawaomba wanachama na wapenzi wa klabu yetu kujitokeza kwa wingi kuijaza Benjamini Mkapa siku hiyo muhimu, ili kuiunga mkono timu yetu.”

Haya hapa matakwa manne ya Yanga SC

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC aliweka wazi matakwa manne ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili kucheza mchezo huo wa mzunguko wa pili ila isiwe Juni 15 2025 bali kwa tarehe nyingine ambayo itapangwa ilikuwa namna hii:-

“Tumetoa matakwa manne. Katika haya manne matatu ni matakwa ambayo tunaamini yakitekelezwa kwa haraka klabu yetu ya Yanga SC itakuwa tayari kwenda uwanjani kucheza mechi kwa tarehe nyingine itakayopangwa.

Ali Kamwe (-)
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Soma hii:Yanga SC wametoa matakwa manne yakitimizwa Kariakoo Dabi kuchezwa

“Takwa letu la kwanza na la pili linahusu ukiukwaji wa kanuni uliofanyika Machi 8. Tunataka Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi pamoja na CEO wa Bodi ya Ligi Almasi Kasongo wawajibike kwa kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia kanuni na kuutia doa mpira wetu. Ligi yetu ni kubwa sana Afrika na inataka watu makini wenye weledi kuiongoza.

“Kuahirishwa kwa mechi ya Machi 8 tunaamini kama klabu hapakufuatwa utaratibu na kulikuwa na uvunjaji mkubwa wa kikanuni hivyo tunaamini CEO wa Bodi ya Ligi na kamati ya uedeshaji wa kamati ya ligi ilifanya hayo kwa ajili ya kuwapa favour timu fulani. Klabu ya Yanga SC haitakuwa tayari kushiriki mechi namba 184 kama kamati nzima ya uendeshaji na usimamizi wa bodi haitajiuzulu au kuvunjwa.

“Takwa letu la tatu ni kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao kwa kushindwa kuchukua hatua dhidi ya maamuzi mabovu ya mara kwa mara ya waamuzi. Kamati ya waamuzi ipo chini ya TFF kwa Katibu Mkuu, unashangaa ni vipi mwamuzi mmoja anafanya makosa yakujirudia na bado anaendelea kupangwa kwenye mechi bila kuchukuliwa adhabu yoyote ile. Takwa la nne zawadi ya ubingwa wa CRDB.”

Juni 13 2025, Simba SC walitoa taarifa kwamba wamepata ruhusu ya kufanya mazoezi ya mwisho Uwanja wa Mkapa, Juni 14 2025 kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga SC. Juni 13 taarifa ikatolewa kuwa mchezo huo namba 184 umepelekwa mbele mpaka Juni 25 2025.

Share this: