Seleman GSeleman G
  • Mshambuliaji wa magoli ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
  • Seleman Mwalimu mguu wake wenye maajabu akiwa uwanjani ni ule wa kulia tayari yupo Tanzania akifanya mazoezi binafsi.
  • Rasmi atajiunga na wachezaji wa Simba SC kambini kwa maandalizi ya Simba Day Septemba 10 2025 Uwanja wa Mkapa.

 Seleman Mwalimu ametambulishwa Simba SC ikiwa ni usajili mpya kwenye kikosi hicho. Agosti 28 2025 Mwalimu ametangazwa kuwa ni ingizo jipya kuelekea msimu wa 2025/26 baada ya tetesi. Anajiunga kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea kikosi cha Wydad Casablanca ya Morocco.

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Nafasi yakushinda mamilioni inakusubiri muda huu hivyo amua kucheza Aviator. Ni rahisi sana kupata mgao wako wa mamilioni. Bofya picha hii chini na upaishe Kindege cha SportPesa.

SEO Banner LV

Utambulisho wa Seleman Mwalimu Simba SC

Sele Mwalimu Gomez
Seleman Mwalimu Gomez nyota mpya wa Simba SC.

Soma hii: Selemani Mwalimu rasmi atua Simba SC: Aungana na Sowah, Mukwala kuelekea Ligi Kuu ya NBC 2025/26

Mapema saa 8:00 mchana Simba SC ilimtambulisha Mwalimu kwenye ukurasa wa Instagram. Huyu ni mshambuliaji mzawa ambaye alikuwa na rekodi nzuri kabla ya kuelekea Morocco. Ni Fountain Gate alikuwa anacheza ambapo hapo alikuwa kwa mkopo msimu wa 2024/25.

Tayari Mwalimu yupo Dar akisubiri kujiunga na kikosi kambini. Kikosi cha Simba SC kiliweka kambi Misri ambayo tayari imekamilika. Usiku wa kuamkia Agosti 29 2025 msafara wa Simba SC unatarajiwa kuwasili Tanzania.

Washambuliaji watatu ndani ya Simba SC

Steven Mukwala
Steven Mukwala nyota wa Simba SC 2025/26. Source: Simba SC.

Soma hii: Wadi Degla SC 0-2 Simba SC: Magoli yote, vikosi, highlights, h2h

Mwalimu anakwenda kuungana na washambuliaji wawili waliokuwa Simba SC. Ni Jonathan Sowah raia wa Ghana na Steven Mukwala raia wa Uganda. Alikuwepo Leonel Ateba kambini rai awa Cameroon huyu amepishana naye kwa kuwa amepewa Thank You.

Rekozi za timu alizozifunga Mwalimu kwenye Ligi ya NBC

Ni mabao 6 alifunga Mwalimu akiwa na Fountain Gate. Alizifunga timu sita kwenye mechi za ushindani. Katika mabao hayo hakufunga kwa mkwaju wa penalti.

Akiwa na uzi wa Fountain Gate msimu wa 2024/25 alikuwa anaongoza chati ya ufungaji. Mpaka anaondoka kwenye ardhi ya Tanzania alikuwa amefunga jumla ya mabao sita. Sio kufunga tu ana uwezo wa kutengeneza pasi za mabao ambapo alitengeneza pasi tano zilizoleta mabao.

Hizi hapa ni timu ambazo alizifunga na matokeo ya Fountain Gate

Agosti 29 2024, Namungo FC 0-2 Fountain Gate mchezo huu ulichezwa saa 1:30 Usiku. Ilikuwa Uwanja wa Majaliwa. Namungo FC ilipoteza pointi tatu na mabao yalifungwa na Edgar William dakika ya 29 huku Seleman Mwalimu akipachika bao dakika ya 45+2.

Septemba 11 2024. Fountain Gate 2-1 KenGold saa 10:15 jioni. Mabao ya Fountain Gate yalifungwa na Abalkassim Suleiman dakika ya 42 na Seleman Mwalimu dakika ya 58. Bao la KenGold ambayo imeshuka daraja lilifungwa na Joshua Ibrahim dakika ya 9.

September 15, 2024. Fountain Gate 2-2 Dodoma Jiji mchezo huu ulichezwa saa 10:15 jioni. Mabao ya Fountain Gate yalifungwa na Seleman Mwalimu dakika ya 50 na Dickson Ambundo dakika ya 86. Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na Hassan Mwaterema dakika ya 27 na Paul Peter dakika ya 76.

September 27, 2024. Fountain Gate 3-1 Kagera Sugar mchezo huu ulichezwa saa 10:00 jioni. Ni Seleman Mwalimu alifunga dakika ya 5, Salum Kihimbwa dakika ya 11 na Elie Mokono dakika ya 90+4. Kwa Kagera Sugar mfungaji ni Obrey Chirwa  dakika ya 50.

Seleman Mwalimu
Seleman Mwalimu 2024/25 alipokuwa na uzi wa Fountain Gate. Source: Fountain Gate.

Soma hii: Man City vs Wydad AC 18/06/2025: H2H, Vikosi Azizi Ki uso kwa uso na Guardiola Marekani leo

October 1, 2024, Tanzania Prisons 3-2 Fountain Gate mchezo huu ulichezwa saa 10:00 jioni. Mabao ya Tanzania Prisons yalifungwa na Nurdin Chona dakika ya 25 kwa mkwaju wa penati, Ezekia Mwashilindi dakika ya 48 na Vedastus Mwihambi dakika ya 50. Kwa Fountain Gate ni Seleman Mwalimu dakika ya 12 na Abalkassim Suleiman dakika ya 37.

October 21, 2024. Fountain Gate 3-1 KMC FC. Mchezo huu ulichezwa saa 8:00 Mchana. Ni Dickson Ambundo dakika ya 8, Seleman Mwalimu dakika ya 23 na Edgar William dakika ya 60. Kwa upande wa KMC mtupiaji alikuwa ni Andrew Vicent ‘Dante’ dakika ya 47.

Mwalimu amecheza Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025

Mshambuliaji mwalimu ni Mtanzania aliyecheza Kombe la Dunia la Klabu la FIFA 2025. Ikumbukwe kwamba taji hilo lipo mikononi mwa Klabu ya Chelsea. Wydad Casblanca ilicheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Manchester City.

Kwa sasa anarejea kwa mara nyingine kwenye ardhi ya Tanzania. Simba SC chini ya Kocha Mkuu Fadlu Davids itakuwa na mshambuliaji huyo kwenye anga la kimataifa. Uzoefu ambao ameupata akiwa Wydad Casablanca ni faida kwa timu hiyo ambayo ngome yake ni Msimbazi, Dar.

Hitimisho

Simba SC inatarajia kuwatambulisha wachezaji wake wote Septemba 10 2025. Siku hiyo ni tamasha la Simba Day. Kauli mbiu ya msimu huu ni Ubaya Ubwela namba 2.

sportpesa jackpot
Share this: