- Yanga SC bado inaendelea na usajili licha ya kutambulisha wapya zaidi ya watano kuelekea msimu mpya wa 2025/26.
- Ali Kamwe amefichua kuhusu usajili wa Zimbwe Jr na wachezaji wengine ambao watakuwa Jangwani kwa msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
- Balla Conte, Doumbia wote wameanza mazoezi kamili kwa msimu mpya wakiwa na uzi mpya wa Yanga SC.
YANGA SC wamebainisha kuwa bado hawajamaliza usajili kuelekea msimu mpya wa 2025/26. Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa kuna wachezaji watatu watambulishwa hivi karibuni. Wachezaji hao ni eneo la ushambuliaji na beki.
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege
Wiki inaanza kwa shangwe ukiwa hewani na mkwanja mfukoni. Paisha kindege na SportPesa ushindi mamilioni. Rahisi sana, cheza Aviator ushindi unakusubiri.

Huyu hapa Ali Kamwe

Soma hii: Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaondoka
“Tutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports Rwanda. Huu utakuwa ni mchezo wa kwanza . Usajili bado hatujamaliza hivyo wanachama wasiwe na presha.
“Usajili wa mwisho ambao tumeufanya ni wa Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Huu wenyewe mmeona namna ilivyokuwa. Huu ni usajili mkubwa.
“Baada ya usajili huo niwaambie wanachama kuwa kuna wachezaji ambao wanafika watatu. Wapo wachezaji wa ndani na wachezaji wakingeni. Hivyo mashabiki na wanachana wa Yanga SC wawe na Subira bado usajili unaendelea.
“Kwenye kila nafasi ni lazima tuwe na wachezaji bora. Tupo kwenye mashindano makubwa ambayo tunashiriki na pia tupo kwenye ligi hivyo ni lazima tuwe imara na kikosi kuwa bora.”
Hawa hapa wapya ndani ya Yanga SC
Ecua Elastin
Agosti Mosi 2025 alitambulishwa Yanga SC kwa dili la miaka miwili. Msimu wa 2024/25 alikuwa anacheza Zoman FC alifunga magoli 15 na pasi 12 za magoli. Rekodi hizo ni kwenye mashindano yote.
Mohamed Doumbia

Soma hii: Yanga SC yashusha mashine hii nyingine usiku: Tetesi, usajili Ligi Kuu ya NBC 2025/26
Ni Agosti 3 2025 Yanga SC ilimtambulisha kiungo, Mohamed Doumbia. Ana miaka 26 amejiunga na Yanga SC akitokea FC Slovan Liberec ya Jamuhuri ya Czech. Anatajwa kuwa na uwezo kwenye majaribio ya mashuti ya mbali na kutengeneza nafasi za mabao kwa wengine.
Boyeli
Yanga SC Julai 31 2025 walimtambulisha Andy Bobwa Boyeli. Nyota huyo ana miaka 24 alikuwa anacheza Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo kwa msimu mmoja. Julai 31 alifunga ukurasa kwa wachezaji waliotambulishwa Julai.
Paul Mattews
Ni Paul Matthews alitambulishwa Yanga SC Julai 29 2025. Yupo Jangwani msimu wa 2025/26. Anaingia kwenye benchi la ufundi yeye ni Mkurugenzi wa Ufundi.
Manu Rodriguez
Anaitwa Manu Rodriguez alitambulishwa Julai 29 2025. Anaingia kwenye benchi la ufundi akiwa ni kocha msaidizi wa Yanga SC. Kocha Mkuu ni Romain Folz ambaye naye ni mrithi mikoba ya Miloud Hamdi.
Lassine Kouma
Lassine Kouma mchezaji mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC. Huyu ni mrithi wa mikoba mikoba ya Khalid Aucho. Kasajiliwa Yanga SC akitokea Stade Malien.
Kiungo huyu amekabidhiwa jezi namba 8 kuwa utambulisho wake akiwa uwanjani. Msimu wa 2024/25 uzi namba 8 ulikuwa ni utambulisho wa Khalid Aucho. Aucho tayari mkataba wake umeisha na hajaongeza mwingine.
Balla Conte
Huyu usajili wake ulikuwa na mvutano mkubwa kwa kuwa alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba SC. Julai 18 2025 Yanga SC ilimtambulusha Moussa Balla Conte. Ingizo hili jipya ni kutoka CS Sfaxien ya Tunisia yeye ni raia wa Guinea.
Offen Chikola

Soma hii: Offen Chikola atambulishwa Yanga SC
Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kushoto akiwa uwanjani kwenye majukumu yake. Anaitwa Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025. Ni kandarasi ya miaka miwili alisaini. 2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Yanga SC inaingia kwenye orodha ya timu ambazo Chikola alizifunga msimu wa 2024/25.
Casemiro
Abdulnassir Mohamed maarufu kwa jina la Casemiro alitambulishwa rasmi Jangwani, Julai 23 2025. Ni mzawa ambaye atakuwa kwenye changamoto mpya. Anaingia kwenye orodha ya wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Yanga SC chenye maskani yake Jangwani, Dar.
Ninju
Jina lake ni Abubakar Nizar Othuman, maarufu kwa jina la Ninju kutoka Azam FC alitambulishwa rasmi Julai 27 2025. Kamwe kuhusu Ninju amesema ni mchezaji makini. Aliongeza kwa kubainisha kuwa Azam FC wamepoteza silaha muhimu.
Romain
Julai 23 2025 Kocha Mkuu wa Yanga SC Romain Folz alitambulishwa. Kocha huyo anabeba mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa akikinoa kikosi hicho. Msimu wa 2025/26 atakuwa kwenye benchi la ufundi na tayari ameanza kazi.
Hitimisho
Yanga SC wanatarajiwa kwenda Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sports. Hayo ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26. Kwenye ligi ni mabingwa watetezi.


