Clement Mzize (-)Clement Mzize (-)
  • CHAN 2024: Tanzania imefuzu hatua ya robo fainali ikishinda mechi zote tatu mfululizo Uwanja wa Mkapa.
  • Clement Mzize ametakata kwenye mchezo dhidi ya Madagascar akitwaa tuzo ya mchezaji bora kwenye mchezo mkubwa kimataifa.
  • Madagascar wamefurukuta na kuifunga goli Tanzania kwenye CHAN 2024 wakitibua rekodi ya Tanzania kutofungwa mechi mbili zilizopita hatua ya makundi.

Tanzania 2-1 Madagascar rekodi mpya imeandikwa kwa Tanzania kutinga hatua ya robo fainali CHAN 2024. Mabao yote mawili kwa Tanzania yamefungwa na mshambuliaji Clement Mzize. Wenyeji Tanzania kwenye Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN 2024) wamekuwa na mwendelezo mzuri uwanjani.

Aviator banner

Wafungaji wa magoli Uwanja wa Mkapa

Mzize CAF
Mzize na wachezaji wa Tanzania wakishingalia goli CHAN 2024. Source: TFF.

Soma hii: Tanzania kuikabili Madagascar CHAN 2024

Mabao ya Tanzania yamefungwa na Clement Mzize dakika ya 13 na 20. Goli la Madagascar likifungwa na Nantenaina Razafimahatana dakika ya 34. Magoli yote matatu yamefungwa kipindi cha kwanza.

Kwenye mchezo wa mapema wa kundi B, Afrika ya Kati 0-1 Mauritania. Ikumbukwe kwamba Mauritania walifungwa na Tanzania mchezo uliopita. Leo wamefuta machozi.

Goli la Mauritania lilifungwa na Ahmed Ahmed dakika ya 9. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa. Goli hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Robo fainali yajibu

Malengo ya Tanzania kutinga robo fainali yamejibu. Ushindi wa mchezo wa leo unaipa tiketi Tanzania kutinga hatua ya fainali. Pointi tisa zimekusanywa.

Kikosi cha Tanzania ambacho kilianza

Tanzania v Madagascar
Tanzania v Madagascar, CHAN 2024, Uwanja wa Mkapa. Source: TFF.

Soma hii: Tanzania vs Madagascar Agosti 9 2025 CHAN 2024

Yakoub Suleiman, Shomary Kapombe, Mohamed Hussein, Ibrahim Hamad. Dickson Job ambaye ni nahodha, Abdurazak Hamza, Idd Suleiman, Mudathir Yahya, Clement Mzize. Kiungo Feisal Salum na Abdul Suleiman maarufu kama Sopu walianza.

Aishi Manula, Hussen Masalanga, Nassor Saadun, Sheikh Khamis. Jammy Jammy, Pascal Msindo, Wilson Nangu, Lusajo Mwaikenda. Elias Lamek, Ibrahim Ahmada, Vedastus Masinde na Mishamo Michael walikuwa wachezaji wa akiba.

Mechi sita za Tanzania ni ushindi

 Eswatini 1-2 Tanzania, mchezo huu ulichezwa Juni 11 2025. Tanzania 1-0 Uganda ulichezwa Julai 22 2025. Tanzania 2-1 Senegal ulichezwa Julai 27 2025.

Tanzania 2-0 Burkina Faso ulichezwa Agosti 2 2025. Huu ulikuwa ni mchezo wa ufunguzi wa CHAN 2024 Uwanja wa Mkapa. Mauritania 0-1 Tanzania, Agosti 6 2025. Tanzania 2-1 Madagascar.

Kwenye mechi sita, safu ya ushambuliaji ya Tanzania ilifunga mabao 10. Ukuta wa Tanzania umeruhusu mabao matano. Kwenye dakika 540 kocha Hemed Suleman mipango yake ilijibu kwa wachezaji kutimiza majukumu kwa umakini.

Safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 54. Safu ya ulinzi ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 108.

Huu hapa msimamo wa Kundi B

Timu ya taifa ya Tanzania inaongoza Kundi B na pointi 9 baada ya kucheza mechi 3. Mauritania nafasi ya pili ina pointi 4 baada ya mechi tatu. Burkina Faso nafasi ya tatu ina pointi 3 baada ya kucheza mechi tatu. Madagascar nafasi ya nne ikiwa na pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.

Jamhuri ya Kati haijakusanya pointi baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wake wa leo Agosti 9 2025 ilipoteza pia. Hivyo ipo inaburuza Kundi.

Wafungaji wa magoli kwa Tanzania CHAN 2024

Mfungaji wa goli la kwanza CHAN 2024 kwa Tanzania ni Abdul Sopu. Kiungo huyo alifunga goli hilo kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso. Ilikuwa ni Agosti 2 2025, Uwanja wa Mkapa.

Mfungaji wa goli la pili kwa Tanzania ni Mohamed Hussen Zimbwe Jr. Beki huyo wa kushoto alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Ilikuwa ni kwa pigo la kichwa Uwanja wa Mkapa.

Goli la tatu lilifungwa na Shomari Kapombe. Beki huyo alifunga kwenye mchezo dhidi ya Mauritania. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 6 2025.

Kapombe alipachika goli hilo akiwa ndani ya 18. Ilikuwa dakika ya 90 akitumia mguu wa kulia kupachika bao la ushindi. Alitumia pasi ya kiungo Idd Nado.

Clement Mzize amefunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Madagascar. Mzize ni mshambuliaji wa kwanza kufunga. Nyota huyo alikuwa chanzo cha penati kwenye mchezo dhidi ya Burkina Faso.

Matokeo ya Tanzania CHAN 2024

Mzize v Madagascar
Mzize v Madagascar, CHAN 2024. Uwanja wa Mkapa. Source: TFF.

Soma hii: Mauritania 0-1 Tanzania CHAN 2024

Agosti 2 2025, Tanzania 2-0 Burkina Faso. Mauritania 0-1 Tanzania. Tanzania 2-1 Madagascar, Agosti 9 2025.

Tanzania kwenye mechi tatu haijapoteza. Mchezo dhidi ya Mauritania ilipata ushindi katika dakika za lalasalama. Imeandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali ikiwa na mechi moja mkononi.

Washindi wa Tuzo za CHAN

Mchezo dhidi ya Burkina Faso ni Feisal Salum alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Mchezo dhidi ya Mauritania ni Mudathir Yahya alichaguliwa. Mchezo dhidi ya Madagascar ni Clement Mzize amechaguliwa.

Hitimisho

Tanzania imefuzu rasmi hatua ya robo fainali. Kwenye mechi tatu ambazo ni dakika 270. Mech izote ilishinda.

image
Share this: