- Zimbwe Jr usajili wake umekamilika ndani ya Yanga SC ametambulishwa usiku mzito kwa ajili ya changamoto mpya akitokea Simba SC.
- Beki mzawa mwenye tuzo zakutosha kabatini kwake na mguu wake wenye nguvu ni ule wakushoto katika kutimiza majukumu yake.
- Amedumu Simba SC kwa muda wa miaka 11 akiwa katika ubora wake uleule, chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids msimu wa 2024/25.
Mohamed Hussen Zimbwe Jr ametambulishwa Yanga SC rasmi akitokea Simba SC. Beki huyo msimu wa 2024/25 alikuwa chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Simba SC Fadlu Davids. Amesajiliwa Yanga SC kwa changamoto mpya kuelekea msimu wa 2025/26.
Yanga SC imeinasa saini ya Zimbwe Jr akiwa mchezaji huru. Mkataba wake na Simba SC uliisha mara baada ya msimu wa 2024/25 kufika tamati. Msimu ujao atakuwa ni kijani na njano.
Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege
Mamilioni yanakusubiri sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Ni rahisi sana hapo ulipo una nafasi ya kushinda. Cheza Aviator upate mgao wako haraka sana.

Mkataba wa Zimbwe Jr na Yanga SC
Zimbwe Jr amesaini kandarasi ya miaka miwili, kwa sasa yupo na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mashindano ya CHAN. Kwenye mchezo wa ufunguzi dhidi ya Burkina Faso uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Agosti 2 2025 Zimbwe Jr alifunga bao moja. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Tanzania 2-0 Burkina Faso huku bao la kwanza likifungwa na Sopu kwa mkwaju wa penati.
Timu alizocheza Zimbwe Jr na mafanikio

Soma hii: Mohamed Hussen Zimbwe Jr amefuta utambulisho wa Simba SC
Zimbwe Jr alicheza Azam FC timu ya vijana kisha akawa ndani ya Kagera Sugar. Simba SC ilinasa saini Zimbwe Jr kutoka Kagera Sugar. 2014 alikuwa ndani ya Simba SC akidumu kwa miaka 11. Akiwa na Simba SC ametwaa mataji manne ya ligi, mataji matatu ya CRDB Federation Cup, mataji matano ya Ngao ya Jamii, mataji matatu ya Mapinduzi na taji moja la Muungano.
Zimbwe alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC ambacho kimetinga mara sita hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CAF. Mafanikio makubwa akiwa na uzi wa Simba SC ni kufika hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika 2024/25. Kati ya 2017-2024 alikuwa ni nahodha msaidizi na msimu wa 2024/25 alikuwa ni nahodha mkuu.
Aliwaaga Simba SC mapema kabisa
Zimbwe Jr baada ya ligi kuisha ilielezwa kuwa kulikuwa na mazungumzo na mabosi wa Simba SC kuhusu kuongeza mkataba wake. Baada ya kushindwa kufikia makubaliano aliamua kuondoka. Julai 19 2025 aliandika ujumbe rasmi kuwaaga Simba SC.
Tetesi zilikuwa zinaeleza kuwa huenda atatambulishwa Yanga SC. Inaelezwa mkataba ambao alisaini una kipengele cha mshahara milioni 25. Mshahara huo ilitajwa kuwa Simba SC waligomea kumpa.
Rekodi za Zimbwe Jr na Simba SC kwenye ligi 2024/25

Soma hii: Simba SC yakata tamaa kuhusu Zimbwe Jr
Baada ya Simba SC kucheza mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Zimbwe Jr ni mechi 27 alipata nafasi yakucheza akikosekana kwenye mechi tatu ambazo ni dakika 270.
Kwenye mechi 27 ambazo alicheza alitumia dakika 1,817. Alihusika kwenye mabao manne kati ya 69 yaliyofungwa na Simba SC kwenye ligi. Ni pasi tatu za mabao alitoa huku akifunga bao moja katika mechi alizocheza.
Mchezaji wa kwanza kusababisha penalti Simba SC 2024/25
2024/25 Simba SC ni namba moja kwa timu iliyopata penalti nyingi. Baada ya mechi 30 ni penalti 13 ilipata. Katika penalti hizo 12 zilijaa nyavuni na moja iliokolewa na mlinda mlango.
Wapigaji wa penalti kwa Simba SC ni wachezaji wawili. Leonel Ateba na Jean Ahoua. Ateba alipiga penalti 7, alifunga penalti sita na alikosa moja dhidi ya Namungo FC. Jean Ahoua alifunga penati 6 katika mapigo yake yeye hakukosa penalti.
Ni Zimbwe huyu alikuwa mchezaji wa kwanza kusababisha penalti ndani ya Simba SC. Ilikuwa mchezo dhidi ya Dodoma Jiji uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Ilikuwa Septemba 29 2024.
Salmin Hoza dakika ya 60 alimchezea faulo Zimbwe Jr ndani ya 18. Mwamuzi wa kati alikuwa ni Omary Mdoe aliamuru adhabu ya penalti. Mpigaji wa kwanza alikuwa ni Jean Ahoua aliyefunga bao la ushindi kwenye mchezo huo.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Dodoma Jiji 0-1 Simba SC. Pointi tatu zilikuwa ni mali ya Simba SC. Hivyo penalti ya Zimbwe ilikuwa ni sababu ya Dodoma Jiji kupoteza pointi tatu wakiwa nyumbani.
Tatu alizokosekana akiwa na uzi wa Simba SC
Zimbwe Jr alikosekana kwenye mechi tatu za ligi. Ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya KMC uliochezwa Uwanja wa KMC Complex ni Novemba 6 2024. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 4-0 KMC FC. Mchezo wa pili ilikuwa Novemba 22 2024, Pamba Jiji FC 0-1 Simba SC.
Mchezo wa tatu ilikuwa Coastal Union 0-3 Simba SC, Machi Mosi 2025. Ni mechi moja Simba SC ilikuwa nyumbani na mechi mbili ugenini. Kwenye msako wa pointi tisa ambazo Zimbwe alikosekana zote zilipatikana kwa ushindi na mabao 8 Simba SC ilifunga.
Pasi za mabao na timu aliyoifunga Zimbwe Jr

Soma hii: Simba SC 1-0 Kagera Sugar ni mchezo wa mwisho 2024/25
Alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo dhidi ya Tabora United, Uwanja wa KMC Complex. Ilikuwa Agosti 18 2024 alimpa Valentino Mashaka. Pasi ya pili alitoa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Desemba 21 2024, pasi ya tatu alitoa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Machi 14 2025.
Bao pekee alilofunga ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Coastal Unioni. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex ilikuwa ni Oktoba 4 alipachika bao dakika ya 25 kwa mguu wa kulia. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal Union.
Hitimisho
Zimbwe Jr alitwaa tuzo ya beki bora msimu wa 2021/22. Ana tuzo ya MVP msimu wa 2016/17. Msimu wa 2023/24 alikuwa kwenye kikosi bora cha msimu ni mchezaji bora ambaye atakuwa na uzi wa Yanga SC 2025/26.


