Shomy na Zimbwe JrShomy na Zimbwe Jr
  • Simba SC yakata tamaa kuhusu Zimbwe Jr kuongeza mkataba kuendelea na majukumu yake msimu wa 2025/26.
  • Yanga SC yatajwa kumpa ofa nono ili asaini mkataba mpya, mpango mzima wasukwa akitua Bongo kumaliza kila kitu.
  • Orodha ya wachezaji walioachwa Simba SC yazidi kuongezeka, kiungo wa kazi Mavambo akutana na Thank You.

Simba SC imekata tamaa kubaki na nahodha Mohamed Hussen Zimbwe Jr kwa msimu wa 2025/26. Zimbwe Jr kwa sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote kwa kuwa hajaongeza mkataba mwingine. Sababu kubwa ni mvutano uliopo pande zote mbili katika suala la maslahi.  

Zimbwe Jr
Zimbwe Jr nahodha wa Simba SC 2024/25. Source: Simba SC.

Soma hii: Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC

Mamilioni yanakusubiri sasa

Vuna mamilioni ukicheza Aviator sasa hivi. Ni mgao ambao unakusubiri ukiwa unapaisha kindege. Wakati kindege kinapaa wewe unashinda.

SEO Banner LV

Mkataba wake ndani ya kikosi cha Simba SC umeisha msimu wa 2024/25 ulipoisha. Baada ya mkataba kuisha inatajwa kuwa mabosi wa Simba SC walifungua ukurasa kuzungumza na uongozi wa mchezaji huyo. Suala hilo halikukufikia pazuri mpaka mchezaji anakwenda Misri kwenye kambi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Zimbwe Jr alijiunga na Simba SC akitokea Kagera Sugar 2015. Aliongeza kandarasi ya miaka miwili Julai 10 2023. Ni yeye na Shomari Kapombe waliongeza miaka miwili ambayo tayari imeisha.

Huyu hapa Ahmed Ally, Semaji la CAF

ahmedally------------------------------------------
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC. Source: Simba SC.

Soma hii: Simba SC kufanya usajili mkubwa

Kwa mujibu wa Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amebainisha kuwa mkataba wa mchezaji umeisha. Ahmed aliongeza kuwa jitihada zinafanyika ili aongeze mkataba. Ikitokea ameongeza itakuwa ni maslahi ya Simba SC na asipoongeza itakuwa ni kwa maslahi ya Simba SC.

“Kwa sasa tulipofikia maamuzi yoyote yatakayoamuliwa itakuwa ni maslahi ya pande zote mbili. Yaani timu na mchezaji mwenyewe. Tukikubaliana tunakwenda na kapteni maana yake ni kwa maslahi yake na klabu.

“Tukisema tunaachana naye maana yake ni kwa maslahi ya Simba SC na mchezaji. Lazima tukubali hilo katika maisha kuna kuja na kuondoka. Hakuna ambaye angetamani kumuona kapteni anaondoka lakini muda ukishaamua umeamua,” alisema Ahmed kupitia Azam TV.

Wapi anakwenda Zimbwe Jr?

Taarifa zinaeleza kuwa ikiwa Zimbwe Jr hataongeza mkataba Simba SC kuna uwezekano akatambulishwa Yanga SC. Mabosi wa Yanga SC wameulizia uwezekano wa kuipata saini ya nyota huyo. Makubaliano inaelezwa yamefikia pazuri.

Zimbwe Jr atasajiliwa Yanga SC akiwa ni mchezaji huru. Ipo wazi kwamba mkataba wake na Simba SC tayari umeisha. Kwa msimu wa 2024/25 Zimbwe Jr alikuwa ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC.

Wachezaji walioachwa Simba SC

Aishi Manula ----
Aishi Manula kipa mpya wa Azam FC 2025/26. Source: Azam FC.

Soma hii: Aishi Manula amesaini mkataba kuitumikia Azam FC akitokea Simba SC i

Wakati Zimbwe Jr akiwa kwenye hesabu za kuondoka kuna orodha ndefu ya wachezaji ambao wameachwa Simba SC. Wapo wale ambao wamepata timu mpya na wengine kandarasi zao zimegota mwisho. Ikumbukwe kwamba wapo wengine ambao wamedumu kwa msimu mmoja pekee ndani ya kikosi cha Simba SC.

Orodha yao ipo namna hii mpaka sasa. Julai 19 2025 Simba SC ilitangaza kuachana na mchezaji mmoja ambaye alikuwa anavaa jezi namba 17. Jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Clatous Chama msimu wa 2023/24 kabla ya kuibukia ndani ya kikosi cha Yanga SC. Hali ipo namna hii:-

Mavambo

Deborah Mavambo alipewa Thank You Julai 19 2025. Nyota huyo alikuwa ni kiungo mkabaji. Amedumu Simba SC kwa msimu mmoja pekee.

Ngoma

Fabrince Ngoma wa Simba SC alitoa Thank You Juni 29 2025. Mkataba wake wa miaka miwili ulikuwa umegota mwisho. Simba SC rasmi walimpa Thank You Ngoma Julai 12 2025.

Omary Omary

Nyota huyu ametolewa kwa mkopo kuelekea Mashujaa. Ni Julai 12 taarifa ilitolewa rasmi. Hivyo hatakuwa na uzi wa Simba SC msimu wa 2025/26.

Air Manula

Aishi Manula, maarufu kwa jina la Air Manula, alipewa Thank You na Simba SC, Julai 12 2025. Kipa huyu msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya kikosi cha Azam FC. Kwa msimu wa 2024/25 hakupata nafasi kikosi cha Simba SC kwenye mechi za ligi.

Valentino Nouma

Nouma alipewa Thank You Julai 12 2025. Huyu ni beki wa kushoto. Ni msimu mmoja pekee amehudumu Simba SC.

Hussen Kazi

Beki Hussen Kazi alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Hakupata nafasi ya kucheza kwenye mechi za ushindani msimu wa 2024/25. Hivyo atakuwa kwenye changamoto mpya msimu ujao wa 2025/26.

Agustine Okejapha

Okejapha alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Nyota huyu ni msimu mmoja pekee amehudumu ndani ya Simba SC. Ni miongoni mwa wachezaji wenye medali ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Kelvin Kijili

Alipewa Thank You Julai 13 2025. Beki huyu bado atakuwa kwenye anga la kimataifa. Singida Black Stars walimtambulisha.

Hitimisho

Simba SC ipo kwenye maboresho kuelekea msimu wa 2025/26. Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC aliweka wazi kuwa ataongea na viongozi kupata wachezaji wenye ubora. 2024/25 Simba SC iliambulia patupu kwenye mataji iliyokuwa inayatafuta ikiwa ni Ligi Kuu Bara ya NBC, CRDB Federation CUP na Kombe la Shirikisho Afrika.

image
Share this: