Simba SC yasajili mashine hizi mbili kwa mpigo,TETESI Tshabalala kutua Yanga
  • Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC, mabosi wavunja benki kumng’oa Simba.
  • Inaelezwa Yanga Rasmi wameanza kujadili ishu za Mshahara, ada ya uhamisho na Bonasi.
  • Kama watafikia makubaliano basi Kiongozi wa Yanga atasafiri kwenda Misri kumsainisha mkataba.

Baada ya kukamilisha na kumtambulisha wa staa wa kimataifa wa Guinea, Balla Moussa Conte mambo hayajapoa kwani tetesi za usajili zimethibitisha kuwa uongozi wa Yanga sasa unaelezwa kuwa umemgeukia mlinzi wa kushoto na nahodha wa Simba, Mohamed Hussein maarufu Tshabalala au ‘Zimbwe Jr’.

‘Kindege’ cha SportPesa kinakupa Mamilioni cheza sasa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.

Aviator banner

Kuhusu utambulisho wa Conte na Yanga

Balla
Balla

Balla Conte amesaini rasmi Yanga mkataba wa miaka miwili na kutambulishwa leo Ijumaa, stori ambayo imekuwa gumzo kubwa kwenye dirisha la usajili. Ikumbukwe ilikuwa ikielezwa kuwa Yanga SC na Simba SC zote zilikuwa vitani kusaka Saini ya nyota huyu wa Guinea.

SOMA HII PIA: Balla Conte amesaini rasmi Yanga SC na kutambulishwa kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26

Vita ilikuwa kubwa kila upande ukifanya umafia wake

Balla Conte rasmi Yanga
Balla Conte rasmi Yanga

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael ameweka wazi kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.

“Kulikuwepo na makubaliano kati ya klabu na klabu (CS Sfaxien na Yanga), ambapo Yanga walipewa Ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga hayajakamilika ndipo usiku Simba walienda na ofa kubwa.

“Kocha mkuu wa Simba, Fadlu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya Simu. Ofa ya Simba kwenda CS Sfaxien ni kubwa sana kuliko Yanga na Fadlu anawapush viongozi wake kumpata kijana kwani ndio chaguo namba moja sokoni.

“Baada ya vita kubwa kati ya Simba na Yanga, usiku wa jana Rais wa Yanga alituma ofa kubwa zaidi kwenda kwa Conte na CS Sfaxien. Ofa hiyo imekubalika na pande hizo mbili, hivyo asubuhi hii dili limekamilika pande zote. Conte ameahidiwa na Yanga kupewa Gari, Nyumba ya kuishi na mshahara mnono.

“Simba waliweka ofa mezani ila changamoto walitaka kulipa hela hiyo kwa awamu mbili, kitu ambacho CS Sfaxien wamekataa, hivyo Yanga wamekubali kulipa hela zote kwa Awamu moja na CS Sfaxien wamekubali biashara.

SOMA ZAIDI HII: Yanga SC imekomalia saini ya Balla Conte | Simba SC vs Yanga SC vitani | Usajili | Wachezaji wapya na wanaoachwa

Ishu ya Tshabalala na Yanga ikoje?

Imeelezwa kuwa Yanga Rasmi Yanga wamefungua mazungumzo na beki na nahodha wa Simba Mohamed Hussein ‘Zimbwe’. Akizungumzia hilo Hans amesema: “Niko hapa kuthibitisha dili la Zimbwe na Yanga bado halijakamilika, ila mazungumzo yanaendelea na yako katika hatua nzuri, hivyo kama watafikia makubaliano basi kiongozi wa Yanga atasafiri kwenda Misri kumsainisha mkataba. Zimbwe kwa sasa ni mchezaji huru, hivyo anaruhusiwa kuzungumza na timu yoyote.”

“Hapa inasubiriwa uamuzi wa mwisho wa mchezaji na wakala wake ambaye anafahamika kama Carlos ‘Mastermind’ ndiye anasimamia michakato yote ya kimkataba ya mlinzi huyo ambaye kwa sasa yuko na majukumu ya kikosi cha timu ya taifa kambini Misri kikijiandaa na mashindano ya Chan.”

Conte, Tshabalala na mipango ya Pre-Season

Baada ya Conte kusaini ‘Tshabalala’ naye anukia Yanga SC Tetesi usajili Ligi Kuu ya NBC
Conte na Kamwe

Huku mchakato wa usajili wa mastaa wa kikosi hiko cha Yanga ukiendelea ambapo tayari Conte ametambulishwa na kukiwa na majina makubwa yanasubiriwa, uongozi wa timu hiyo pia umejitanabaisha kuwa kwenye mipango mikubwa ya maandalizi ya msimu ‘Pre-Season’ kuelekea msimu ujao wa 2025/26.

SOMA HII PIA: Baada ya Conte Yanga SC yatua kwa Tshabalala wa Simba SC Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26

Hitimisho

Kutokana na namna kila timu inaonekana kuwa Siriaz na dirisha hili la uhamisho wa wachezaji, ni wazi kuwa msimu ujao wa 2025/26 unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kwani kila timu inaonekana kujipanga ipasavyo.

Ni wito kwa kila timu kuweka mipango yao sawa kabla ya msimu kuanza, ili kuondokana na malalamiko yanayoweza kujitokeza dhidi ya Mamlaka pasipo ulazima.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.