- Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kusaini Zesco United kwa ajili ya msimu wa 2025/26
- Mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Yanga SC umeisha, atasaini dili jipya akiwa mchezaji huru ikiwa Yanga SC hawamuongezea.
- Simba SC mabosi wake wa zamani wanatajwa kuhitaji kumrejesha nyumbani kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa kutumia mguu wa kulia.
Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kusaini Zesco United ya Zambia.Tetesi zinaeleza hivyo huku ikitajwa kuwa kuna uwezekano akarejea ndani ya Simba SC. Ikumbukwe kwamba kiungo huyo alitambulishwa Yanga SC Julai Mosi 2024 ikiwa ni ingizo jipya kutoka Simba SC.

Soma hii: Chama kutua Yanga, Ali Kamwe atangaza kuna mtu atakula 10
Paisha kindege, uvune mamilioni
Ukicheza Aviator sasa unavuna mamilioni. Ni rahisi sana na ushindi unakusubiri sasa hivi. Cheza ili upate mgao wako wa mihela.

Chama alitambulishwa Yanga SC akitokea ndani ya kikosi cha Simba SC baada ya mkataba wake kuisha. Mkataba wake na Yanga SC ulikuwa ni mwaka mmoja. Chama ameshatumikia timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ya NBC msimu wa 2024/25 mwaka mmoja tayari, hivyo mkataba wake umeisha.
Chama ndani ya Yanga SC

Soma hii: Chama kutua Yanga 2024/25 mazito yaibuka, ukweli wote huu hapa
Msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga SC Chama alicheza jumla ya mechi 24. Ni dakika 957 alizitumia akiwa uwanjani kuvuja jasho. Alifunga mabao 6 ndani ya ligi ya NBC.
Ni pasi tatu za mabao Chama alitoa. Katika mabao sita ambayo alifunga bao moja alifunga kwa mguu wa kushoto, bao moja kwa pigo la kichwa. Ni mguu wa kulia ulifunga jumla ya mabao manne.
Hivyo mguu wenye nguvu kwa Chama kwenye kufunga ni ule wa kulia. Kushoto na mapigo ya kichwa haijawa mara nyingi kwake kutumia akiwa ndani ya uwanja. Msimu wa 2024/25 alianza benchi kwenye mechi zote mbili dhidi ya mabosi wake wa zamani Simba SC.
Alianza balaa lake kwenye fainali Ngao ya Jamii
Kwenye mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii, Chama alianza balaa lake. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa alianzia benchi. Alipoingia alitoa pasi moja ya bao dakika ya 90 ilikuwa dhidi ya matajiri wa Dar, Azam FC.
Mchezo huo ulichezwa Agosti 11 2024. Ilikuwa ni kwenye ufunguzi wa ligi ambapo Yanga SC ilitwaa taji hilo mbele ya Azam FC. Chama alinyanyua taji hilo ikiwa ni msimu wake wa kwanza.
Kimataifa aliendeleza kazi Chama

Soma hii: Aziz Ki, Chama watikisa dirisha la usajili Bongo
Kwenye anga la kimataifa Yanga SC ilikuwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Mchezo dhidi ya Vital’O alipachika bao moja. Ilikuwa ni Agosti 17 2024 Uwanja wa Azam Complex. Chama alifunga bao moja dakika ya 68 akiwa ndani ya 18.
Mchezo wa marudiano kwa mara nyingine dhidi ya Vital’O alifunga. Ilikuwa Uwanja wa Azam Complex dakika ya 50 kwa pigo huru. Mchezo huo ulichezwa Agosti 24 2024 ilikuwa ni hatua ya awali.
Anaingia kwenye orodha ya viungo waliotoa pasi nne za mabao kwenye anga la kimataifa. Ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Vital’O. Alitoa pasi dakika ya 48 akiwa ndani ya 18 alimpa Clement Mzize, dakika ya 70 alitoa pasi kwa Prince Dube.
Pasi ya tatu alitoa kwa Aziz Ki dakika ya 78 na alikamilisha pasi ya nne kwa kiungo mshambuliaji Mudathir Yahya. Mudathir alipachika bao ndani ya nyavu dakika ya 86 kwenye mchezo wa kimataifa. Chama alikuwa nyota wa mchezo huo.
Mbele ya CBE SA Chama alifunga bao moja dakika ya 35. Mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ulichezwa Uwanja wa New Amaan Complex. Septemba 21 2024 ilikuwa ni tarehe ya mchezo huo wa kimataifa.
Chama ndani ya ligi ya NBC
Kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania, Chama alifungua ukurasa wa mabao akiwa na uzi wa Yanga SC. Ilikuwa dakika ya 43 akiwa nje ya 18 kwa pigo huru. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex ilikuwa ni Oktoba 22 2024.
Alifunga mabao mawili kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC. Ilikuwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma Februari 23 2025. Alifunga mabao hayo dakika ya 73 na dakika ya 82.
Fountain Gate aliwafunga bao moja ilikuwa dakika ya 89. Pigo huru kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 liliwaadhibu wapinzani wao Uwanja wa Tanzanite Kwaraa ilikuwa ni Aprili 21 2025. Kwenye mchezo huo pointi tatu Yanga SC walichukua zote.
Aliwafunga Tanzania Prisons bao moja ilikuwa dakika ya 35. Bao hilo lilikuwa ni la tano kwa Chama akiwa na uzi wa Yanga SC. Lilifungwa Uwanja wa Sokoine, Juni 18 2025. Kamba ya sita ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji, dakika ya 4 Uwanja wa New Amaan Complex.
Hitimisho
Clatous Chama akiwa na uzi wa Yanga SC kahusika kwenye mabao 9 kati ya 83 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni pasi tatu alitoa akifunga mabao sita. Yanga SC ni mabingwa wa ligi msimu wa 2024/25.


