Chama na Aziz Ki------------------------------------------------n
CHAMA
 Clatous Chama

SAKATA la kiungo wa kimataifa wa Simba, Clatous Cahma kuondoka ndani ya timu hiyo na kutua kwa watani zao wa jadi Yanga limeingia katika sura mpya ambapo inaelezwa timu hizo mbili kwa sasa ziko kwenye vita kubwa ya kuinasa saini yake.

MKATABA WA CHAMA NA SIMBA UNAISHA LINI?

Mpaka sasa Chama bado ni mchezaji halali wa Simba mpaka Juni 30, mwaka huu ambapo anatarajia rasmi kumaliza mkataba wake wa kuwatumia Wanasimba.

SAKATA HILI LIMEANZIA WAPI?

Taarifa kutoka ndani ya Simba ambazo zimethibitishwa na Meneja wao wa habari na mawasiliano, Ahmed Ally ni kuwa kweli bado hakijaeleweka kati ya Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya michezo ya SportPesa na Simba, mchezaji huyo bado hajamwaga saini ya kuendelea kubaki ndani ya timu hiyo baada ya mazungumzo ya awali ya kusaini mkataba mpya kugonga mwamba.

Mabosi wa Msimbazi wanaonekana bado hawajawa kuwa tayari kukubali kumtekelezea mahitaji aliyohitaji mchezaji huyo.

Utata ulianza kuibuka baada ya mabosi wa Simba kugoma kuongezea ada ya usajili ‘sign on fee’ ambayo kiungo huyo alikuwa anaitaka, ili asaini mkataba wa kuendelea kusalia katika timu hiyo.

Baadhi ya viongozi wa timu hiyo ni kama waliona inatosha na hawapaswi kuendelea na Chama kwa kuwa wanataka kujenga timu mpya itakayokuwa bila ya mchezaji huyo.

Imeelezwa pia kuwa wawakilishi wa Chama pia walitoa mapendekezo ya mshahara mkubwa ambao ungemfanya kuwa miongoni mwa mastaa wanaolipwa fedha nyingi ndani ya timu hiyo kukalibiana na ule ambao alikuwa akilipwa, Luis Miquissone ambaye amepewa ‘Thank You’.

ALICHOSEMA MCHAMBUZI HANS RAPHAEL

Miongoni mwa wadau wa soka ambao walianza mapema kuripoti uhamisho wa Chama ni mchambuzi, Ansbert Raphael ambaye kupitia akaunti yake rasmi ya mtandao wa kijamii wa Instagram aliandika: “Chama atasaini mkataba wa kuitumikia Yanga tarehe 30/06/2024. Chama ana makubaliano na Yanga tangu mwezi January mwaka huu.

“Chama anakwenda kuwa mchezaji wa pili kwa kulipwa mshahara mkubwa nyuma ya Aziz Ki, Chama, Pacome watacheza timu mmoja msimu uajo.”

SIMBA WANAPAMBANA KUPINDUA MEZA

CHAMA 2024/25
Mohammed Dewji

Licha ya taarifa hiyo ya awali, mchambuzi Ansbert ametoa taarifa mpya kuwa Simba inataka kupindua meza juu ya sakata la Chama ambapo ameandika: “Tajiri Mo Dewji ameingilia kati dila Chama kujiunga na Yanga, ambapo amewasiliana na Chama na kuomba kufanya nae kikao Alhamisi hii.

“Baada ya kelele nyingi za mashabiki wa Simba viongozi wa klabu hiyo wameona ni jambo la aibu kuachana na legend wao, hivi sasa wanajaribu kufanya kila liwezekanalo ili kumbakisha Chama ambaye anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Yanga tarehe 30/06/2024 siku ambayo mkataba wake Simba unatamatika.

KUHUSU UWEZEKANO WA CHAMA KUCHEZA NA AZIZ KI KWENYE KIKOSI KIMOJA

CHAMA
Chama (kushoto), Aziz Ki (kulia)

Akizungumzia hilo, Ansbert amesema: “Wote ni namba 10 ila Aziz ni mtu ambaye yupo huru zaidi kufanya maamuzi akiwa na mpira kwani akipokea mali palepale anawaza kupiga mbele ili kuifungua defence ya timu pinzani, ana utashi na nguvu ya kupiga mashuti ndio maana anafunga sana magoli.

“Muda wote Aziz anawataka mawinga na mshambuliaji wake wa mwisho wafanye mikimbiop kila wakati ili pasi zake zisipotee hovyo. Ila Chama ana utulivu zaidi, mara nyingi hupenda kuachia pasi ya uhakika, kwa kifupi anakutesa kabla ya kukuua.

INONGA NAYE APEWA ‘THANK YOU’

CHAMA
Henock Inonga

Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati, Henock Inonga Baka kwenda FAR Rabat inayoshiriki Ligi Kuu nchini Morocco. Kwa mujibu wa Simba, Inonga raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amebakisha Mkataba wa mwaka mmoja unaomalizika 2025 lakini kutokana na klabu kujali maslahi ya wachezaji, wamemruhusu beki huyo kuondoka kwenda kujiunga na Rabat.

Inonga alijiunga na kikosi cha Simba mwaka 2021 akitokea DC Motema Pembe ya Congo.

KUHUSU ISHU YA LAMECK LAWI

CHAMA
Lameck Lawi

Kufuatia kuwepo taarifa za Simba kumalizana na mlinzi wa Coastal Union, Lameck Lawi mchambuzi wa michezo Edward Kumwembe amenukuliwa akisema: “Naweza kuthibitisha kwamba ghafla Coastal walipokea ofa kutoka katika timu moja ya Ubelgiji.

“Kwamba dau ambalo watalipata katika dili hilo ni kubwa kuliko la Simba. Kwamba hata Lawi angepokea mshahara mkubwa kuliko ule anaopokea Aziz Ki Yanga. Angelipwa euro 8,000 (Sh 22m) kwa mwezi. Hata hivyo, unajiuliza, hilo linawahusu nini Simba?

“Simba walipeleka dili lao wakakubaliwa. Mambo ya Ubelgiji yanawahusu nini? Wao walikuwa wameiwahi biashara mapema. Bahati yao. Timu ya Ubelgiji haikuwahusu chochote. Labda tu kama wangeamua kuwa waungwana kwa kumruhusu Lawi aende huko na wao wapate chochote kutoka katika biashara hiyo kwa makubaliano maalumu na Coastal.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.