- Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26, ndiyo habari kubwa kwenye tetesi za usajili kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26.
- Conte ni staa wa kimataifa wa Guinea ambaye anakipiga kwenye klabu ya CS Sfaxien ya Tunisia.
- Katika hatua nyingine Yanga wametangaza Kampeni kubwa ya kuongeza msuli wa kifedha iliyopewa jina la Tofali la Ubingwa.
Moto unazidi kuwaka kuhusu tetesi za usajili Ligi Kuu NBC 2025/26, ambapo sokoni taarifa inayosumbua ni ile ya Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte, kuelekea Ligi Kuu NBC 2025/26 huku Yanga wakianza kwa kishindo kikubwa cha kutangaza kampeni kubwa ya Tofali la ubingwa inayolenga Wanachama kuchangia misuli ya kifedha ya timu hiyo.
Shinda mamilioni na ‘Kindege’ cha SportPesa

Endelea kuhabarika na makala hii, huku pia ukicheza na kushinda mamilioni kupitia mchezo wa aviator maarufu kama Kindege kutoka Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa kwa kubonyeza picha hii chini.
Yanga SC vs Simba SC vitani usajili wa Conte
Ukiachana na majina makubwa yanayotamba sokoni kwa sasa likiwemo la kiungo Mzambia, Clatous Chama habari kubwa kwa sasa ni kuhusu wakongwe hao wa Kariakoo kuingia vitani kwa ajili ya kuisaka saini ya staa wa kimataifa wa Guinea na CS Sfaxien ya Tunisia, Balla Moussa Conte.
SOMA HII PIA: Clatous Chama kiungo wa Yanga SC kusaini Zesco United | Mkataba umeisha | Simba SC yatajwa
Yanga SC yamfuata, Simba SC yapandia juu

Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya usajili, Hans Raphael ameweka wazi kuwa Yanga SC ndiyo ilikuwa timu ya kwanza Bongo kuulizia uwezekano wa kumpata kiungo huyo, kabla ya Simba kumpandia dau baada ya maelekezo ya kocha wao mkuu, Fadlu Davis.
“Jana mchana kulikuwepo na makubaliano kati ya klabu na klabu (CS Sfaxien na Yanga), ambapo Yanga walipewa Ruhusa ya kuzungumza na mchezaji Conte, kabla makubaliano ya mchezaji na Yanga hayajakamilika ndipo usiku wa Jana Simba walienda na ofa kubwa.
“Kocha mkuu wa Simba, Fadlu amefanya mazungumzo ya moja kwa moja na mawakala wa mchezaji kwa njia ya Simu. Ofa ya Simba kwenda CS Sfaxien ni kubwa sana kuliko Yanga na Fadlu anawapush viongozi wake kumpata kijana kwani ndio chaguo namba moja sokoni.
“Yanga nao wanapush kukubaliana na mchezaji, Ila kwa sasa Balla Moussa Conté, amelalia Simba hii ni Baada ya kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na Fadlu,” amesema Hans.
SOMA HII PIA: Tetesi usajili Ligi Kuu NBC 2025/26: Straika mpya Yanga huyu hapa, Chama ‘Out’
Yanga watangaza Tofali la ubingwa

Katika hatua nyingine uongozi wa Yanga umetangaza Kampeni kubwa ya kuongeza msuli wa kifedha wat imu hiyo kupitia mtaji wa Wanachama ambayo inaenda kwa jina la Tofali la Ubingwa. Kampeni hii imezinduliwa rasmi leo Ijumaa na Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe.
Akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni hiyo, Ali Kamwe amesema: “Nyumba yetu ya mwaka 2024/25 imeshamalizika na sasa tunataka kujenga nyumba mpya ya Ubingwa ya 2025/26, Nyumba hii haiwezi kujengwa kwa kitu kingine isipokuwa nguvu kubwa ya Kiuchumi na ndiyo maana leo hii tunazindua kampeni ya Tofali la UBINGWA.
“Tofali hili la Ubingwa ni Ada yako ya Uanachama Mwananchi mwenzangu na huu ndiyo wakati wa kulipa Ada zetu ili kuijenga Yanga imara. Kipindi hiki ndiyo kipindi muhimu kwelikweli kwenye kuijenga Timu yetu, hiki ndicho kipindi cha kuseti mafanikio ya Ubingwa wa mwaka 2025/26.
“Kwa mantiki hiyo klabu yetu inapaswa kuwa na misuli mikubwa ya kifedha, hili ni Jukumu letu sote Wananchi kwa kulipa Ada zetu za mwaka za Uanachama, hakuna muujiza utakaotokea pasipo na sisi kujiandaa vizuri.
“Na hii ndiyo sababu sisi kama klabu kuanzisha kampeni hii ya Tofali la Ubingwa, kwahiyo kila mtu aweke Tofali lake ili tuijenge Nyumba tunayoitaka, kwa ajili ya msimu mpya wa 2024/25.
SOMA HII PIA: Ellie Mpanzu kusaini RS Berkane ama Yanga SC | Simba SC yatoa masharti mazito | Magoli na rekodi zake CAF
Tofali la ubingwa kuvuka mipaka ya Afrika
Kampeni hii ndugu zangu siyo ya Dar Es salaam, siyo Dodoma, siyo Kigoma pekee, ni Kampeni ya duniani kote kuhakikisha tunaipa nguvu klabu yetu ili tuweze kufikia malengo tunayojiwekea.
“Tukikosea hapa mwanzoni kwenye kuijenga timu yetu basi tutakuwa tumekosea msimu mzima, hiki ni kipindi muhimu sana Mwananchi, nafasi ya kuijenga Yanga bora ndiyo hii ndugu zangu basi kila mtu aitumie nafasi hii kuandaa Parade lijalo la Ubingwa.
“Tofali la ubingwa la mwaka 2025/26 linauzwa shilingi 24,000/= pekee, lengo letu ni kukusanya matofali milioni 1 ndani ya miezi hii miwili, najua tupo Wananchi wengi hapa duniani, tukianza na Tanzania tu tunaweza kufika mpaka Milioni 40.”
Hitimisho safari ya Rwanda kujiandaa na msimu ‘Pre-season’
Tukifanikisha matofali haya maana yake tutakuwa na Yanga imara itakayofanya maandalizi bora kuanzia Pre Season mpaka kutimiza malengo yetu kwa msimu mzima. Nataka kuwaambia kuwa tumejipanga vizuri kuhakikisha tunatetea ubingwa msimu ujao.
“Tayari tumepata mwaliko wa kwenda Rwanda kwa ajili ya kushiriki siku ya kilele cha klabu ya Rayo Sports na napenda kuwahakikishia kuwa tutashiriki, na tutawatangazia mapema wanachama safari hiyo.”

