- Pacome Zouzoua kiungo wa Yanga SC na Jean Ahoua wa Simba SC vita yao ya nani mkali iliisha kibabe Uwanja wa Mkapa Juni 25 2025.
- Aziz Ki alitwaa tuzo ya MVP mwaka uliopita, na mwaka huu ipo baina ya wababe wawili wa Yanga na Simba SC.
- Pacome kahusika kwenye mabao 22 na Yanga SC ni bingwa, Ahoua kahusika kwenye mabao 25 Simba SC nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.
Pacome Zouzoua na Jean Ahoua nani mkali? Vita yao waliimaliza kibabe Juni 25 2025. Wababe hao walikutana kwenye Kariakoo Dabi mzunguko wa pili 2024/25. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Mastaa hawa wanapewa chapuo majina yao kuwania tuzo ya Most Valuable Player, (MVP) kazi ipo kumpata mrithi wa Aziz Ki aliyetwaa tuzo hiyo 2023/24.
Muda wa kuvuna mamilioni ni sasa na Aviator
Muda ni sasa kuvuna mamilioni. Haihitaji siku ndefu ila dakika mkwanja unavuna. Ni sasa vuna mamilioni kwa kupaa na kindege.


Simba SC yapoteza nje ndani mbele ya Yanga SC
Simba SC kwa msimu wa 2024/25 ilipoteza nje ndani mbele ya Yanga SC. Mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga SC na mzunguko wa pili ilikuwa Yanga SC 2-0 Simba SC. Pointi sita Yanga SC walivuna mbele ya Simba SC.
Vita yao ilikwisha namna hii kwa Mkapa

Soma hii: Yanga SC waifunika Dar kw Paredi la ubingwa la kihistoria
Vita ya viungo Pacome na Ahoua iligota mwisho kwa Mkapa. Ni Pacome aliibuka shujaa kwenye mchezo huo akihusika kwenye mabao yote yaliyofungwa na Yanga SC. Alifunga bao moja kwa penati na alitoa pasi ya bao kwa Clement Mzize.
Rekodi zinaonyesha kuwa Pacome Zouzoua ndani ya Yanga SC iliyofunga mabao 83 amehusika katika mabao 22. Amefunga mabao 12 na kutoa pasi 10 za mabao. Ni dakika 1,626 katumia. Kacheza jumla ya mechi 26 kati ya 30 ambazo Yanga SC imecheza.
Pacome amekosekana kwenye mechi nne pekee kati ya 30. Ni chaguo la kwanza la Miloud kwenye mechi za ushindani za ligi. Mchezo raundi ya 29 dhidi ya Tanzania Prisons alifunga mabao mawili na alianza kikosi cha kwanza. Mchezo wa raundi ya 30 aliaza kikosi cha kwanza dhidi ya Dodoma Jiji.
Kwenye mabao 12 ambayo Pacome amefunga mabao mawiili kwa penati. Ukurasa wa penati ulifunguliwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa KMC Complex mlinda mlango wa Kagera Sugar alikuwa ni Ramadhani Chalamanda. Penati ya pili ilikuwa dhidi ya Simba SC, Uwanja wa Mkapa.
Kwenye mchezo dhidi ya Simba SC, Pacome alianza kikosi cha kwanza. Alikomba dakika zote 90 mbele ya mtani wa jadi. Alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Mbele ya Kagera Sugar na Simba SC ambazo Pacome alifunga kwa penati pointi zilibaki Jangwani. Mbele ya Kagera Uwanja wa KMC Complex na mbele ya Simba SC Uwanja wa Mkapa. Mguu wakewa maangamizi ni ule wa kulia.
Huyu hapa Jean Ahoua wa Simba SC

Simba SC ni Jean Ahoua amehusika katika mabao 25. Simba SC imefunga jumla ya mabao 69. Ni pasi 9 kateneneza akifunga mabao 16. Ni kinara katika chati ya wafungaji ndani ya NBC Premier League.
Ahoua amecheza jumla ya mechi 28 kati ya 30 akikosekana katika mechi mbili ambazo ni dakika 180. Katika mabao 16 aliyofunga kafunga mabao 6 kwa penalti. Penalti yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Dodoma Jiji.
Ni Mohamed Hussen alisababisha penati hiyo kipindi cha pili. Ahoua alifunga penati hiyo kwa mguu wake wa kulia. Rekodi zinaonyesha kuwa Ahoua kafunga mabao 15 kwa mguu wa kulia na bao moja kwa pigo la kichwa.
Camara apotezwa mazima mbele ya Diarra

Soma hii: Aziz Ki atarejea Yanga SC
Kwenye kukusanya hati safi katika Kariakoo Dabi, kipa wa Simba SC kapotezwa na yule wa Yanga SC. Djiguia Diarra kipa namba moja wa Yanga SC kampoteza Moussa Camara wa Simba SC. Dakika 180 zote shujaa alikuwa ni Diarra.
Camara anaongoza kwa hati safi akiwa nazo 19 kibindoni. Camara ni mechi 28 amekaa langoni akifungwa mabao 13. Mechi mbili Ally Salim alikaa langoni kwa Simba SC na hakufungwa. Amekomba dakika 2,520 Camara.
Diarra ni mechi 23 alikaa langoni ametumia dakika 2,070 ni hati safi 17 kakusanya akifungwa mabao 8. Juni 22 2025 hakuwa langoni dhidi ya Dodoma Jiji, Aboutwalib Mshery alikaa langoni. Baada ya dakika 90 ilikuwa Yanga SC 5-0 Dodoma Jiji.

Soma hii: Uongozi wa Yanga SC umeweka wazi vita ya MVP
Ni muda wetu wakukunja mamilioni kwa kupaa na kindege. Aviator Challenge inakupa fursa yakuvuna mamilioni kwa kupaa sasa. Cheza kila siku uwahi mgao wa mamilioni.
Yanga SC bingwa 2024/25
Yanga SC ni mabingwa wa ligi ya NBC msimu wa 2024/25. Tofauti yao ni pointi nne na watani zao wa jadi ambao ni Simba SC. Yanga SC imekamilisha msimu ikiwa na pointi 82, Simba SC pointi 78.


