Ateba na DiarraAteba na Diarra
  • Yanga SC vs Simba SC kwenye msako wa pointi tatu ndani ya ligi Juni 18 2025 ndani ya dakika 90.
  • Mechi namba 184, Yanga SC vs Simba SC ni kimebembe imeyeyuka mara mbili ndani ya msimu wa 2024/25.
  • Ubingwa wa ligi jasho litamwagika wababe Yanga SC vs Simba SC tofauti yao ni pointi moja.

Yanga SC vs Simba SC kwenye msako wa pointi tatu ndani ya ligi Juni 18 ndani ya dakika 90 ikiwa ni mzunguko wa pili. Wababe hawa ambao kila mmoja anapambania ubingwa watakuwa kazini kwenye viwanja tofauti.

Ateba v Aucho
Ateba v Aucho kwenye mchezo wa ligi mzunguko wa kwanza. Source: Simba SC.

Soma hii: Yanga SC vs Simba SC ni Juni 25 2025 sio Juni 15 2025

Yanga SC itakuwa kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya saa 10:00 jioni kwenye msako wa pointi tatu muhimu ikiwa ni mzunguko wa pili na Simba SC watakuwa wakisaka pointi tatu dhidi ya KenGold, Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Simba SC imeachwa na Yanga SC kwa pointi moja kwenye msimamo hivyo wababe hawa vita yao inaendelea ndani ya uwanja mpaka mwisho wa msimu itakapofahamika nani atakuwa bingwa wa ligi kwa msimu wa 2024/25.

Kituo kinachofuata kwa Simba SC

Fadlu -
Fadlu, Kocha Mkuu wa Simba SC: Source: Simba SC.

Soma hii:Ibenge & Maxi watikisa taarifa mpya usajili Bongo

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Simba SC kituo kinachofuata ndani ya Ligi Kuu Bara ni mchezo dhidi ya KenGold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ikiwa ni mzunguko wa pili. Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wababe hawa wawili walipokutana Desemba 18 2024, ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 2-0 KenGold. Pointi tatu zilikuwa mali ya Simba SC.

Wanakutana mzunguko wa pili wababe hawa wawili kila timu ikiwa na malengo yake kwenye hesabu za kusaka pointi tatu muhimu. KenGold wenyeji mpango mkubwa ni kulipa kisasi kutokana na kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza huku Simba SC wakiwa na hesabu za kuvuna pointi tatu kwa ajili ya kutwaa ubingwa.

Simba SC yenyewe inapambania ubingwa na watani zao wa jadi Yanga SC ambao nao watakuwa kazini Juni 18 kwenye msako wa pointi tatu dhidi ya Tanzania, Prisons, Mbeya Uwanja wa Sokoine kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Mchezo wa mwisho kwa Simba SC kwenye ligi

Mukwala Vs Singida BS
Mukwala akiwa kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars Uwanja wa KMC. Source: Simba SC.

Soma hii:Mechi namba 184 Yanga SC vs Simba SC ni pasua kichwa

Simba SC mchezo wake wa mwisho kwenge ligi ilikuwa dhidi ha Singida Black Stars uliochezwa Uwanja wa KMC Complex na mwisho ubao ulisoma Simba SC 1-0 Singida Black Stars.
Mchezo huo ulichezwa Mei 28 2025 na mfungaji wa bao la ushindi alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo alipotumia pasi ya kiungo chaguo la kwanza la Fadlu, Jean Ahoua ambaye anafikisha jumla ya pasi 8 za mabao ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.


Bao pekee la ushindi katika mchezo huo lilifungwa na mshambuliaji Steven Mukwala. Nyota Mukwala ndani ya ligi anafikisha jumla ya mabao 12 ikiwa ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye eneo la ushambuliaji wakishirikiana na Leonel Ateba.

Msimamo wa KenGold vs Simba SC


KenGold kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 16 ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi 28 msimu wa 2024/25. Nafasi iliyopo kwa KenGold nim baya jumlajumla kwa kuwa haitakuwa na nafasi kushiriki ligi msimu wa 2025/26 baada ya kushuka daraja.

Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili pointi 72 baada ya mechi 27 ikiwa inapambania kutwaa ubingwa mbele ya Yanga SC ambao ni vinara wenye pointi 73. Tofauti ya wababe hawa wawili ni pointi moja pekee wakiwa wamecheza mechi ambazo ni sawa kwa kila mmoja.

Kwa upande wa mabao Simba SC imefunga mabao 63 inakutana na KenGold ambayo imefunga jumla ya mabao 22. KenGold reodi zinaonyesha kuwa safu yake ya ushambuliaji haijawa imara kwenye mechi za ushindani. Mbali na kufunga mabao machache KenGold imeruhusu mabao 52 yakufungwa ikiwa ni timu namba mbili kuruhusu mabao mengi yakufungwa ndani ya ligi vinara wakiwa ni Fountain Gate ambao wameruhusu jumla ya mabao 54.

image

Simba SC ni timu namba mbili kuruhusu mabao machache ambayo ni 11 baada ya mechi 27. Mabao yote hayo katunguliwa kipa namba moja wa Simba SC Moussa Camara ambaye kacheza jumla ya mechi 25 na mechi mbili ni Ally Salim alikaa langoni.

Mchezo namba 184 uliyeyuka tena


Mchezo ambao ulitarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 ambao ulikuwa ni Kariakoo Dabi, Yanga SC vs Simba SC mchezo namba 184 umepelekwa mbele na sasa utachezwa Juni 25 kwa wababe hawa kukutana uwanjani katika msako wa pointi tatu muhimu.

Kariakoo Dabi imeyeyuka kwa mara ya pili ndani ya msimu wa 2024/25, mara ya kwanza ilikuwa ni Machi 8 2025 ukapangiwa tarehe nyingine ambayo ni Juni 15 2025 Juni 13 2025 ukayeyuka kwa mara nyingine unatarajiwa kuchezwa Juni 25 2025, Uwanja wa Mkapa.

Share this: