- Hamza arejesha mzuka Simba SC vs RS Berkane, hii ni baada ya taarifa kuwa kitasa huyo amerejea mazoezini kujiandaa na fainali ya 25/05/2025.
- Hamza alitolewa Uwanjani dakika ya 21 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Mlinzi wa kimataifa wa Cameroon, Che Malone Fondoh ambaye alirejea ukiwa ni mchezo wake wa pili tangu alipoumia mwezi Februari.
- Simba wataikaribisha RS Berkane Jumapili ya Mei 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Mlinzi wa kimataifa wa Simba, Abdalazak Hamza arejesha mzuka Simba vs RS Berkane mara baada ya kuonekana akishiriki mazoezi ya kikosi cha timu hiyo kinachojiandaa na mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho utakaopigwa 25, Mei mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Hamza alizua hofu baada ya kuumia na kutolewa Morocco

Hamza alizua hofu miongoni mwa mashabiki wa Simba ikiwa angeweza kuwa sehemu ya mchezo wa Jumapili hii, mara baada ya kushindwa kumaliza mchezo na kutolewa kipindi cha kwanza cha mchezo huo mara baada ya kupata maumivu.
Nyota huyo alitolewa Uwanjani dakika ya 21 ya mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Mlinzi wa kimataifa wa Cameroon, Che Malone Fondoh ambaye alirejea uwanjani ukiwa ni mchezo wake wa pili tangu alipoumia kwenye mchezo dhidi ya Azam mwezi Februari.
SOMA HII PIA: JKT Tanzania FC Vs Simba SC 5/5/2025: Mabosi Simba wafanya kikao kizito cha Ubaya ubwela
Fadlu kichwa kuwaka moto

Kurejea kwa, Hamza kunafanya kocha mkuu wa Simba, Fadlu Davis kukuna kichwa juu ya nani na nani wanaweza kuanza katika mchezo huo wa Jumapili, ambapo mara kadhaa amekuwa akiwatumia kwa utofauti Hamza, Che Malone na Chamou Karabou.
Simba vs RS Berkane: “HII TUNABEBA.”

Uongozi wa Simba umeendelea kutamba kuwa wanakwenda kupindua meza kuifunga zaidi ya mabao mawili Berkane na kubeba ubingwa wa mashindano hayo ya pili kwa ukubwa barani Afrika.
Akizungumzia mchezo huo Meneja wa habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesem: “Mashabiki 16,000 walikuwa tayari wamenunua tiketi kwa ajili ya kushuhudia mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
“Kutokana na mazingira ya kubadilishwa Uwanja, sasa tiketi zao zitatumika katika Tamasha la Simba Day. Uwanja wa Amaan Zanzibar ambao utapigwa fainali hiyo unaingiza mashabiki 15,000 pekee hivyo tayari kuna watu 10,000 ambao wasingekuwa na nafasi.
“Hivyo tumeamua kuzitumia kwenye tamasha la Simba Day, na tunawaomba mashabiki wetu wazitunze hadi itakapofika siku ya Tamasha la Simba Day.
“Uongozi ulikuwa unapambana kuhakikisha mchezo unapigwa Benjamin Mkapa lakini ilivyoshindikana imebidi tusitishe zoezi la kuuza tiketi, huku walionunua wakiwa ni wengi zaidi ya uwezo wa uwanja wa Amaan Zanzibar,” amesema Ahmed.
SOMA HII PIA: Simba SC wanautaka ubingwa wa CAF, kuwavutia kasi RS Berkane Zanzibar, Mei 25 2025 fainali ya maamuzi
Unaiona Simba SC vs RS Berkane kwa Shilingi ngapi?
Katika hatua nyingine, Ahmed Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo wa Mei 25, mwaka huu ambavyo ni kama ifuatavyo; VIP A Sh. 50,000 Jukwaa la Urusi 30,000 Mzunguko Sh. 10,000. Tayari tiketi zimeanza kuuzwa kwa njia ya mtandao.
Wanaotaka kuiona Simba SC vs RS Berkane kwa ndege wamefikiwa

Ahmed ameongeza kuwa kutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi siku ileile ya mchezo, ambayo gharama yake itakuwa Shilingi 350,000.
“Tutakuwa na usafiri wa Ndege wa kwenda na kurudi na mashabiki watakaolipa kiasi hicho watapata tiketi za VIP A, jezi za fainali pamoja na usafiri wa kutoka na kurudi Uwanja wa Ndege,” amesema Ahmed.
Tujikumbushe sakata la Uwanja wa Benjamin Mkapa
Ikumbukwe hapo awali mchezo huo ulitarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa na tayari mchakato wa kuanza kuuza tiketi za mchezo huo zilianza kuuzwa.
Wakati mchaakato wa mauzo ya tiketi ukiendelea kwa mshituko mkubwa taarifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Mei 14 kupitia ripoti ya wakaguzi huru wa kimataifa walibatilisha ubora wa dimba la Mkapa na kuamuru mchezo huo uchezwe Uwanja wa Amaan.
CAF walibainisha kuwa sababu kubwa ni sehemu ya kuchezea ya Uwanja wa Mkapa ‘pitch’ kutofikia viwango ambavyo vinatakiwa kuelekea kwenye fainali na hivyo kuelekeza mchezo uchezwe Zanzibar.
Licha ya jitihada za Serikali, Simba SC na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kupambania mchezo uchezwe Uwanja wa Mkapa kutokana na maboresho ambayo yamefanyika kwenye uwanja huo bado msimamo wa CAF ulibaki palepale.

