KarabakaKarabaka
  • Jonathan Nahimana kipa wa Namungo FC aliokoa michomo zaidi ya 10 kwenye lango kutoka kwa wachezaji wa Yanga SC.
  • Aziz Ki kombora lake lilikuwa la maajabu kutoka kwenye miguu ya mchezaji huyo anayevaa jezi namba 10 mgongoni.
  • Bakari Nondo beki wa Yanga SC alikula sahani moja na staa wa Namungo FC, aliokoa hatari zaidi ya tano kuiweka ngome yao salama dakika 90 alizovuja jasho.

Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Namungo FC ilikomba pointi tatu jumlajumla huku wachezaji wa timu zote mbili wakiandika rekodi zao uwanjani.

Bakari
Bakari nahodha wa Yanga SC 2024/25. Source: Yanga SC.

Hapa tunakuletea rekodi za baadhi ya wachezaji kile ambacho walifanya Uwanja wa KMC Complex walipokuwa wakivuja jasho huku beki wa Yanga SC, Bakari Nondo akiwa miongoni mwa mabeki waliofanya kazi ngumu.

Ukiweka kando Nondo, Jonathan Nahimana alifanya kazi kubwa kuokoa kichapo zaidi na nyota wa mchezo huo alikuwa ni Maxi Nzengeli, hapa tunakuletea rekodi wachezaji wa Yanga SC na Namungo FC namna hii:-

Wafungaji mabao mchezo wa Yanga SC 3-0 Namungo FC

Prince Dube vs Namungo FC
Prince Dube na Kibwa Shomari kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC. Source: Yanga SC.

Aziz Ki alipachika bao la ufunguzi dakika ya 26, kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 akitumia pasi ya Maxi Nzengeli, bao la pili lilifungwa na Prince Dube dakika ya 30 ndani ya 18 akitumia pasi ya Kibwana Shomari.

 Bao la tatu kwa Yanga SC lilifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 72 akiwa ndani ya 18 kwa pasi ya Israel Mwenda ambaye huyu alianzia benchi, aliingia akichukua nafasi ya Kibwana Shomari.

Rekodi kwa wachezaji mchezo wa Yanga SC 3-0 Namungo FC

Diara wa Yanga SC na Nahimana wa Namungo FC

Kipa wa Yanga SC, Djigui Diara alikomba dakika 90 na aliokoa hatari dakika ya 9 kutoka kwenye miguu ya Fabrince wa Namungo FC ambaye alipata maumivu dakika ya 35 alikwama kukamilisha dakika 90.

Kipa wa Namungo FC, Jonathan Nahimana ambaye alianza kikosi cha kwanza licha ya kutunguliwa mabao matatu, mikono yake ilikuwa kwenye kazi kubwa aliokoa hatari dakika ya 19, 20, 24, 31, 38 double save dakika ya 45. Kipindi cha pili aliendelea kazi yake langoni akiokoa hatari dakika ya 46, 47, 67, 70, 90.

Mudathir Yahya

Mudathir Yahya, kiungo wa Yanga SC alitoa pasi fupi dakika ya 40 aliokoa hatari dakika ya 43 alipiga krosi dakika ya 61 alikomba dakika 66 nafasi yake ilichukuliwa na Aziz Andambwile.

Prince Dube

Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC alipachika bao moja dakika ya 30 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 45, alicheza faulo dakika ya 46. Bao hilo mbele ya Namungo FC linamfanya afikishe mabao 13. Aligotea dakika ya 78 nafasi yake aliingia Kennedy Musonda.

Kibabage

Nickson Kibabage wa Yanga SC alitoa pasi dakika ya 8, alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 16 alicheza faulo dakika ya 4, alipiga krosi dakika ya 46.

Mzize

Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC cheza faulo dk 3, otea dk 4, 9, chezewa faulo dk 31 na Kabunda, alicheza faulo dakika ya 67, aligotea dakika ya 78 nafasi yake aliingia Dennis Nkane.

Dickson Job

Dickson Job aliokoa hatari dakika ya 6, 14 alikomba dakika zote 90.

Bakari Nondo

Bakari Nondo, aliokoa hatari dakika ya 3, 4, 8, 18, 40 alichezewa faulo dakika ya 11, alicheza faulo dakika ya 35 kwa Fabrince na alionyeshwa kadi ya  njano dakika ya 35, aliokoa hatari dakika ya 55.

Aziz Ki

Aziz Ki alipiga faulo dakika ya 6, alipiga kona dakika ya 16, 19, alifunga bao dakika ya 26 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 31, alipiga faulo dakika ya 45,58 alikomba dakika 60 nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama.

Maxi Nzengeli

Maxi Nzengeli
Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC. Source: Yanga SC.

Maxi Nzengeli alicheza faulo dakika ya 6, alipiga kona dakika ya 25, 45, alitoa pasi ya bao dakika ya 26 alimpa Aziz Ki, alikokota mpira dakika ya 40 alipiga kona dakika ya 70, alipachika bao moja kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18.

Kibwana Shomari

Kibwana Shomari alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 14, 20, aliokoa hatari dakika ya 19, 42 alitoa pasi ya bao dakika ya 30 alimpa Dube. Kibwana Shomari aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Israel Mwenda, aliyetoa pasi ya bao kwa Maxi.

Hawa hapa nyota wa Namungo FC

Ukiweka kando Jonathan Nahimana ambaye alianza langoni kwa kuokoa hatari zaidi ya 10 akifungwa mabao matatu, vijana wa Namungo FC walikuwa kazini.

Saleh Karabaka alichezewa faulo dakika ya 10, alicheza faulo dakika ya 11, alipiga kona dakika ya 23.

Fabrice alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 9 alichezewa faulo dakika ya 36 na Nondo alikwama kukamilisha dakika 90 nafasi yake ilichukuliwa na Meddie Kagere.

Hassan Kabuda alichezewa faulo na Mzize dakika ya 3, 22, Kabuda aligotea dakika ya 50 nafasi yake ikachukuliwa na Jacob Masawe ambaye ni nahodha.

Share this: