Stellenbosch Vs SimbaStellenbosch Vs Simba

  • Stellenbosch FC Vs Simba SC ni mechi inayosubiriwa na mamilioni ya Watanzania na Wanasimba kote Duniani.
  • Mechi hii ya marudiano itapigwa leo Jumapili saa 10:00 jioni nchini Afrika Kusini.
  • Simba wanahitaji angalau matokeo yoyote ya sare ikiwemo 0-0 kufuzu Fainali.

Stellenbosch FC Vs Simba SC ‘live’ saa 10:00 jioni ndio habari kubwa ya soka wikiendi hii, ambapo Kikosi cha Simba kitakuwa mgeni nchini Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa marudiano Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch.

Mchezo huo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa, Moses Mabhida ni mchezo unaotarajiwa kufuatiliwa na mamilioni zaidi kutokana na matokeo ya mchezo wa kwanza uliopigwa Tanzania na kumalizika kwa suluhu yaani 0-0.

KOCHA SIMBA ATOA TAMKO ZITO KUELEKEA STELLENBOSCH FC Vs SIMBA SC ‘LIVE’ SAA 10:00 LEO

Coach Fadlu
Coach Fadlu

Kocha Mkuu wa Simba , Fadlu Davids ameweka wazi kuwa mchezo wa leo wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch utakuwa mgumu zaidi ya ule kwanza walioshinda bao 1-0 nyumbani Tanzania.

Fadlu amesema Stellenbosch ni timu ambayo haichezi kwa kumiliki mpira, lakini inafanya mashambulizi ya kushtukiza pamoja na kurusha mipira kuelekea golini jambo ambalo Simba inapaswa kuchukua tahadhari.

Akizungumzia hali ya kikosi chake, Fadlu amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri na wataingia katika mchezo wa leo Stellenbosch FC Vs Simba SC ‘LIVE’ saa 10:00 kwa malengo ya kutafuta bao la ugenini, huku wakiwa makini kwenye kuzuia wasiruhusu bao.

“Itakuwa mechi (Stellenbosch FC Vs Simba SC ‘LIVE’ saa 10:00) ngumu lakini, malengo yetu ni kuhakikisha tunavuka na kutinga fainali. Tunahitaji sare ya aina yoyote kama ikishindikana kabisa hata bila kufungana lakini tumejipanga kutafuta bao la ugenini ili kuwapa wakati mgumu wapinzani.”

KOCHA SIMBA AWAONYA MASTAA WAKE

Kocha Fadlu amendelea kusema: “Makosa tuliyokuwa tunafanya kuanzia hatua ya awali, makundi mpaka robo fainali yamepungua kwa kiasi kikubwa na tupo tayari kwa ajili ya malengo yetu kama timu ya kuvuka hatua hii.

“Hatupaswi kufanya makosa ambayo yanaweza kutugharimu, tunahitaji kucheza kwa umakini,” amesema Fadlu.

MUKWALA ASEMA WACHEZAJI WANAITAKA FAINALI

Hatuishii Hapa- #TunaitakaFainali #WenyeNchi #NguvuMoja
Mukwala na Camara

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji Simba, Steven Mukwala amesema katika mchezo wa mkondo wa kwanza waliibuka na ushindi wa bao moja lakini wanahitaji kushinda zaidi leo Stellenbosch FC Vs Simba SC ‘LIVE’ saa 10:00 ili kutinga fainali.

“Bado kuna dakika 90 za kupambana kwenye mchezo wa leo (Stellenbosch FC Vs Simba SC ‘LIVE’ saa 10:00) ili kufikia malengo yetu tuliyojiwekea. Bao moja tuliloshinda nyumbani hatuwezi kusema limetuvusha moja kwa moja tupo tayari kupambana hadi mwisho kuona tunaweza kufika fainali,” amesema Mukwala.

MCHEZO WA KWANZA ULIKUWAJE?

Ahoua v Stellenbosch FC
Mpanzu Vs Stellenbosch

Wenyeji waliuanza mchezo kwa kasi na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umaliziaji haukuwa mzuri huku Stellenbosch wakitumia muda mwingi kujilinda na kafanya mashambulizi ya kushtukiza.

Jean Charles Ahoua aliipatia bao hilo pekee dakika ya 45 baada ya kupiga mpira wa adhabu uliotinga wavuni moja kwa moja na kuwashinda walinzi wa Stellenbosch.

Kipindi cha pili Simba hatakurudi kwa kasi kama ilivyokuwa cha kwanza, huku Stellenbosch nao wakipata nafasi ya kufanya mashambulizi ingawa wenyeji walikuwa imara kuwadhibiti.

Ahoua alipoteza nafasi nzuri ya kuipatia bao la pili dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kumpiga hadi chenga mlinda mlango, Oscarine kufuatia pasi safi ya Mpanzu lakini mpira aliopiga ulitoka nje kidogo ya lango.

KIKOSI CHA SIMBA KINACHOTARAJIA KUANZA MCHEZO WA LEO

Stellenbosch FC Vs Simba SC 'LIVE' SAA 10:00
Kikosi cha Simba

Kuelekea mchezo wa leo, haitarajiwi kuona kocha Simba akifanya mabadiliko makubwa ya kikosi kulinganisha na kile kilichocheza mchezo wa kwanza hivyo kikosi kinachotarajiwa kuanza ni:

Camara, Kapombe Zimbwe Jr, Chamou, Hamza, Kagoma, Kibu Ngoma, Mukwala, Ahoua, Mpanzu.

SIMBA: “KWETU KAMA KWAO”

Licha ya kuwa ugenini Simba wametamba kuwa wanajisikia kuwa nyumbani kutokana na sapoti kubwa ambayo wamepewa na Serikali, mashabiki wa timu hiyo waliosafiri na wale wanaoishi nchini humo

MAMBO MUHIMU KUHUSU STELLENBOSCH FC Vs SIMBA SC ‘LIVE’ SAA 10:00 LEO

  • Timu hizo mbili zimekutana kwa mara ya kwanza katika historia yao mwaka huu ambapo mchezo wa kwanza uliopigwa Tanzania visiwani ulimalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa Simba.
  • Simba na Stellenbosch wote wameandika rekodi ya kucheza hatua hiyo ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza Katika historia ya timu hizo.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.