Yanga SC yatinga Nusu FianaliYanga SC yatinga Nusu Fianali

  • Simba ndio mabingwa watetezi wa mashindano hayo, ubingwa ambao waliutwaa msimu uliopita wa 2023/24 chini ya kocha Abdelhak Benchikha.
  • Mashindano hayo yanashirikisha timu 8 msimu huu, 4 kutoka Tanzania Bara na 4 kutoka Tanzania Visiwani.
  • Yanga kuvaana na Zimamoto katika mchezo wa Nusu Fainali.

Yanga sc yatinga Nusu fainali Muungano cup 2025, hii ni baada ya Wananchi kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali dhidi ya KVZ.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani wa aina yake ulipigwa kwenye Uwanja wa Gombani, Zanzibar usiku wa kuamkia leo Jumapili ya Aprili 27, mwaka 2025.

JESHI LA WACHEZAJI TU 25 LA YANGA KUPAMBANIA KOMBE

Jonathan na Mzize
Baadhi ya wachezaji wa Yanga

Yanga SC waliwasili visiwani Zanzibar tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Muungano 2025. Ambapo Kikosi cha Yanga kilikuwa kikiongozwa na kocha na wachezaji 25, pamoja na sehemu ya benchi la ufundi wakiwa na lengo la kuonyesha ushindani mkali dhidi ya timu nyingine kubwa.

MCHEZO ULIKUWAJE?

--’- #MuunganoCup KVZ FC --- Young Africans SC#TimuYaWananchi #DaimaMbeleNyumaMwiko
Aziz Ki akipambana na mchezaji wa KVZ

Licha ya matokeo hayo ya ushindi wa mabao 2-0 Yanga SC katika mchezo huo wa Robo Fainali, Yanga SC walionyesha kiwango cha juu cha soka, wakitawala sehemu kubwa ya mchezo huo.

 Ushindi huo wa Yanga ulichagizwa na mabao ya Stephanie Aziz Kin na Denis Nkane ambapo kila mmoja alifunga bao moja. Ushindi huu unawafanya Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025. ​

KUVAANA NA ZIMAMOTO NUSU FAINALI

Baada ya Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025, sasa mabingwa hao watetezi wanatarajia kuvaana na kikosi cha Zimamoto katika mchezo wa Nusu Fainali ambao unasubiriwa kwa hamu na mamilioni ya mashabiki wa soka nchini.

Ikumbukwe Zimamoto wao walikata tiketi ya kucheza Nusu Fainali baada ya kuwaondosha Coastal Union kwa ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa Robo Fainali ya mapema.

ZILIZOFUZU NUSU FAINALI YA MUUNGANO 2025

LUSAJOOO! ️--' KMKM --- Azam FC#muunganocup---- #weareazamfc #timuborabidhaabora
Kikosi cha Azam

Mpaka sasa Robo Fainali zote 4 za mashindano hayo zimekamilika ambapo wamepatikana washindi wanne ambao watavaana katika hatua ya Nusu Fainali. Ukiachana na Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025, timu ambazo zimefuzu Nusu Fainali mpaka sasa ni Yanga SC, Azam FC, Zimamoto na JKU.

Azam wamepata nafasi ya kucheza nusu Fainali kwa kuwacharaza KMKM bao 1-0, JKU wao waliiduwaza Singida Fountain Gate na kuwaondosha kwa ushindi wa changamoto ya mikwaju ya Penalti.

WALICHOSEMA YANGA

Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano CUP 2025
Mudathir Yahya

Mara Baada ya ushindi huo na Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025. wameweka wazi kuwa malengo yao ni kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo wa nusu fainali na kwenda kubeba ubingwa kwenye mchezo wa fainali.

Akizungumzia malengo yao mchezaji bora wa mchezo huo wa Robo Fainali, Mudathir Yahya amesema: “Ulikuwa mchezo mgumu, tunawapongeza KVZ kwa kuonyesha ushindani mzuri nami nafurahi kuisaidia Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025.

“Malengo yetu ni kushinda mchezo wa nusu fainali na fainali ili kushinda ubingwa huu, tunajua haitakuwa rahisi lakini tumejiandaa kufanya vizuri.”

Nalo benchi la ufundi la Yanga SC limeelezea furaha yake kuhusu ushindi huo, akisema kuwa Yanga SC yatinga Nusu Fainali Muungano Cup 2025 ni matokeo ya maandalizi mazuri na ushirikiano mzuri wa wachezaji na kuongeza wako tayari kwa changamoto zinazofuata katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

MAONI YA MASHABIKI WA YANGA SC

Mashabiki wa Yanga SC walijitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Gombani, wakishangilia timu yao kwa nguvu. Baada ya mchezo, mashabiki walionyesha furaha yao kwa kusherehekea ushindi huo, wakisema kuwa ni ishara ya mafanikio makubwa katika michuano ya Kombe la Muungano 2025.​

YANGA WAANZA MAANDALIZI YA NUSU FAINALI

Baada ya ushindi huo, Yanga SC hakuna kulaza damu ambapo tayari wameanza maandalizi ya mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Muungano 2025, ambapo kama makala haya yalivyoeleza wanatarajia kuvaana na Zimamoto.

Mchezo huo ni miongoni mwa michezo inayosubiriwa kwa hamu kubwa kuona nani ataibuka mbabe na kutinga Fainali, huku ikionekana ni kama kuna vita ya Tanzania Bara na Visiwani kwani kila upande umeingiza timu mbili.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.