Jonathan na MzizeJonathan na Mzize
  • Fountain Gate dakika 180 yaonja joto ya jiwe nje ndani kwa kupokea kipigo kutoka kwa Yanga 2024/25.
  • Kipa John Noble alitoa sadaka pasi yake kwa muuaji Aziz Ki akiwa nje ya 18 jambo lililota hasara kwao.
  • Clement Mzize moto wake haupimiki kwenye kucheka na nyavu akamatia usukani kwa wakali na kucheka nyavu, tuzo tatu kabatini.

Fountain Gate hawana bahati na Yanga kwenye mechi zote walizokutana uwanjani msimu wa 2024/25 kwa kuwa walipoteza pointi tatu mazima ndani ya dakika 180 za ushindani kwenye ligi.

Mzize na Tuzo
Clement Mzize kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa kafunga mabao 13 msimu wa 2024/25. Source: Yanga.

Yanga chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ni mabingwa watetezi wakiwa na pointi 70 kibindoni baada yakucheza mechi 26 ni mechi nne zimesalia kukamilisha mzunguko wa pili.

REKODI ZA YANGA MOTO

Yanga inayodhamiwa na SportPesa katika mechi 26 ushindi ni mechi 23 ikipoteza mechi mbili ilikuwa Yanga 0-1 Azam FC na Yanga 1-3 Tabora United, sare ni JKT Tanzania 0-0 Yanga. Safu ya ushambuliaji ni namba moja kwenye kutupia ikiwa na mabao 68.

Safu ya ulinzi imeokota mabao 10 ikiwa nit imu namba mbili kuruhusu mabao machache namba moja ni Simba ambayo imeruhusu jumla ya mabao 8 yote alitunguliwa kipa namba moja Moussa Camara.

Job v Singida
Dickson Job beki wa Yanga ambaye ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi 2024/25. Source: Yanga.

Fountain Gate ni timu namba moja kwa timu iliyoruhusu mabao mengi yakufungwa ambayo ni 51 baada yakucheza mechi 27 ipo nafasi ya 12 kwenye msimamo na pointi zake ni 29.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Clement Mzize ambaye huyu alifunga mabao mawili ilikuwa dakika ya 38 kwa mguu wake wa kulia akiwa ndani ya 18 hii ilitokana na makosa ya kipa John Noble kutema mpira wa faulo iliyopigwa na Aziz Ki anayevaa jezi namba 10 kwa mguu wake wa kushoto.

Mzize alipachika bao la uongozi na alifunga bao la pili dakika ya 69 akitumia pasi ya Jonathan Ikangalombo akiwa ndani ya 18 akifikisha mabao 13 ndani ya ligi, mzawa anayeongoza kwa kucheka na nyavu kwa msimu wa 2024/25.

Kiungo Aziz Ki alipachika bao moja dakika ya 43 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kipa John aliyekuwa ametoka ndani ya 18 kutoa pasi mkaa ambayo ilikutana na bao moja lilifungwa na Clatous Chama kwa pigo la faulo dakika ya 89 akitumia mguu wa kulia.

Chama v Fountain Gate
Chama Clatous, Maxi Nzengeli, Farid Mussa kwenye moja ya mchezo wa ligi 2024/25. Source: Yanga.

Chama alimtungua kipa Parapanda aliyechukua nafasi ya John na faulo hiyo ilisababishwa na Mzize ambaye aliwafunga makipa wote kwenye mchezo huo alianza kipindi cha kwanza na John kisha kipindi cha pili akamtungua Parapanda.

Alihusika kwenye mabao matatu Mzize na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Aprili 21 2025 Yanga wakikomba pointi tatu mazima.

HUYU HAPA MZIZE

Mshambuliaji namba moja kwenye utupiaji Bongo akiwa na mabao 13 baada ya mchezo huo alikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora ikiwa ni tuzo yake ya tatu msimu wa 2024/25 ndani ya ligi namba nne kwa ubora alibainisha kuwa juhudi zinawapa matokeo mazuri.

“Kwenye kila mchezo tunauchukua kwa umuhimu wake, ninamshukuru Mungu kwa kuwa tupata matokeo na ipo hivyo licha ya ushindani uliopo kikubwa ni kuona kwamba furaha inakuwepo na matokeo yanapatikana.

“Hii ni tuzo yangu ya tatu kwenye ligi ikitokana na ushirikiano ambao upo na wachezaji wenzangu, mazoezi ambayo tunafanya na kuwa tayari kwa ajili ya mchezo hivyo mashabiki wazidi kuwa nasi kwenye mechi zetu zote.”

FOUNTAIN GATE WAPOTEZA SITA MAZIMA NA TISA

Fountain Gate wamepoteza pointi sita mazima mbele ya Yanga kwa msimu wa 2024/25 wakiwa wamekwama kuambulia pointi mbele yao na safu ya ushambuliaji haijafunga mbele ya Yanga ndani ya dakika 180.

Ipo wazi kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 5-0 Fountain Gate na mchezo wa mzunguko wa pili ni Fountain Gate 0-4 Yanga wakifungwa jumla ya mabao 9.

Issa Mbuzi, Ofisa Habari wa Fountain Gate ameweka wazi kuwa mpango kazi ulikuwa kwenye kusaka ushindi lakini ulivurugika dakika ya 36 baada ya Yanga kupata bao la kuongoza dakika ya 38 kupitia kwa Mzize.

“Tulikuwa tunahitaji matokeo kwenye mchezo wetu hasa ukizingatia tulikuwa nyumbani na mianya yote tuliziba, kilichotokea ni sehemu ya mchezo. Wachezaji walijituma mwanzo mwisho hatujapata matokeo hivyo tunajipanga kwa mechi zijazo.”

KIKOSI CHA YANGA AMBACHO KILIANZA DHIDI YA FOUNTAIN

Djigui Diarra ni kipa namba moja ndani ya kikosi cha Yanga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Duke Abuya

Maxi Nzengeli, Mudathir Yahya huyu aligotea dakika ya 64 nafasi yake akachukua Jonathan Ikangalombo dakika ya 65, Prince Dube alimpisha Farid Mussa dakika ya 88, Stephane Aziz Ki alimpisha Clatous Chama dakika ya 65 na alipachika bao alipoingia na Clement Mzize alikuwa kiongozi safu ya ushambuliaji.

Share this: