Man United Vs Man CityMan United Vs Man City
n
Mpambano wa Man United Vs Man City; Source Man United

Manchester United Vs Manchester City mechi namba 196 iliyopigwa siku ya jana Jumapili imekosa mbabe mara baada ya dakika 90 za mchezo huo kumalizika bila upande wowote kuona lango la mpinzani wake huku ikishuhudiwa Alejandro Garnacho, Manuel Ugarte, na Joshua Zirkzee wakikosa nafasi za wazi kwa upande wa United, huku tishio kubwa la City likiwa kupitia straika wao Mmisri Omar Marmoush.

Suluhu hiyo kwenye Manchester Derby jana imewafanya City kukosa fursa ya kupanda hadi nafasi ya nne juu ya Chelsea kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na katika vita yao kali ya kusaka nafasi ya kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Derby hiyo isiyo na magoli, ilionyesha wazi matatizo yanayokumba timu zote mbili kwa sasa ambapo United na City zimekuwa kwenye viwango vya kawaida msimu huu na sare hii isiyo na magoli kwenye Old Trafford ilithibitisha hilo.

USHAMBULIAJI TATIZO KWA WABABE WA MANCHESTER MSIMU HUU

Searching for the opener #MUFC #ManUtd #OldTrafford #PremierLeague
Straika wa Unied, Hojlund

Timu zote mbili msimu huu zinaonekana kupitia wakati mgumu kwenye safu zao za ushambuliaji ambapo United licha ya kuwa na makali katika mashambulizi ya kushambulia kwa kasi, lakini walishindwa kuonyesha ubora mbele ya lango la City jana, kitu ambacho kilionekana pia kwa City.

Alejandro Garnacho alikosa nafasi nzuri kutoka umbali wa karibu na goli kipindi cha kwanza, wakati Manuel Ugarte alikosa nafasi muhimu kwa kupiga mpira nje kwenye kipindi cha pili. Straika wa United, Rasmus Hojlund aliondolewa uwanjani akiwa kagusa mipira 15 tu, na bila kupiga shuti lolote kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na straika, Joshua Zirkzee ambaye alikosa bao muda mfupi baada ya kuingia.

MANCHESTER CITY NAO NI MAJANGA

n
Straika wa City, Omar Marmoush

Hali ya City, kwa upande mwingine, bado inaonekana kuwa tete kwani walionekana kuwa dhaifu bila uwepo wa straika wao kiongozi, Erling Haaland. Msaidizi wake Omar Marmoush alionyesha juhudi za kawaida kipindi cha pili hususani kwa shuti la moja kwa moja kwa Andre Onana, huku Phil Foden naye akitolewa uwanjani dakika ya 56 baada ya kuwa na mchango mdogo kwa mara nyingine.

DERBY YA MWISHO BILA USHINDI KWA DE BRUYNE

Semis!
Kelvin De Bruyne; Source Manchester City

Nyota Kevin De Bruyne, ambaye alicheza derby yake ya 21 dhidi ya United katika wiki ambayo pia alitangaza kuwa ataondoka City msimu huu. Hii inamaanisha kuwa nyota huyo anaondoka bila ushindi katika derby yake ya mwisho baada ya kuwa na utawala mkubwa akiwa na City.

VIWANGO VYA WACHEZAJI KWENYE DERBY

Searching for the opener #MUFC #ManUtd #OldTrafford #PremierLeague ( )
Mchezaji bora wa mechi, Bruno Fernandes

Hivi hapa ni viwango vya mchango wa kila mchezaji kwenye mchezo wa jana, kadiri namba inavyokuwa kubwa ndivyo mchango wake ulivyokuwa mkubwa huku staa wa kimataifa wa Ureno, Bruno Fernandes akitajwa kuwa mchezaji Bora wa Mechi.

Man Utd:

Onana (6); Mazraoui (6), Maguire (5), Yoro (6); Dalot (5), Ugarte (6), Casemiro (8), Dorgu (7); Garnacho (5), Fernandes (8); Hojlund (5)

Walioingia: Lindelof (6), Zirkzee (6), Mount (6)

Man City:

Ederson (6); Nunes (6), Dias (7), Gvardiol (6), O’Reilly (6); Kovacic (5), Gundogan (5), De Bruyne (6); Foden (5), Marmoush (6), Bernardo (5)

Walioingia: Doku (5), Grealish (6), Lewis (6)

KOCHA MAN UNITED AFUNGUKA

Kocha mkuu wa Manchester United, Ruben Amorim alisema anaona maendeleo katika utendaji wa wachezaji wake lakini alikubali kuwa wanahitaji kuboresha kila eneo: “Tulikuwa karibu na kufunga goli, walikuwa na umiliki mkubwa wa mpira lakini hilo ni la kawaida. Kila mchezaji anaweza kuboresha. Sisi ni timu hatari katika mashambulizi ya kushtukiza lakini tunahitaji kuboresha eneo la mwisho kutumia fursa.

“Naelewa kuwa tukiangalia wapinzani kuna pengo kubwa lakini kama kiongozi siwezi kusema tutachukua muda mwingi, klabu kama yetu, huna muda mwingi wa kusubiri matokeo. Timu zote mbili hazipiganii ubingwa hiyo ilichangia kubadilisha mchezo. Tunahitaji kupigania mambo makubwa.

GUARDIOLA NAYE AWAKINGIA KIFUA MASTAA WAKE

n
Pep Guardiola

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, alikubali kuwa wachezaji wa City hawakuwa bora vya kutosha kugeuza nafasi walizopata lakini akakiri pointi moja waliyoipata ilikuwa ya muhimu: “Kwa kasi Garnacho, Dalot walishirikiana vizuri na kutusumbua, hivyo wana timu nzuri, lakini tumefanikiwa kuchukua pointi. Tunahitaji kuboresha ili kushinda,” amesema Guardiola.

UNAWEZA KUBASHIRI NA KUSHINDA MAMILIONI KUPITIA SPORTPESA

R
Ukurasa wa nyumbani wa SportPesa

Tembelea www.sportpesa.co.tz

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.