Man U Vs Man CityMan U Vs Man City

MOTO utawaka leo Jumapili katika dimba la Old Trafford pale wababe wa jiji moja la Manchester watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu England, mchezo unaofahamika kwa jina maarufu kama ‘Manchester Derby’.

United (A) archives
Mastaa wa City wakishangilia bao: Source Man City

Unaweza kujishindia mamilioni leo ikiwa utaweka ubashiri wako kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz

Kuelekea mchezo huu muhimu Man City wanatarajia kukosa huduma ya straika wao kiongozi, Earling Haaland ambaye alipata majeraha katika mchezo wao dhidi ya Bournemouth na kuna hofu kuwa huenda akakosa sehemu ya msimu iliyosalia. Huku United nao wakitarajiwa kumkosa nyota wao, Amad Dialo ambaye aliamua ushindi huo wa Desemba mwaka jana ambaye pia anauguza majeraha.

Ikumbukwe wababe hao wa Manchester walikutana mwezi Desemba kwenye mchezo wa ligi ambao United walifanikiwa kuibuka na ushindi, huku wachambuzi wawili maarufu, Gary Neville na Jamie Carragher wakibashiri kuwa mchezo huo una uwezekano mkubwa wa kuisha kwa matokeo ya sare.

MANCHESTER UNITED WALIPATA USHINDI WA KUSHANGAZA MWEZI DESEMBA

n
Amad Dialo: Source Man United

Manchester United ilishinda kwa mshangao ugenini kwenye Uwanja wa Etihad Stadium mwezi Disemba, na mchambuzi, Neville amevutiwa na jinsi timu hiyo ya, Ruben Amorim inavyocheza kwenye mechi kubwa msimu huu.

Mbali na ushindi huo wa derby, kwenye mechi kubwa msimu huu, Amorim aliongoza timu yake kushinda kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Arsenal kwenye Kombe la FA. United pia ilitoka sare na Arsenal kwenye ligi mwezi Machi na pia ilipata sare ya 2-2 dhidi ya vinara wa ligi Liverpool.

MASHABIKI UNITED, CITY WAUNGANA

Today is about you Today is about our city We will do you proud #MUFC #ManUtd #OldTrafford
Mashabiki wa United: Source Manchester United

Kinyume na matarajio licha ya uhasimu uliopo kati yao ndani ya Uwanja lakini kuelekea mchezo wa leo mashabiki wa Man United na Man City wameungana dhidi ya kuongezeka kwa bei za tiketi ambapo Vikundi vyao vya mashabiki ni sehemu ya kampeni ya ‘Stop Exploiting Loyalty’ ya Chama cha Wapenda Soka (FSA).

Maandalizi ya mechi ya leo kati ya United na City huko Old Trafford yameshuhudia mashabiki hao wakizigeuka klabu zao. Jioni ya Jumatano, maelfu ya mashabiki wa City waligomea dakika tisa za mwanzo za ushindi wa 2-0 dhidi ya Leicester kutokana na sera ya tiketi ya klabu.

Baada ya derbi ya leo ya 196 ya Manchester, mashabiki wa United wanapanga kushinikiza kupinga ongezeko la bei za tiketi, kumalizika kwa punguzo la asilimia 50 kwa wazee, na uamuzi wa kuhamisha mashabiki kwenye jukwaa la, Sir Bobby Charlton Stand ili kutoa nafasi kwa ujenzi wa sehemu mpya ya VIP.

Licha ya kuungana huko usitarajie hili kuashiria kumalizika kwa uhasama kati ya United na City kama ambavyo amenukuliwa msemaji wa kundi la maandamano la United, The 1958, Steve Crompton akisema: “Tunahitaji kulinda mchezo, lakini tutatunza uhasama na ushindani wetu dhidi ya wapinzani wetu.

“Singependa kitu kingine zaidi kuliko habari za kesho kuwa City imethibitishwa na hatia ya mashtaka 115 ya Premier League. Huko City, mashabiki wanapandikizwa bei. Vivyo hivyo huko Chelsea na Tottenham. Vilabu vinajaribu kuwafurusha mashabiki wa mechi za bei ya chini, na hali ya sasa kila uwanja unateseka. Utamaduni wa mashabiki utafaulu mbele ya macho yetu.

MPANGO WA MASHABIKI MANCHESTER ULIANZA NOVEMBA

FIXTURE CONFIRMATION Nottingham Forest FA Cup semi-final Sunday April - (UK) Wembley
Mashabiki wa Man City: Source Man City

“Mawasiliano ya kwanza na City yalifanyika Novemba. Mwezi uliofuata, mashabiki wa United na Liverpool walifanya maandamano ya pamoja huko Anfield. ‘Tulikuwa tumejipanga kwenye baa iliyo karibu na Anfield na Spirit of Shankly,” anasema Crompton.

Kundi la 1958 lilikusanya maelfu ya mashabiki kuandamana kabla ya mchezo wa mwezi uliopita dhidi ya Arsenal kupinga familia ya Glazers na jinsi Sir Jim Ratcliffe anavyoiendesha klabu.

“Hakuna kitu kizuri kilichotokea kutoka kwa klabu tangu Ratcliffe aingilie kati. Hakuna kitu cha kushikilia, hakuna hata dalili ya matumaini,” alisema msemaji wa The 1958. Kundi la 1894 liliongoza gomeo la City la Jumatano baada ya kutangazwa kwa mkataba ambao uliamsha hofu zaidi kuhusu ongezeko la bei za tiketi.

“Ikiwa itachukua wiki chache zaidi kufikia matokeo sahihi kwa mashabiki, hiyo ndiyo tunapaswa kufanya. Tunaondolewa. Inatengenezwa tena jamii ya mashabiki kwa gharama ya utambulisho, uaminifu na uhusiano wetu wa kizazi na klabu.

“Vilabu vinashirikiana dhidi ya mashabiki, hivyo msimu huu mashabiki wameanza kushirikiana dhidi ya vilabu. Kitu pekee kinachotutofautisha ni timu tunazozishabikia.”

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.