WAKIMATAIFA Simba katika Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika wote wakiwa kwenye hatua ya makundi 2024 wanakazi ugenini kusaka pointi tatu kwenye mechi zao ambazo zinatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa mchezo wao uliopita katika Ligi ya Mabingwa Afrika walipoteza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Yanga 0-2 Al Hilal ya Sudan.

Wakati Yanga ikipoteza, Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids ilikomba pointi tatu mazima kwenye mchezo wao dhidi ya Bravos ya Angola kwa bao la Jean Ahoua ambaye alipachika bao hilo dakika ya 27.
HUU HAPA MSAFARA WA SIMBA ALGERIA
Kikosi cha Simba kitakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu dhidi ya Constantine unatarajiwa kuchezwa Desemba 8 2024 kwa timu zote mbili kusaka pointi tatu muhimu na hiki hapa kikosi cha Simba namna hii:-
MAKIPA

Mousa Camara, Aishi Manula na Ally Salim.
MABEKI
Che Malone, Karaboue Chamou, Abdurazack Hamza, Shomari Kapombe, Valentino Nouma, Kelvin Kijili. Zimbwe Jr.
VIUNGO
Mzamiru Yassin, Deborah Mavambo, Fabrice Ngoma, Ladack Chasambi, Augustin Okejapha, Omary Omary, Edwin Balua, Jean Ahoua na Awesu Awesu.
WASHAMBULIAJI
Leonel Ateba, Steven Mukwala.
WATAKOSEKANA
David Kameta yeye ni beki jina lake halipo kwenye orodha ya wachezaji waliokwea pipa kueleka Algeria kuikabili Constantine.
Jina lingine ambalo halipo ni Yusuph Kagoma, Joshua Mutale hawa hawapo fiti kama ilivyo kwa Hussen Abel na Ayoub Lakred ambao haw ani makipa.
SEMAJI HILI HAPA
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na mpango mkubwa ni kupata matokeo chanya dhidi ya Constantine kwenye mchezo wao wa kimataifa.
Simba Desemba 8 inatarajiwa kutupa kete ya pili kimataifa kwenye Kombe la Shirisho Afrika ikiwa ugenini na mchezo wa kwanza hatua ya makundi ni bao 1-0 walishinda dhidi ya Bravos uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Ikumbukwe kwamba kwa sasa ili kutinga hatua ya robo fainali ni muhimu kuvuna pointi tatu ndani ya uwanja kwenye dakika 90 za kazi mwanzo mwisho.
Ally amesema; “Ni mechi muhimu kwetu na ambacho tunahitaji ni kupata pointi ili kufikia malengo yetu ambayo ni kuvuka kwenye hii hatua ya makundi.
“Ushindi mchezo wa kwanza dhidi ya Bravos umetupa nguvu kuelekea mechi zijazo na hakuna timu nyepesi hapa kutokana na kila timu kuwa imara kwenye kutafuta matokeo.”
YANGA HAWA HAPA

Kikosi cha Yanga kipo katika maandalizi ya mwisho kuwakabili MC Alger mchezo unatarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024 ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
HIKI HAPA KIKOSI CHA YANGA
MAKIPA
Djigui Diarra, Khomein Aboubhakar, Aboutwalib Mshery.
MABEKI
Bakari Nondo, Job, Bacca, Yao, Kibabage, Kibwana Shomari, Ladack Boka.
VIUNGO
Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Jonas Mkude, Duke Abuya, Maxi Nzengeli, Dennis Nkane, Farid Mussa, Shekhan, Pacome, Clatous Chama, Aziz Ki.
WASHAMBULIAJI

Jean Baleke, Musonda, Clement Mzize, Prince Dube.
HUYU HAPA ALI KAMWE
Uongozi wa Yanga umebainisha kwamba mchezo wao wa kimataifa dhidi ya MC Alger ya Algeria unaotarajiwa kuchezwa Desemba 7 2024 utakuwa mgumu na wanakwenda kwa tahadhari zote kupata matokeo mazuri.
Ikumbukwe kwamba huo utakuwa ni mchezo wa pili kwa Yanga baada ya mchezo wa kwanza katika hatua ya makundi kupoteza mbele ya Al Hilal mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ukasoma Yanga 0-2 Al Hilal.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kupeperusha bendera ya Tanzania kimataifa na watakwenda kwa tahadhari zote kutafuta matokeo mazuri.
“Tumetazama mchezo wao uliopita na tumeona namna ambavyo walifanya, sisi tuna tahadhari zote wao ni wakubwa na wanacheza nyumbani kwao hilo tunalitambua.
“Mchezo wetu utakuwa ni mgumu hasa ukizingatia kwamba kwenye hatua za makundi na Ligi ya Mabingwa Afrika huku zinacheza timu kubwa na tunakwenda kupambana na wakubwa.
“Kwa wachezaji wanatambua ushindani uliopo na taarifa ambayo imetolewa ni kwamba mechi hii haitakuwa na mashabiki kwa sababu ya adhabu ambayo wanaitumikia, sijui walikosea wapi na walifanya nini sisi tunachotambua kwamba hawatakuwa na mashabiki.”

