SportPesa Shabiki CupSportPesa Shabiki Cup

SPORTPESA
Mashabiki timu zinazodhaminiwa na SportPesa

Mara baada ya kuwepo matamanio ya muda mrefu ya mashabiki mbalimbali na wadau wengine wa michezo hatimaye Kampuni bora ya ubashiri ya SportPesa imezindua mashindano maalum yaliyopewa jina la ‘SportPesa Shabiki Cup’.

SportPesa Shabiki Cup ni mashindano ya soka yatakayoendeshwa na jamii ambayo yameandaliwa na SportPesa, yakiwa na lengo la kuwakutanisha wapenda soka kutoka mikoa mbalimbali kushirikiana na vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa.

Mashindano haya yanalenga kuimarisha uhusiano kati ya jamii na mashabiki wa soka wa maeneo ya karibu kwa kutoa fursa ya kushiriki, kushindana, na kushirikiana.

MUUNDO WA MASHINDANO UTAKUWAJE?

Mashindano yatafanyika katika mikoa mbalimbali nchini. ambapo kila eneo, timu mbili zitashindana:

  • Timu 1: Timu iliyoundwa na wachezaji kutoka vilabu vinavyodhaminiwa na SportPesa.
  • Timu 2: Timu iliyochaguliwa kutoka kwa jamii ya eneo husika.

Washindi wa kila eneo watapokea tuzo zao kama ilivyoelezwa kwenye sehemu ya zawadi.

MBEYA KINAWAKA MAPEMA SANA

SPORTPESA
Ali Kamwe na Mashabiki wa Yanga

Mashindano haya yanatarajiwa kuanza kutimua rasmi jijini Mbeya ambapo kwa wewe shabiki wa soka nchini, timu yako ya ushindi SportPesa itakuletea zawadi kibao.

VIGEZO VYA USHIRIKI NI VIPI?

  • Wachezaji lazima wawe na umri wa miaka 18 na kuendelea.
  • Washiriki lazima wawe raia, au wakazi wa kudumu wa Tanzania.
  • Kwa Timu 1, wachezaji wote lazima wawe wanachama hai wa tawi linalotambulika.
  • Kwa Timu 2 (Timu ya Jamii ya Wenyeji), wachezaji wote lazima watoke katika jamii ya eneo linaloandaa tukio.

Usajili

Fomu za usajili zitapatikana kwenye vibanda maalum vya SportPesa katika kila  eneo pamoja na ofisi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa. Wachezaji lazima wajisajili mmoja mmoja, wakitoa uthibitisho wa makazi katika  jamii husika.

Mchakato wa Uteuzi

Kamati ya uteuzi, ikijumuisha makocha wa soka wa eneo, wawakilishi wa matawi, na maafisa wa SportPesa, watapitia wachezaji wote waliosajiliwa.

Maonyesho ya vipaji yatafanyika kwa siku mbili katika kila eneo, ambapo wachezaji waliosajiliwa wataonyesha ujuzi wao mbele ya kamati ya uteuzi. Kamati ya uteuzi itawapima wachezaji kwa kuzingatia ujuzi wa soka, ushirikiano wa timu, na nidhamu ya michezo.

Kamati itachagua wachezaji 14 (11 wa kuanza na 3 wa akiba) kuunda Timu ya Jamii ya Wenyeji. Uteuzi utatangazwa mwishoni mwa majaribio.

Sheria za mashindano;

  • Muda wa Mchezo: Kila mchezo utakuwa na vipindi viwili vya dakika 30, na mapumziko ya dakika 10 katikati.
  • Kuamua Mshindi: Iwapo mchezo utamalizika kwa sare ya 0-0 katika dakika ya 70, mshindi ataamuliwa kwa kupiga mikwaju ya penalti.
  • Badiliko la Wachezaji: Kila timu itaruhusiwa kufanya mabadiliko matatu kwa kila mechi.
  • Madhibiti: Mechi zote zitaendeshwa na waamuzi waliothibitishwa na shirika husika.
  • Hatua za Nidhamu: Sheria za kadi ya njano na nyekundu zitatumika kulingana na kanuni za kawaida za soka. Wachezaji watakaopokea kadi nyekundu watafungiwa kushiriki.

Zawadi

Timu Inayoshinda: Timu itakayoshinda mechi ya mwisho ya mashindano itazawadiwa Kikombe cha SportPesa Shabiki Cup na zawadi ya Fedha kiasi cha TZS 500,000.

Jezi za Timu: Seti kamili ya jezi za mpira kwa wachezaji wote na benchi la ufundi.

Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.

Timu ya Pili

Zawadi ya Fedha: TZS 250,000, Medali: Medali kwa kila mshiriki wa timu.

Zawadi za Wachezaji Binafsi

Mfungaji Bora: TZS 100,000.

Kipa Bora: TZS 100,000.

Mchezaji Bora (MVP): TZS 100,000.

Sheria za Jumla

SPORTPESA
Shabiki Cup
  • Uamuzi wa waamuzi na kamati ya waandaaji ni wa mwisho na lazima uheshimiwe.
  • Timu lazima zifuate ratiba ya mashindano. Kushindwa kufika kwa wakati wa mchezo kutasababisha kupoteza.
  • SportPesa inahaki ya kuwaondoa timu au mchezaji yeyote atakayekiuka sheria za mashindano au kuonyesha tabia isiyo ya kimichezo.

Udhamini na Uwekaji Nembo

  • SportPesa inahifadhi haki zote za kipekee kwa matangazo na shughuli za utangazaji zinazohusiana na mashindano.
  • Timu zote zinahitajika kuvaa jezi zenye nembo za SportPesa wakati wa mechi.

Vyombo vya Habari na Matangazo

Kwa kushiriki kwenye mashindano, wachezaji na timu wanakubali kuruhusu SportPesa kutumia picha zao, majina, na sura kwa ajili ya matangazo na uendelezaji kwenye majukwaa mbalimbali ya vyombo vya habari.

Mabadiliko

SportPesa inahifadhi haki ya kubadili Masharti na Vigezo hivi wakati wowote washiriki watajulishwa mapema kuhusu mabadiliko yoyote.

Dhima

SportPesa haitahusika kwa majeraha, ajali, au uharibifu wowote utakaotokea wakati wa mashindano na washiriki wanahimizwa kuchukua tahadhari zinazofaa.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.