Everton FCEverton FC

HAKUNA kupumzika wikiendi kikitoka kitu kinaingia kitu kutokana na ratiba kuwa yamoto viwanjani kwa mechi kali kuchezwa ambapo kuna dakika 90 za kuvuja jasho kwa wachezaji kusaka ushindi uwanjani.

Imekuwa hivyo wale wazee wamikeka kwao ni kicheko na muda huu una nafasi ya kuandaa mkeka wako kupitia SportPesa kisha dakika 90 zikigota mwisho unakunja kikilicho chako mapema bila mashaka.

AZAM FC
MASTAA wa Azam FC wakishangalia moja ya bao kwenye mchezo wa ushindani. Source: Azam FC.

Ligi zinaendelea na mechi kali zinachezwa hilo lipo wazi kwani sio Bongo pekee hata Ulaya nako Ligi Kuu England moja ya ligi maarufu duniani wakali wa kazi nao wapo uwanjani kwa mara nyingine ikiwa ni wiki ya tano sasa.

Kuna waliokunja mkwanja wao mapema Septemba 19 kupitia SportPesa baada ya matajiri wa Dar Azam FC kupata ushindi wa kwanza kwa kushuhudia ubao wa Uwanja wa KMC Mwenge ukisoma KMC 0-4 Azam FC.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo huo mabao ya Azam FC yalifungwa na Idd Suleiman dakika ya 19, Lusajo Mwaikenda dakika ya 55, Saadun dakika ya 60 na Freddy Tangalo alijifunga dakika ya 76 alipokuwa kwenye harakati za kuokoa hatari kutoka kwa Nathaniel Chilambo.

Sahau kuhusu matajiri wa Dar Azam FC ambao mchezo wao ujao unatarajiwa kuchezwa Septemba 26 2024 Uwanja wa Mkapa dhidi ya Simba itakuwa Mzizima Dabi kuna kazi zinaendelea leo kwenye mechi za ligi na Jumamosi kutakuwa na mechi ngoma ni mpaka Jumapili.

HAPA TUNAKULETEA RATIBA WIKIENDI NAMNA HII

Fountain Gate
NYOTA wa Fountain Gate akiwa kwenye maandalizi ya mechi za ushindani wikiendi. Source: Fountain Gate.

Tabora United v Fountain Gate saa 10:00 jioni. Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

Kagera Sugar v Ken Gold FC, saa 1:00 usiku. Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

SEPTEMBA 21
Tanzania Prisons v Dodoma Jiji, saa 8:00 mchana. Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Pamba Jiji v Mashujaa saa 10:15 jioni. Mchezo huu utachezwa uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

SEPTEMBA 22

JKT Tanzania v KMC saa 8:00 mchana. Mchezo huu utachezwa Uwanja wa Mej.Jen. Isamuhyo.

Azam FC v Coastal Union, Uwanja wa Azam Complex, saa 1:00 usiku, Dar.

KATIKA ANGA LA KIMATAIFA WIKIENDI

 

NYOTA WA YANGA
NYOTA wa Yanga ikiwa ni Aziz Ki, Mzize, Musonda wakishangilia bao kwenye moja ya mchezo wa ushindani.Source: Yanga.

Yanga v CBE SA ya Ethiopia saa 2:30 usiku itakuwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Ikumbukwe kwamba Yanga inayodhaminiwa na SportPesa mchezo wake uliopita ugenini ilipata ushindi wa bao 1-0.

Bao la ushindi la Yanga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika lilipachikwa kimiani na Prince Dube dakika ya 45 akitumia pasi ya Aziz Ki na wote wapo fiti kuelekea mchezo utakaoamua nani atatinga hatua ya makundi.

SEPTEMBA 22

 

YUSUPH Kagoma
Kiungo wa Simba Yusuph Kagoma anatarajiwa kuwa kwenye kazi wikiendi dhidi ya Al Ahli Tripoli. Source: Simba.

Simba v Al Ahli Tripoli saa 10:00 jioni. Huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mshindi kwenye mchezo huu atatinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.

Katika mchezo uliopita ugenini baada ya dakika 90 ubao ulisoma Al Ahli Tripoli 0-0 Simba hivyo kazi kubwa kuelekea kwenye mchezo huo kusaka mshindi kwenye mchezo huo wa dakika 90 ambao utakuwa na ushindani mkubwa.

PREMIER LEAGUE KAZI INAWAKA, (EPL)

 

WESTHAM
Westham mastaa wakishangilia moja ya bao. Source: WestHam.

West ham maarufu kama wagonga nyundo watakuwa kazini kumenyana na  Chelsea hawa maarufu kwa jina la watoto wa darajani.

Aston Villa v Wolverhampton kwenye msako pointi tatu muhimu uwanjani. Aston Villa ipo nafasi ya tano kwenye msimamo na pointi 9 inawakaribisha wapinzani wake ambao wapo nafasi ya  18 ni pointi moja imekusanya.

Liverpool v Bournemouth. Majogoo watakuwa Uwanja wa nyumbani Anfield, nafasi ya nne na pointi tisa inakutana na wapinzani wao ambao wapo nafasi ya 11 na pointi 5.

Tottenham v Brentford. Ni nafasi ya 13 na pointi zao kibindoni ni 4 kibindoni huku Brentford wakiwa nafasi ya 9 pointi zao kibindoni ni 6.

Leicester v Everton. Wakali hawa watakuwa kwenye msako wa pointi tatu huku wenyeji Leicester wakiwa na pointi mbili nafasi ya 15 inakutana na Everton iliyo nafasi ya 20 haijakusanya pointi.

Southampton v Ipswich. Katika mchezo huu Southampton ihaina bahati baada ya kucheza mechi nne haijakusanya pointi nafasi ya 19 na wapinzani wao wapo nafasi ya  17 pointi mbili timu zote zimecheza mechi nne.

 

Share this: