
UBAYA ubwela wanasema hivyo kwa sasa Wanasimba kutokana na kazi kubwa wanayofanya kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuanza Agosti. Kwenye maboresho katika dirisha kubwa la usajili kuna wachezaji wapya zaidi ya 10 ambao tayari wameshatambulishwa kuwa ndani ya kikosi hicho.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 Simba ilishuhudia taji la ligi likiwa mikononi mwa watani zao wa jadi Yanga waliokamilisha msimu wakiwa nafasi ya kwanza na pointi 80 baada ya kucheza mechi 30 hivyo Simba inapambana kujinasua kutoka nafasi ya tatu ilipogotea msimu wa 2023/24 ikiwa na pointi 69.
Miongoni mwa wachezaji ambao wametambulishwa Simba ni pamoja na Augustine Okejapha huyu ni raia wa Nigeria alitambulishwa Julai 6 2024. Kwa msimu wa 2023/24 kwenye mechi za mwisho Simba ilikamilisha msimu ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda na msaidizi wake Seleman Matola wote hawa ni wazawa.
UBAYA UBWELA BENCHI LA UFUNDI
Ubaya ubwela umetambulishwa pia kwenye benchi la ufundi ambapo Simba ilimtambulisha kocha mpya ambaye ni Fadlu Davids ilikuwa ni Julai 5 2024 kocha huyo alitambulishwa kuwa mali ya Simba.
MASHAKA
Kutoka ndani ya kikosi cha dhahabu ni Valentino Mashaka yeye ni kiungo mshambuliaji alikuwa akitimiza majukumu ndani ya Geita Gold ambayo msimu wa 2024/25 itashiriki Championship baada ya kushuka daraja. Mchezo wa mwisho mzunguko wa pili ikiwa Uwanja wa Nyakumbu, ubao ulisoma Geita Gold 0-2 Azam FC..
Ilikuwa ni Julai 5 2024 Valentino alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba. Huyu ni kiungo mshambuliaji ambapo alipokuwa ndani ya Geita Gold alikuwa ni chaguo la kwanza. Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 24 za ushindani ndani ya ligi na alifunga mabao sita akitoa pasi moja ya bao. Ikumbukwe kwamba Geita Gold itashiriki Championship msimu wa 2024/25 baada ya kushuka daraja.
Mashine ya ubaya ubwela iliyotambulishwa ndani ya Simba imeingia kwenye sekeseke kutokana na mabosi wa timu aliyokuwa akicheza kueleza kuwa bado ni mali yao. Nyota wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba anaitwa Lameck Lawi ambaye ni beki aliyeibuka ndani ya kikosi cha Simba kutoka Coastal Union. Lawi alitambulishwa Juni 20 2024.
MUTALE
Joshua Mutale alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba Julai Mosi 2024 ikiwa ni siku ambayo Clatous Chama alitambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya mkataba wake wa kuitumikia Simba kugota mwisho.
MUKWALA
Steven Mukwala ni nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba alitambulishwa Julai 2 2024 kuwa ndani ya kikosi hicho ambacho kitashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
UBAYA UBWELA KWA JEAN
Ingizo jingine jipya jingine ndani ya Simba ni Ahoua Jean Charles ambaye alitambulishwa Julai 3 2024 kuwa kwenye changamoto mpya kwenye kikosi hicho.
HAMZA
Nyota mwingine mpya ndani ya kikosi cha Simba ni Abdulrazack Mohamed Hamza alitambulishwa rasmi Julai 4 2024 kuwa ni nyekundu na nyeupe. Nyota huyo anaingia kwene orodha ya wapya kwenye kikosi cha Simba.
KAGOMA
Yusuph Kagoma kiungo aliyekuwa ndani ya Singida Fountain Gate alitambulishwa ndani ya Simba kuwa ingizo jipya ilikuwa ni Julai 8 2024. Kiungo huyu alikuwa anatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga kabla ya kusaini dili lake ndani ya kikosi cha Simba.
CHAMOU

Raia huyu wa Ivory Coast yeye ni beki anaitwa Karaboue Chamou alitambulishwa ndani ya kikosi Julai 7 2024. Wanamuita mashine ya zege kutokana na uimara wake kwenye eneo hilo la ulinzi mkataba wa miaka miwili.
NOUMA
Beki mwingine ni raia wa Burkina Faso anaitwa Valentin Nouma alitambulishwa ndani ya Simba Julai 7 2024 kwa ajili ya changamoto mpya kwenye kikosi hicho
FERNANDES
Kiungo Debora Fernandes Mavambo mwenye uwezo wa kuchezesha timu akiwa na mpira ni ingizo jipya ndani ya Simba kuelekea msimu mpya wa 2024/25. Ni Julai 6 2024 alitambulishwa kuwa ndani ya Simba kwa kandarasi ya miaka miwili.
OMARY
Omary Abdalha huyu ni kiraka alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba rasmi Julai 6 akitokea Mashujaa FC. Nyota huyo mwenye miaka 19 ana uwezo wa kucheza namba 10, 8, 9, 6 kwa umakini na ana sifa ya kuwa na spidi uwanjani.
KIJILI

Kelvin Kijili alitambulishwa rasmi ndani ya Simba Julai 12 2024 yeye ni beki. Tayari yupo kambini nchini Misri kwa maandalizi ya msimu ujao.
UBAYA UBWELA NI KWA MKAPA
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kuwa Ubaya Ubwela ni slogan yao kwa msimu wa 2024/25 kuelekea kwenye Simba Day, Agosti 3 2024 inayotarajiwa kufanyika Uwanja wa Mkapa.
“Ubaya ubwela itakuwa hiyo ni slogan yetu, kuna mashine za ubaya ubwela zenye ambazo zipo na zitafanya kazi kwelikweli.”.
Kwa mujibu wa mchambuzi wa michezo Mohamed Mohamed amesema kuwa Ubaya Ubwela ni neno ambalo linamaanisha kuwa ubaya Ubaya.

