PA OMAR JOBE (-)PA OMAR JOBE (-)
JOBE
Pa Omar Jobe

Hatimaye Uongozi wa Simba umethibitisha kuwa umefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na mshambuliaji raia wa Gambia, Pa Omar Jobe baada ya kipindi kifupi cha miezi sita.

Jobe mwenye umri wa miaka 25 ni raia wa Gambia ambayeb alijiunga na Simba katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Zhenis inayoshiriki Ligi Kuu nchini Kazakhstan.

Katika taarifa yao Simba ambao wamewahi kula shavu la udhamini wa Kampuni bora ya kubashiri ya SportPesa wamemuelezea, Jobe kuwa ni mmoja ya washambuliaji bora na mwenye uwezo mkubwa, lakini ameshindwa kuendana na kasi ya timu yao na malengo ya klabu.

Taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa katika kipindi chote alichokuwa na Simba, Jobe alikuwa mchezaji msikivu mwenye nidhamu ya hali ya juu na alikuwa anajituma mazoezini na uwanjani.

Baada ya kuachana na Jobe, Simba wamesema kuelekea msimu mpya wa mashindano 2024/25 wamefanya marekebisho makubwa ya kikosi na malengo yao ni kurejesha makali waliyokuwa nayo miaka minne iliyopita.

Simba wamemtakia kila la kheri Jobe katika maisha mapya ya soka nje ya Simba na kusema siku zote wataendelea kuthamini mchango wake ndani ya kikosi chao.

CHASAMBI AAHIDI MAKUBWA SIMBA

Katika hatua nyingine kiungo mshambuliaji wa Simba, Ladaki Chasambi amesema ana matumaini msimu ujao watafanya vizuri kutokana na maandalizi na kikosi tulichonacho.

Chasambi amesema kikosi chao kimeundwa na wachezaji wengi vijana na wapo tayari kuipambania timu kuhakikisha wanafanya vizuri.

Chasambi ameongeza kuwa maandalizi wanayofanya kupitia benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha, Fadlu Davids ni mazuri na hayo yanampa matumaini kuwa msimu ujao watakuwa bora zaidi.

“Kambi yetu ni nzuri hapa Misri, tunafanya mazoezi chini ya Kocha Fadlu na wasaidizi wake na kila kitu kinaenda sawa na tunaamini tutakuwa bora zaidi msimu ujao.”

“Timu yetu inaundwa na wachezaji vijana na tuna ari ya kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuirejesha Simba katika nafasi yake iliyokuwepo,” amesema Chasambi.

MO DEWJI KWENYE MKAKATI MZITO

JOBE
Mohammed Dewji

Rais wa heshima wa Simba ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohammed Dewji ‘Mo’ amekutana na kufanya mazungumzo na mtandao wa Simba Executive Network (SEN), lengo likiwa kujadiliana mambo mbalimbali ya maendeleo.

SEN ni mtandao wa mashabiki wa Simba ambao huchangia ada ya 1,500,000 kwa mwaka kwa ajili ya miradi maalumu ya miundombinu ya klabu.

Wanachama wa SEN hupata faida nyingi kama bima za maisha, tiketi za mechi na faida nyingine nyingi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa SEN akiwapo Mwenyekiti Abdulrazak Badru, Makamu wake Farouk Baghoza, Katibu Dkt. George Ruhago, Katibu Msaidizi Richard Mwalibwa na wanachama wa SEN.

Menejimenti ya Simba iliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula

KAPOMBE ATOA TAMKO

Nayue mlinzi wa kulia, Shomari Kapombe amesema wanaendelea vizuri na kambi ya maandalizi ya msimu katika mji wa Ismailia nchini Misri.

Kapombe amesema Kocha wao Mkuu, Fadlu Davids amekuwa akiwafundisha vitu vipya huku akisisitiza katika mazoezi ya stamina ili wawe imara.

Kapombe ameongeza kuwa tangu waanze kambi ya maandalizi nchini Misri, wachezaji wamekuwa wanajitahidi kufuatia maelekezo wanayopewa.

“Kambi inaendelea vizuri hapa Misri, tunazidi kupokea mafunzo kutoka kwa walimu wetu. Kocha anasisitiza tuwe haraka sana tunaposhambulia na kutumia kwa ufasaha nafasi.”

“Tangu tuanze kambi ya maandalizi naamini hadi tukimaliza tutakuwa imara na tayari kwa mashindano,” amesema Kapombe.

KIJIRI “NILIKUWA NA NDOTO YA KUCHEZA SIMBA”

JOBE
Kelvin Kijiri

Mlinzi mpya wa Simba, Kelvin Kijili amesema ndoto yake ilikuwa kucheza kwenye kikosi hiko tangu akiwa mtoto na anafurahi kuwa imetimia rasmi.

Kijili ameyasema hayo muda mfupi baada ya kujiunga kambini na wenzake nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

Kijili amesema alikuwa ana ndoto za kucheza Simba na na atahakikisha anajitoa kwa kila kitu ili kuwafurahisha mashabiki.

Kijili amewaahidi mashabiki atapambana muda wote kwa ajili ya kuwafurahisha pamoja na kuisaidia timu hiyo kupata matokeo chanya akisaidiana na wachezaji wenzake.

“Nimefurahi kuwa hapa, hii ni ndoto yangu ambayo nilikuwa nao tangu nikiwa mtoto na leo imetimia. Simba ni Klabu ya ndoto yangu na nitahakikisha naisadia kufanya vizuri.”

 

“Mashabiki wetu naomba mnipe ushirikiano mkubwa nami nitahakikisha nawalipa furaha uwanjani,” amesema Kijili.

 

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.