Prince DubePrince Dube
Ali Kamwe
HAWANA dogo Yanga kuelekea 2024/25, Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe ni kicheko. Source: Yanga.

HAWANA jambo dogo Yanga mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 wakikomba jumla ya pointi 80 baada ya kucheza mechi 30 chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi ambaye bado yupo.

Gamondi na balaa lake la kutembeza kipigo cha mabao 5-0 kwa wapinzani wao ikiwa ni pamoja na Simba kwenye mzunguko wa kwanza ubao uliposoma Simba 1-5 Yanga ameongeza mkataba wa mwaka mmoja kusalia ndani ya kikosi hicho.

Ikumbukwe  kwamba ni Yanga  walitwaa ubingwa wa ligi. Wapo waliokuwa wakichana mikeka na wapo ambao walikula kirahisi hata wewe unaweza jisajili ukawa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz 

Licha ya kuwa na mwendo mzuri hawajakubali yote yaliyotokea wameamua kuongeza wachezaji wengine wa kazi kuelekea msimu mpya wa 2024/25. Ipo wazi kuwa Yanga inadhaminiwa na SportPesa kampuni ambayo imekuwa ikitoa mkwanja mrefu kwa wanaocheza michezo mbalimbali ya kubashiri kwa muda na kwa uhakika.

Katika dirisha kubwa la usajili Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga aliweka wazi kuwa watafanya maboresho makubwa kwa kuwatambulisha wachezaji wenye majina makubwa na uwezo ili kuleta ushindani ndani ya uwanja.

“Tutafanya usajili mkubwa kwa wachezaji wenye uwezo wa kuwa kikosi cha kwanza. Hatuna mashaka ukitazama kikosi kilichokuwa msimu uliopita kilikuwa ni bora na msimu ujao pia tunahitaji kuwa na kikosi bora zaidi.

KAZI IMEANZA

Tayari Yanga imeanza kutambulisha wachezaji wapya ambapo Julai Mosi 2024 walibadilisha upepo kwenye anga la mpira.Yanga waliinasa saini ya Clatous Chama kiungo mshambuliaji aliyekuwa anacheza Simba.

Ikumbukwe kwamba mabosi wa Simba walikuwa kwenye majadiliano na Chama kuhusu kuongeza mkataba mpya. Kabla hawajafikia muafaka tayari mwamba alisaini Yanga na kutambulishwa.

FARID MUSSA

Baada ya kumtambulisha mwamba wa Lusaka Chama Julai Mosi hawakupoa walimuongezea mkataba Farid Mussa. Kiungo huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada ya timu mbalimbali, mabosi wakamfungia kazi.

Julai Mosi alitambulishwa kuongeza kandarasi mpya kutoka 2024 mpaka 2026 hivyo ni uhakika atakuwa miongoni wa nyota wa kikosi cha Yanga msimu wa 2024/25.

DJIGUI DIARRA

Diarra
UHAKIKA kuwa ndani ya Yanga 2024/25 kipa Diarra. Source: Yanga.

Mwamba Diara wanamuita mdaka mishale yeye pia Julai 5 mkataba wake uliongezwa. Ni kutoka 2024 mpaka 2027 kipa huyo atakuwa akitimiza majukumu yake Yanga. Ipo wazi kwamba ni chaguo la kwanza la Gamondi.

MWAMNYETO

Nahodha Bakari Mwamnyeto alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada ya timu mbalimbali Bongo ikiwa ni pamoja na Simba. Julai 3 alitangazwa kuongeza mkataba mwingine utakaomfaya awepo hapo mpaka 2026.

KIBABAGE

Julai 4 ilikuwa ni kwa Nickson Kibabage ambaye aliongezewa kandarasi nyingine.Kutoka 2024 yupo mpaka 2027 ndani ya kikosi hicho. Yeye ni mbavu ya kushoto.

MSHERY

Kipa Aboutwalib Mshery ambaye aliibuka hapo akitokea Mtibwa Sugar Julai 4 ilitangazwa kuwa bado ni njano na kijani. Kipa huyo ni mpaka 2027.

MWANA WA MFALME

Dube Prince
ATAKUWA ndani ya Yanga 2024/25 baada ya kutambulishwa na mabingwa wa ligi msimu wa 2023/24. Source: Yanga.

Hawakuishia kwenye utambulisho wa wachezaji waliongeza mikataba tu bali walitambulisha nyota mpya usiku wa kuamkia Julai 7 2024 ikiwa ni zawadi ya 7/7 kwa mashabiki.

Ni Prince Dube alitambulishwa ambapo alikuwa akicheza ndani ya Azam FC alipovunja mkataba wake kwa makubaliano ya pande zote.

Dube alivunja mkataba na Azam FC kwa kufuata masharti yaliyokuwa kwenye mkataba wake hivyo alikuwa huru kujiunga na mabingwa wa msimu wa 2023/24 Yanga.

Raia huyo wa Zimbabwe amesaini dili la miaka miwili kuitumikia timu ya Yanga atakutana na Simba ndani ya ligi kwenye Kariakoo Dabi akiwa na uzi wa Yanga.

Msimu wa 2023/24 walipokutana na Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana bao 1-1 na bao la Simba lilifungwa na Clatous Chama ambaye kwa sasa yupo ndani ya Yanga.

JEMBE AMCHAMBUA DUBE

Legend Saleh Jembe ambaye ni mwandishi mkongwe aliyefanya mahojiano na wachezaji, makocha wenye mafanikio makubwa amebainisha kuwa Dube ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa.

“Dube ni mshambuliaji mzuri ambaye anaonesha uimara wake akiwa ndani ya uwanja. Sio wa kumbeza kwa namna yoyote kwa kuwa kazi yake inaonekana kwa vitendo.”

BOKA

Boka
Boka ni ingizo jipya ndani ya Yanga 2024/25 yeye ni beki wa kupanda na kushuka. Source: Yanga.

Beki wa kushoto kutoka FC Lupopo wakuitwa Boka Chadrak alitambulishwa usiku wa kuamkia Julai 8. Anakuja kuwa mbadala wa Joyce Lomalisa ambaye hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2024/25 baada ya mkataba wake kugota mwisho.

KHOMEINY

Mchana wa Julai 8 2024 Yanga hawajapoa wamemtambulisha kipa Aboubhakar Khomeiny ambaye msimu wa 2023/24 alikuwa ndani ya Ihefu.

Share this: