Fei TotoFei Toto
FEISAL Salum
KIUNGO wa Azam FC, Feisal Salum mwenye mabao 19 msimu wa 2023/24. Source:Azam FC.

MTAMBO wa mabao ndani ya Azam FC ishu yake ni nzito kusepa hapo huku mabosi wa timu hiyo wakiuliza kimtindo kama kuna shido kwa nyota huyo kuwa katika mazoezi. Ilikuwa inatajwa kwamba huenda Feisal Salum angesepa ndani ya Azam FC na timu iliyokuwa inatajwa kuwania saini yake ilikuwa ni Simba.

Mwamba huyo ambaye ni ingizo jipya ndani ya Azam FC akitokea Yanga ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Yusuph Dabo kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi msimu wa 2023/24.  Ipo wazi kwamba ni Yanga  walitwaa ubingwa wa ligi. Wapo waliokuwa wakichana mikeka na wapo ambao walikula kirahisi hata wewe unaweza jisajili ukawa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz 

Ni namba moja kwenye kucheka na nyavu akifunga jumla ya mabao 19 huku kinara akiwa ni Aziz Ki wa Yanga aliyefunga jumla ya mabao 21.

Julai 5 2024 kiungo huyo alikuwa kwenye orodha ya wachezaji Azam FC waliopo kwenye kambi ya Azam Complex kwa ajili ya mazoezi maalumu kuelekea msimu mpya unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Picha za mazoezi hizo zilisindikizwa na ujumbe kutoka kwa Admin wa Azam FC ikiwa ni kama dongo kimtindo kwa wale waliokuwa wanatajwa kuwania saini yake miongoni mwa timu zilizokuwa zikitajwa ilikuwa ni Simba.

Fei Salum
Fei Salum akitabasamu katika maandalizi ya msimu wa 2024/25 ndani ya Azam FC. Source: Azam.

“Kwani kuna shido!? (Kiswahili sanifu ikiwa ni kwamba kuna shida)
Mfungaji wetu bora msimu uliopita Feisal Salum, aliporejea na tabasamu kwenye mazoezi ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.”

Kwa upande wa kocha Dabo amebainisha kuwa mipango inakwenda sawa kuelekea msimu mpya ambapo maandalizi yanaendelea kukiwa na mpango kazi maalumu kufuatana na program ambazo zipo.

“Tunaendelea na maandalizi kuelekea msimu mpya na tupo na mpango kazi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya, tulianza na program ya GYM na nyingine zinafuata ili kuwa imara na wachezaji wanazidi kuwa imara.”

Kambi ya Azam FC inatarajiwa kuwa sehemu tatu tofauti, Tanzania Bara na Visiwani na nje ya nchi pia wana mpango wa kuweka kambi huko.

Fei Toto anaingia kwenye orodha ya mastaa ambao walifunga hat trick mapema zaidi kwa msimu wa 2023/24 ikiwa ni moja kati ya rekodi aliyoandika katika mchezo wake wa kwanza akiwa na uzi wa Azam FC.

Amekuwa akihusishwa kujiunga na Simba pamoja na timu nyingine huku mabosi wa Azam FC wao wakiweka wazi kuwa ikiwa atahitajika kwa timu yoyote ile basi utaratibu ufuatwe kwani hawana nia ya kumzuia mchezaji kuwa kwenye timu mpya.

Ni uwezo wa kutumia mguu wa kushoto kwenye kufunga pamoja na kulia ni jadi yake na mchezo wake wa mwisho alifunga bao moja mbele ya Geita Gold, msimu wa 2023/24.

MABAO YA FEI KWA KUSHOTO

Nyota Fei Toto alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 4 akitumia mguu wa kushoto. Hivyo ana uwezo wa kutumia miguu yote miwili kwenye suala la kufunga jambo ambalo linaongeza thamani yake sokoni.

MABAO YA KULIA

Hapa ndipo ujanja wake ulipo kutokana na mabao yake mengi kufunga akitumia mguu huo kwenye mechi za ushindani ndani ya ligi Feisal alifunga mabao hayo 13

Ukiweka kando hatari yake kwa mguu wa kulia pia Feisal alikuwa na hatari zaidi  ndani ya 18 ambapo alifunga jumla ya mabao 17 akiwa kwenye eneo hilo.

NJE YA 18

Mwamba Feisal  katupia mabao mawili akiwa nje ya 18. Bao lake la19 la kufungia msimu alipachika akiwa nje ya 18 dhidi ya Geita Gold walipokomba pointi tatu mazima ugenini.

PASI ZA MABAO

Feisal alitengeneza jumla ya pasi 7, alitoa pasi ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, Uwanja wa Lake Tanganyika dakika ya 68.

Wakati wakisepa na pointi tatu ugenini kwenye mchezo huo Feisal alitoa pasi mbili ile ya pili alitoa dakika ya 72 ilikuwa ni Novemba Mosi 2023.

HUSIKA KATIKA MABAO

Fei Toto
Feisalum akiwa kwenye uwanja wa mazoezi viunga vya Azam Complex. Source. Azam .

Feisal amehusika kwenye mabao 26 kati ya 63 yaliyofungwa na Azam FC ikiwa ni namba mbili kwa timu zilizofunga mabao mengi. Ukiweka kando kuwa namba mbili kwa safu kali ya ushambuliaji na ile ya ulinzi ni namba mbili ikiwa imeruhusu mabao 21.

Yanga na Azam FC zitaipeperusha bendera ya Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba na Coastal Union itakuwa ni kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Share this: