-----------------------------------------------n-----------------------------------------------n
EURO
Hatua ya Robo Fainali EURO

Mashindano ya EURO 2024 yanazidi kushika kasi ambapo leo Jumamosi hatua ya Robo fainali inatarajiwa kuhitimishwa  kwa michezo miwili ambapo England watavaana  na Switzerland huku Uholanzi wakivaana na Uturuki na mechi zote hizi unaweza kubashiri kupitia Kampuni namba moja ya michezo ya kubashiri nchini SportPesa kwa kutembelea www.sportpesa.co.tz

Hatua hiyo iliendelea jana usiku ambapo Ufaransa na Uhispania walifanikiwa kutinga hatua ya Nusu Fainali ya mashindano hayo baada ya kuziondosha timu za Ureno na wenyeji Ujerumani.

Ureno waliondoshwa kwenye EURO kwa changamoto ya mikwaju ya Penalti 5-3 mara baada ya dakika 90 na zile 30 za nyongeza, huku mchezaji pekee ambaye alikosa mkwaju wake wa Penalti akiwa ni Joao Felix.

Katika mchezo huo Ufaransa ambao wamekuwa wakikosolewa sana kwa makosa ya safu yao ya ushambuliaji waliacha Ureno watawale sehemu kubwa ya mchezo huo huku wao wakishambulia kwa kushtukiza.

ENGLAND KUPANGUA KIKOSI LEO

EURO
Harry Kane

Nahodha wa kikosi cha England, Harry Kane ameweka wazi kuwa wanatarajia kufanya mabadiliko ya mfumo na kikosi chao kuelekea mchezo wao wa leo Jumamosi dhidi ya Switzerland.

England wametinga hatua hiyo baada ya kuwaondosha kigumu Slovakia katika hatua ya 16 bora.

Kane amesema: “Tulipata faida ya kufunga miongoni mwa mabao bora katika historia ya soka la uingereza, ambalo amefunga Jude, na kama tutaibuka na ubingwa wa EURO, hiki ni kitu ambacho hatuwezi kukisahau ni tukio ambalo tulilihitaji kama timu.”

Huku England wakiendelea kushutumiwa kwa ubovu wa kiwango chao, Kane anaamini kuwa bado kuna vitu watu hawataki kuvizungumzia juu ya ubora wa kikosi chao kwenye EURO ikiwemo ukuaji wa ubora wa timu yao.

Kane ameendelea kusema: “Nadhani kocha amejitahidi kutuelekeza na kujitolea kila kitu, hivyo huu ni muda wetu sisi wachezaji kwenda kumlipa kwa kupambana kuonyesha kiwango bora, licha ya kwamba mara zote tumekuwa tukijitahidi kucheza vizuri.

“Tangu mara baada ya mchezo wetu na Denmark tumezungumza kama wachezaji kukumbushana umuhimu wa kufanya vizuri na tunatarajia mabadiliko makubwa dhidi ya Switzerland.

HIKI HAPA KIKOSI CHA ENGLAND KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO

EURO
England wakishangilia goli

Kuendana na mazoezi yaliyofanyika kikosi cha England kinachotarajiwa kuanza ni kama ifuatavyo; (3-4-2-1): 1. Pickford 2. Walker 3. Trippier 4. Stones 5. Konsa 6. Rice 7. Foden 8. Mainoo 9. Kane 10. Bellingham 11. Saka.

HABARI NJEMA KWA ENGLAND

Kuelekea mchezo wao wa leo kambi ya England imepokea habari njema za kurejea kwa staa wao na mlinzi wa kushoto wa timu hiyo, Luke Shaw taarifa ambayo imetolewa na kocha mkuu wa England, Gareth Southgate.

Luke Shaw alikuwa miongoni mwa mastaa ambao waliitwa kwa bahati ndani ya kikosi cha timu hiyo kushiriki EURO kwani aliitwa kwenye kikosi cha timu hiyo licha ya kutokuwa nba utimamu wa mwili wa asilimia 100, kufuatia kuwa amekaa nje ya uwanja kwa muda mrefu wa takribani miezi minne.

Licha ya hali hiyo lakini  kocha wa England, Gareth Southgate amekuwa akisisitiza kuwa bado wana matumaini makubwa kuwa nyota huyo ana nafasi ya kuiwakilisha England kwenye mashindano haya ya EURO.

Tayari, Southgate amethibitisha kuwa mlinzi huyo wa kushoto wa Man United yuko tayari kutumika kwenye mchezo wa leo dhidi ya Switzerland.

Shaw hajashuka uwanjani tangu mwezi Februari kufuatia majeraha ya misuli ya paja na wiki hii kwa mara ya kwanza ameonekana kurudi mazoezini.

Southgate amesema: “Ni kweli amekuwa kwenye wakati mgumu katika kipindi cha wiki kadhaa zilizopita, lakini najivunia kazi kubwa ambayo imekuwa ikifanywa na timu yetu ya matabibu na wataalamu wa utimamu wa mwili.

“Nafurahi amerejea na kutupa chaguzi zaidi kwani awali ilikuwa kazi ngumu kwetu kutengeneza uwiano wa kikosi chetu. Tungeweza kumrejesha tangu mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi,lakini hakukuwa na haja ya kumuwahisha kwa kuwa tulihofia huenda ingepelekea majeraha zaidi.

“Hatutarajii kumpa muda mwingi kwa kuanzia lakini hata atakapopata dakika 5 bado ana uwezo wa kuleta tofauti kubwa ya mchezo na hili ni jambo ambalo tumelishuhudia sana kwenye michuano hii”

 

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.