Kibu DennisKibu Dennis
Jean Baleke
Jean Baleke miongoni mwa washambuliaji waliopewa Thank You ndani ya Simba 2023/24. Source: Simba.

INASUKWA upya Simba kuelekea msimu wa 2024/25 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kambi ya maandalizi kwa kikosi hicho kilichomaliza Ligi Kuu Bara msimu wa 2023/24 nafasi ya tatu itakuwa ni nchini Misri.

Majembe yamezidi kutambulishwa ikiwa ni pamoja na kiungo mkabaji Augustine Okejapha ametambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kupata changamoto mpya. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2023/24 mabingwa ni Yanga inayodhaminiwa na SportPesa.

Haikuwa kazi nyepesi kwa Yanga kutwaa ubingwa huku Mtibwa Sugar na Geita Gold hizi zikishuka daraja hivyo kwa msimu wa 2024/25 zitashiriki Championship. Wapo waliokuwa wakichana mikeka na wapo ambao walikula kirahisi hata wewe unaweza jisajili ukawa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz 

Nyota huyo mpya ndani ya Simba ni raia wa Nigeria anatarajiwa kuwa kwenye changamoto mpya kwa msimu wa 2024/25 ndani ya Simba.

Julai 5 2024 Simba ilimtambulisha kocha mpya ambaye ni Fadlu Davis ambaye atafanya kazi na ingizo hilo jipya lenye miaka 23.

Julai 6 2024 nyota huyo mwenye miaka 23 nyota mpya wa Simba alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye eneo la ukabaji.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Habari za Michezo Bongo, Marco Mzumbe ameweka wazi kuwa kiungo huyo ni mtu wa kazi alikuwa anakipiga ndani ya Rivers United kabla ya kujiunga na Simba.

“Moja ya kiungo mwenye uwezo mkubwa kwenye eneo la ukabaji kwa kuwa hapo kulikuwa na tatizo kwa muda mrefu. Kumbuka kwamba awali kulikuwa na Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin hawa wote ni viungo wakabaji lakini sio asilia.

“Saini ya kiungo huyu ikiwa atafanya vizuri itakuwa ni faida kubwa kwa Simba kwa kuwa atakuwa anawapa kile kitu ambacho kilikosekana kwa muda mrefu. Hivyo ni suala la kusubiri kuona namna gani atafanya ndani ya uwanja kwa kuwa ni mchezaji mzuri.

“Usajili ambao unafanyika kwa sasa ndani ya Simba unawachukua wale wachezaji wenye tuzo kubwa kama ilivyo kwa Mnigeria huyu ambaye ni MVP akiwa na umri mdogo pia miaka 23.

“Pia Che Malone naye alisajiliwa ndani ya Simba akiwa ni MVP amekuwa akifanya vizuri ndani ya Simba kwenye mechi za ushindani hivyo kikubwa kila mmoja atakuwa kwenye majukumu yake ndani ya uwanja.”

Ukiweka kando nyota huyo pia Simba ilimtabulisha Valentino Mashaka ambaye ni kiungo mshambuliaji alikuwa akikipiga Geita Gold.

Ilikuwa ni Julai 5 2024 Valentino alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba. Huyu ni kiungo mshambuliaji ambapo alipokuwa ndani ya Geita Gold alikuwa ni chaguo la kwanza.

Rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 24 za ushindani ndani ya ligi na alifunga mabao sita akitoa pasi moja ya bao. Ikumbukwe kwamba Geita Gold itashiriki Championship msimu wa 2024/25 baada ya kushuka daraja.

HUYU HAPA NYOTA WA KWANZA

Nyota wa kwanza kutambulishwa ndani ya Simba ni Lameck Lawi ambaye ni beki aliyeibuka ndani ya kikosi cha Simba kutoka Coastal Union. Lawi alitambulishwa Juni 20 2024.

MUTALE

Joshua Mutale alitambulishwa ndani ya kikosi cha Simba Julai Mosi 2024 ikiwa ni siku Clatous Chama alitambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga akitokea ndani ya Simba.

MUKWALA

Steven Mukwala ni nyota mpya ndani ya kikosi cha Simba alitambulishwa Julai 2 2024 kuwa ndani ya kikosi hicho ambacho kitashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

JEAN

Jean
Jean ingizo jipya ndani ya kikosi cha Simba kuelekea 2024/25. Source: Simba.

Ingizo jingine jipya ndani ya Simba ni Ahoua Jean Charles ambaye alitambulishwa Julai 3 2024.

 

HAMZA

Nyota mwingine mpya ndani ya kikosi cha Simba ni Abdulrazack Mohamed Hamza alitambulishwa rasmi Julai 4 2024 kuwa ni nyekundu na nyeupe.

MASHAKA

Valentino Mashaka alitambulishwa ndani ya Simba Julai 5 2024 yeye ni kiungo mshambuliaji akitokea Geita Gold.

 

HAWA HAPA WALIKUTANA NA THANK YOU

BOCCO

Bocco
John Bocco nahodha wa Simba msimu wa 2023/24. Source: Simba.

Nahodha John Bocco anaingia kwenye orodha ya nyota wa kwanza kukutana na Thank You ilikuwa ni Juni 17 2024 alipoagwa mazima ndani ya Simba.

Ikumbukwe kwamba Bocco mwisho wa msimu aliwashukuru Simba na kuaga kutokuwa ndani ya kikosi hicho ambacho kiligotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

NTIBANZOKIZA

Kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza alifuata kupewa Thank You ilikuwa ni Juni 18 2024. Ikumbukwe kwamba wakati anasepa ndani ya Simba alikuwa namba moja kwenye utupiaji ndani ya kikosi hicho kilichokuwa kinanolewa na Juma Mgunda.

Mabao 11 alifunga akiwa na Simba na msimu wa 2022/23 alikuwa namba moja alitupia mabao 17 akitwaa tuzo ya kiungo bora, mfungaji bora na jina lake lilikuwa kwenye orodha ya wachezaji bora.

CHILUNDA

Shaban Chilunda kiungo mshambuliaji alikutana na Thank You Juni 19. Chilunda mkataba wake wa mwaka mmoja uligota mwisho hivyo hakuongezewa kandarasi nyingine.

LUIS

Kiungo wa kazi Luis Miquissone alikutana na Thank You kwa kuwa hakuongezewa mkataba mwingine ndani ya timu hiyo. Nyota huyo kwa sasa amejiunga na UD Songo ya Msumbiji aliyokuwa hapo kabla ya kuwa ndani ya Simba.

JUMA

Kenedy Juma beki wa kazi alikutana na Thank You, Juni 20 2024 baada ya kudumu ndani ya kikosi hicho kwa miaka mitano.

INONGA

Inonga
Inonga Baka beki aliyecheza mechi 10 za ligi msimu wa 2023/24. Source Simba.

Beki aliyedumu kwa misimu mitatu ndani ya Simba, Henock Inoga alikutana na Thank You Juni 24 2024. Mkataba wake ulikuwa unatarajiwa kugota 2025 walifikia makubaliano ya kusitisha mkataba.

BADO WAPOWAPO

MZAMIRU

Mzamiru Yassin   kiungo mkabaji bado yupo ndani ya kikosi cha Simba. Mkataba wake utakuwa mpaka 2026 ni Juni 25 alitangazwa kuongezewa mkataba mpya.

MWENDA

Israel Mwenda, beki wa kazi ameongezewa mkataba mpya mpaka 2026 hivyo ataendelea kuwa ndani ya kikosi hicho. Juni 25 alitangazwa kuongezewa mkataba mwingine.

KIBU

Mkandaji Kibu Dennis aliongezewa mkataba mpya ndani ya Simba mpaka 2026. Ikumbukwe kwamba alifunga bao moja ilikuwa dhidi ya Yanga.

 

Share this: