
WALIOCHEZA dakika kiduchu 2023/34 wapo kwenye timu nyingi ndani ya Bongo lakini kuna wale ambao walizua gumzo kutoka timu kubwa mbili Yanga inayodhaminiwa na SportPesa na Simba ambayo imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo.
Haikuwa kazi nyepesi kwa Yanga kutwaa ubingwa huku Mtibwa Sugar na Geita Gold hizi zikishuka daraja hivyo kwa msimu wa 2024/25 zitashiriki Championship. Wapo waliokuwa wakichana mikeka na wapo ambao walikula kirahisi hata wewe unaweza jisajili ukawa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz
Kwa sasa dirisha la usajili linaendelea huku kila timu ikiwa sokoni kufanya maboresho ndani ya timu husika kuelekea msimu wa 2024/25.
MASHINE MPYA SIMBA

Wekundu wa Msimbazi Simba sio kinyonge licha ya kiungo Clatous Chama kuibukia Yanga wametambulisha mashine nyingine ya kazi iliyokuwa Geita Gold. Ni nyota wa kazi anaitwa Valentino Mashaka yeye ni kiungo mshambuliaji.
Ikumbukwe kwamba alipokuwa ndani ya Geita Gold alicheza jumla ya mechi 24 na kufunga mabao sita kwenye ligi akitoa pasi moja ya bao hivyo alikuwa ni chaguo la kwanza ndani ya Geita Gold atakuwa kwenye changamoto mpya ndani ya kikosi cha Simba.
Wakati Simba wakimpa dili la miaka miwili, Yanga wamejihakikishia huduma ya kipa Aboutwalib Mshery ambaye atakuwa ndani ya timu hiyo mpaka 2027. Ikumbukwe kwamba Mshery aliibuka ndani ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar.
KETE 30 ZILIVYOKUWA
Kete zilizochezwa ilikuwa 30 ndani ya msimu wa 2023/24 ambazo ni dakika 2,700.Wachezaji walikuwa na kazi ya kuvuja jasho kusaka ushindi huku wengine wakikomba dakika kibao na wengine kiduchu. Tunakuletea mastaa kutoka mitaa ya Kariakoo, Yanga na Simba ambao walikomba dakika chache wakicheza chini ya mechi 15 namna hii:-
METACHA MNATA
Mechi nne alikaa langoni akitumia dakika 327, alifungwa bao moja na alikuwa hajafungwa kwenye mechi tatu. Kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja.
MSHERY
Kipa Mshery alikaa langoni kwenye mechi 6 alikomba dakika 438 alifungwa mabao 3 hakufungwa kwenye mechi 3.
KIBWANA SHOMRI
Beki wa kupanda na kushuka ndani ya Yanga ni mechi 10. Dakika 416 alikomba huku akitoa pasi moja kati ya mabao 71 ambayo yalifungwa na timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
MKUDE

Kiungo mkabaji ingizo jipya akitokea Simba baada ya kukutana na Thank You Jonas Mkude. Mechi 9 kacheza akikomba dakika 311.
NKANE
Wonder Kid, Dennis Nkane hakuwa chaguo la kwanza chini ya Gamondi akikomba dakika 60 kwenye mechi nne ambazo alicheza.
SKUDU
Mechi 11 alikomba dakika 413 alitoa pasi moja ya bao na alifunga bao moja pia namba 6 wa Yanga Skudu Makudubela.
GIFT
Gift Fred beki wa kazi ni mechi 9 ambazo alicheza ndani ya kikosi akikomba dakika 585 ndani ya kikosi cha Yanga kwa msimu wa 2023/24.
ZAWADI
Mechi 7 alipata nafasi ya kucheza ambapo alisepa na dakika 377 ni Zawad Mauya kiungo wa kazi ngumu ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni mabingwa wa ligi.
FARID
Kiungo huyu Farid Mussa alipata nafasi ya kucheza mechi 9 pekee ndani ya ligi akikomba dakika 350 msimu wa 2023/24.
SURE BOY
Salim Aboubhakar maarufu kama Sure Boy alicheza mechi 11 akikomba dakika 740 chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi.
SHEKHAN NA OKRA
Kiungo Shekhan Ibrahim huyu ni mechi sita alipata nafasi ya kucheza 131 ilikuwa dakika zake huku Kiungo mshambuliaji Okra ni mechi 8 alicheza na kukomba dakika 288.
HAWA HAPA MASTAA WA SIMBA
SALIM NA MANULA
Ally Salim mechi 6 dakika 540 fungwa mabao 6. Hakufungwa kwenye mechi moja. Aishi Manula hakuwa fiti ndani ya 2023/24 ni mechi nne alicheza akitunguliwa mabao 7 akikomba dakika 360. Hakufungwa kwenye mechi mbili.
HUSEN ABEL
Kipa huyu alikaa langoni kwenye mechi mbili alikomba dakika 180 huku akifungwa bao moja na hakufungwa kwenye mchezo mmoja.
MWENDA
Israel Mwenda beki wa kupanda na kushuka ni mechi 14 alicheza akikomba dakika 857.
Abdallah Khamis Mechi nne kacheza akikomba dakika 77 msimu wake wa kwanza ndani ya Simba.

BOCCO
Mechi 5 kacheza akikomba dakika 199 kafunga mabao mawili. Ni nahodha John Bocco ambaye hatakuwa na kikosi kwa msimu wa 2024/25.
KAMETA
David Kameta kacheza jumla ya mechi tano kafunga bao moja ilikuwa kwenye Mzizima Dabi dhidi ya Azam FC. Alikomba dakika 75.
INONGA
Henock Inonga ni mechi 10 alicheza ndani ya Simba akikomba dakika 687. Pia Hussen Kazi beki huyu ni mechi tatu alicheza akikomba dakika 210 ndani ya kikosi cha Simba.
CHILUNDA
Shaban Chilunda ni mechi tatu alicheza akikomba dakika 210. Yupo mwamba Edwin Balua
Mechi 11 kacheza akisepa na dakika 693 mabao aliyofunga ni mawili.
CHASAMBI
Ladack Chasambi mechi 9 kasepa na dakika 670 katupia mabao matatu kibindoni. Saleh Karabaka kiungo wa kazi kafunga bao moja akicheza mechi mbili ni dakika 57.
LUIS
Luis Miquissone ni mechi 19 kwenye ligi akitumia dakika 410 na kutoa pasi tatu zilizoza mabao ile ya tatu ilikuwa dhidi ya Ihefu Uwanja wa Mkapa alipa Moses Phiri mzunguko wa kwanza.

