
ROBO fainali ya mashindano ya Euro 2024 inatarajiwa kuanza kutimua vumbi rasmi Ijumaa hii ambapo kunatarajiwa kuwa na michezo miwili ya kukata na shoka.
Timu mbili ambazo zimekuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao yaani Uhispania na waliofunga mabao nane na Ujrerumani ambao wanaongoza kwa kufunga mabao mengi mpaka sasa wakiwa tayari wamefanikiwa kufunga mabao 10 wanatarajiwa kuvaana jijini Stuttgart.
Wakati Ujerumani wakionekana kupewa nafasi kubwa ya kutinga nusufainali mbele ya Uhispania, mchezo ambao unaonekana kuvuta hisia za watu wengi ni utakaozikutanisha Ureno ya Cristiano Ronaldo na Ufaransa ya nyota Kylian Mbappe.
Makala hii inakuchambulia kwa ufupi kuhusu namna gani hatua hiyo ya Robo Fainali inatarajiwa kuwa kama ifuatavyo, huku pia ukiwa na nafasi ya kushinda kwa kutabiri na kuweka mkeka wako na Kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa. Tembelea www.sportpesa.co.tz
Ujerumani Vs Uhispania
Uhispania ndio timu ambayo imepewa nafasi kubwa ya kuibuka na ubingwa wa mashindano haya kuendana na ubashiri wa mashine ya ‘computer’ lakini wanatarajiwa kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa Ujerumani.
Spain wanatajwa kuwa miongoni mwa timu zenye vikosi bora kwenye Euro ya mwaka huu, huku uwepo wa makinda wawili, Nico William na Lamine Yamal ukitajwa kuwa sababu kubwa ya makali ya Uhispania ya kocha Luis de la Fuente.
Ujerumani ya, Julian Nagelsmann nayo inaonekana kuwa kwenye mikono salama ya staa wao, Jamal Musiala. Kucheza kwenye ardhi ya nyumbani ni miongoni mwa sababu kubwa ambazo zinawafanya Ujerumani wapewe nafasi kubwa ya kufanya vizuri.
Yoyote ambaye atashinda mtanange huu anatazamiwa kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi ya kuibuka bingwa wa Euro 2024.
Ureno Vs Ufaransa

Hii inatajwa kuwa vita ya timu ambazo zina safu bora zaidi ya ushambuliaji kwenye makaratasi, lakini kiuhalisia timu zote mbili zinaonekana kujikongoja kwenye mashindano haya mpaka sasa.
Cristiano Ronaldo ameandika rekodi mbovu ya kuwa mchezaji ambaye amefanya majaribio mengi ambayo yamefeli akijaribu mara 20 bila kufunga bao lolote, akifuatiwa kwa karibu na staa wa Ufaransa, Antoine Griezmann, huku staa wao Kylian Mbappe naye akionekana kupoteza nafasi nyingi.
Mpaka sasa ndani ya kikosi cha Ufaransa nyota ambaye amekuwa na namba nzuri ni William Saliba ambaye wengi walibeza kuitwa kwakwe kwenye kikosi cha timu hiyo.
Safu imara ya ulinzi ambayo imeruhusu bao moja tu, tena la Penalti ya Robert Lewandowski ndio sababu inayowapa jeuri Ufaransa kutinga nusu fainali ya Euro ya mwaka huu. Baada ya kuimzuia vizuri Lukaku sasa wengi wanatamani kuona kama, Saliba anaweza kumzuia Ronaldo.
Ronaldo ameweka wazi kuwa anatarajia mashindano haya ya Euro kuwa ya mwisho kwake baada ya kuandika rekodi nyingi kali.
England vs Switzerland

Ni wazi kuwa England wanakwenda kukutana na miuongoni mwa timu bora sana katika hatua hii ya Robo Fainali.
Switzerland ndiyo timu ambayo hawapewi nafasi kubwa ya kufuzu nusu fainali ya mashindano haya kati ya timu zote nane.
Lakini ubora ambao walionyesha dhidi ya Hungary na Italy ni miongoni mwa sababu zinazowafanya kuwa timu ya kuchungwa.
Straika wao, Dan Ndoye mwenye umri wa miaka 23 tu, anatajwa kuwa nyota anayepaswa kuchungwa sana na England hasa baada ya kufunga dhidi ya Ujerumani.
Uholanzi Vs Uturuki
Arda Guler staa wa timu ya Taifa ya Uturuki amekuwa nyota ambaye ameonyesha wastani wa kiwango bora kwenye Euro ya mwaka huu.
Kocha mkuu wa Uturuki, Vincenzo Montella ameweka wazi kuwa anajivunia vijana wake ambao wanaonekana kupambana sana mpaka kufika hatua ya Robo Fainali.
Uturuki wanajivunia sapoti kubwa ambayo wanaipata kutoka kwa mashabiki wao, wngi wakiwa wamesafiri kutoka kwao na wale ambao wanavutiwa nao.
Sapoti kubwa ya Uturuki inafananishwa na sapoti ambayo Morocco waliipata kwenye makala iliyopita ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Saudia.
Straika wa Uholanzi, Cody Gakpo anatarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo dhidi ya Uturuki huku akicheza zaidi kama msaidizi wa mshambuliaji wa mwisho.
Cody Gakpo mpaka sasa ameisaidia Uholanzi kwa mchango wa mabao 3 akiwa na vita kubwa dhidi ya Mjerumani, Jamal Musiala katika kuweania tuzo ya ufungaji bora wa Euro 2024.

