SportPesa- AlphonceAlphonce Bonus Winner-Artboard - copy -
  • Milioni 5,349,439 za Jackpot ya SportPesa zaenda Kinyerezi

Dar-es-Salaam, 30 Mei, 2024 – Mkazi wa mkoa wa Dar es Salaam, wilaya ya Ilala, Alphonce. A. Fungo amejishindia Tshs 5,389,439 kama bonus ya Jackpot ya SportPesa baada ya kupatia kwa usahihi mechi 10 kati ya mechi 13.

Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za SportPesa jijini Dar-Es-Salaam, Alphonce anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2023  . ‘’Nilianza kucheza na Sportpesa mwaka 2023 mwezi kama huu wa tano, na katika kipindi chote hiko nimefanikiwa kushinda kiasi tofauti kama laki 8, laki 7, laki 3 na kiasi cha mwisho ni hiki ambacho nimebahatika wiki iliyopita ambacho ni zaidi ya milioni 5 ambazo zote nimeshinda kwenye Jackpot ya mechi 13.

SportPesa- Alphonce

SportPesa nimeifahamu muda mrefu, kwa mara ya kwanza niliona nikiwa Mbeya,mara nyingi  nikiwa na rafiki yangu sehemu ya kazi alikuwa akitumia muda mwingi kwenye simu yake, siku moja nilimuuliza huwa nakuona uko busy sana na simu yako, ndipo aliponiambia huwa natumia muda mwingi kupanga mikeka, ndipo nilipoanza kujifunza kucheza Jackpot, pia SportPesa ni kampuni ambayo haina longo longo kwenye ulipaji pale ambapo unakuwa umeshinda.

Akiongelea kuhusu mkeka alioshinda, Alphonce anasema huwa anachukua masaa mawili hadi matatu kuzikagua timu na kujua timu ipi ataipa ushindi.

‘’Mimi  napenda kutumia muda  mrefu wa kuangalia kwanza timu na kuzichambua kabla sijaweka mkeka wangu, na huwa natumia masaa mawili hadi matatu kupangilia mkeka wangu mara nyingi huwa naweka mikeka 20 hadi 30

Akiongelea kuhusu ushindi alioupata, Alphonce alisema niliweka mikeka 30, na kati ya hiyo miwili ndio imetoa ushindi.

Anaendelea kusema wakati anasubiri matokeo alikuwa na shauku kubwa sana baada ya kuona mkeka mmoja ameshinda mechi 9, hapo ndio alianza kuamini kuwa anaweza kuwa mshindi wa jackpot au ataweza kupata bonus.

Sportpesa-Alphonce mkeka

Nakumbuka mechi ya mwisho inachezwa nilikuwa maeneo ya nyumbani kwenye mida ya saa sita usiku, nilikuwa nimekaa nasubiria matokeo ya ushindi, na hapo hapo meseji iliingia, kwakweli nilifurahi sana, alisema Alphonce.

Aliendelea kuwashauri watanzania wasisite kucheza kwa wingi kwani Jackpot ya SportPesa ni halali, kinachotakiwa wacheze kwa umakini kwa kiasi ambacho wanaweza kukipoteza ili wasije wakashindwa kulisha familia. ‘’Nawaomba muitumie fursa hii kwani ndio njia ya uhakika kulamba mkwanja kama mimi’’.

Anamalizia kwa kusema fedha aliyopata ataongeza mtaji kwenye biashara zake, kumalizia makazi yake ambayo anajenga.

Akiongelea ushindi alioupata Alphonce Mkuu wa  kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano SportPesa, Sabrina Msuya alisema, inahamasisha kuona sisi kama SportPesa tunaendelea kubadilisha maisha ya watu kila siku, ushindi huu wa Alphonce uwape hamasa hata wale ambao hawaamini kuwa watu wanaweza kushinda pesa nyingi kuwa inawezekana, pia ningependa kumwambia Alphonce aendelee kucheza kwani nina amini ipo siku huenda atabahatika kushinda Jackpot yote.

 

“Niwakumbushe watanzania Jackpot ipo na itaendelea kuwepo kila wiki kutegemeana na lini haswa inatoka. Endeleeni kutuamini kama ambavyo Alphonce ametuamini na matokeo ya ushindi mtayapata’’ alimaliza Sabrina.

Share this: