YANGA-AZIZ KI
https://sportpesa.co.tz/YANGA
Nembo ya Shirikisho la soka Afrika, CAF

BAADA ya bongo Yanga kuibuka mabingwa msimu huu wa 2023/24, ligi mbalimbali za soka barani Afrika kwa msimu huu tayari zimemalizika, ambapo tayari sehemu ya kubwa ya wawakilishi wao katika mashindano ya kimataifa yaani Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho wamejulikana.

Kwa kawaida kanuni za uwakilishi wa mashindano ya Afrika zinatofautiana kuendana na pointi ambazo nchi husika imekusanya katika mashindano hayo ya kimataifa.

Kwa mataifa ambayo yamekusanya pointi nyingi zaidi katika mashindano hayo katika kipindi cha miaka mitano huwakilishwa na timu nne, ambapo timu mbili zilizomaliza nafasi ya juu kwenye ligi za mataifa yao huenda katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na timu mbili zilizomaliza nafasi ya tatu na ya nne hushiriki mashindano ya Kombe la Shirikisho.

Kwa mataifa ambayo yamekusanya pointi chache hupeleka timu mbili pekee kwenye mashindano ya kimataifa ambapo timu bingwa kwenye mashindano ya Ligi zao hushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na timu iliyomaliza nafasi ya pili huenda kwenye Kombe la Shirikisho.

MPAKA SASA HIZI HAPA TIMU ZILIZOFUZU LIGI YA MABINGWA AFRIKA
Al Ahly, Mamelodi Sundowns, AS FAR, Raja CA, MC Alger, Orlando Pirates, SC Villa, APR, FC Nouadhibou, Yanga, Azam, Teungueth FC, Mbabane Swallows, Gor Mahia, Vital’O, Arta Solar, Jwaneng Galaxy, Watanga, Saint Louis, Bo Rangers, Red Arrows, AS Psi, AS Douanes, Leopards de Dolisi, San Pedro, Lioli, Nyasa Big Bullets, Djoliba.
Orodha hii inatarajia kuendelea kuongezeka timu kutoka kwenye nchi ambazo ligi zao zinaendelea kutamatika.

VIPI KUHUSU TANZANIA?

Msimu wa Ligi Kuu Bara 2023/24 umemalizika ambapo tayari kila kitendawili kilichokuwa kinazua maswali kimepatiwa majibu.

UWAKILISHI KIMATAIFA
Msimu ujao Tanzania itaendelea kuwakilishwa na timu nne kimataifa ambapo mabingwa wanaojivunia nguvu kubwa ya udhamini wa Kampuni ya michezo ya  SportPesa Yanga na waliomaliza nafasi ya pili Azam watacheza Ligi ya Mabingwa Afrika, huku Simba na Coastal Union wakishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

AZIZ KI MFUNGAJI BORA

https://blog.sportpesa.co.tz
Kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz KI

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki ameibuka mfungaji bora akimaliza msimu kwa kufunga mabao na 21 na kumshinda mshindani wake mkubwa, Feisal Salum wa Azam FC ambaye amemaliza na mabao 19.

Baada ya mafanikio hayo, Aziz KI ambaye ni mfungaji bora amesema: “Ninachukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa mambo yote, ulikuwa ni msimu wenye ushindani mkubwa na kila mmoja ameona na napenda kuwashukuru mashabiki, benchi la ufundi na wachezaji wenzangu kwa ushirikiano waliokuwa wakinipa kila siku mpaka kufikia hatua hii, ni wazi isingewezekana bila wao kunisaidia kuanzia mazoezini mpaka uwanjani.

COASTAL UNION NA REKODI YA KIMATAIFA
Coastal Union ambao walimaliza mchezo wao wa mwisho kwa suluhu mbele ya KMC wameandika rekodi ya kukata tiketi ya ushiriki wao kimataifa msimu ujao.

Coastal na pointi zao 43 wanaungana na Simba kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

DIARRA APINDULIWA

https://sportpesa.co.tz/YANGA
Mlinda mlango wa Yanga, Djigui Diarra

Mlinda mlango namba moja wa Yanga raia wa Mali, Djigui Diarra baada ya kuibuka na tuzo ya kipa bora wa msimu wa Ligi Kuu Bara kwa misimu miwili hatimaye amepoteza taji hilo.

Ni mlinda mlango wa Coastal Union, Ley Matampi ambaye amepeleka machungu kwa mlinda mlango huyo wa Yanga baada ya kucheza jumla ya mechi 24 na kufanikiwa kukusanya ‘clean sheet 15’ huku Dijigui Diarra wa Yanga baada ya kukaa langoni kwenye mechi 21 amekusanya clean sheet kwenye mechi 14 pekee.

Walinda milango hao wawili walikuwa kwenye vita yao bora na kali ya kusaka nyota ambaye atamaliza msimu akiwa na clean shjeet nyingi zaidi yaani kusimama langoni bila kuruhusu bao kwenye michezo mingi.

Baada ya vita ya msimu mzima hatimaye Matampi ametupa majibu ya nani mkali wa kuokoa michomo ya washambuliaji kwa msimu huu wa 2023/24.
Kabla ya Diarra na Matampi kiti hiko cha mlinda mlango bora kilikaliwa na mlinda mlango namba moja wa Tanzania, Aishi Manula kwa kipindi cha misimu zaidi ya sita ambapo kwa upande wake bado anauguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji wa nyonga, ambapo tangu amerejea bado anapambana kurudisha utimamu wakle wa mwili.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.