Timu mbili Tanzania Yanga na Simba zaandika rekodi kubwa kwenye soka la Afrika wakitinga robo fainali kibabe
Mgeni rasmi Henock Inonga alifanya kazi kubwa kutimiza majukumu yake
UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wachezaji wote wa timu hiyo wakiongozwa na beki wa kati Henock Inonga wanastahili pongezi kwa kutimiza majukumu yao kwa umakini Machi 2 2024 dhidi ya Jwaneng Galaxy na Simba wakitinga robo fainali kibabe.
Ipo wazi kwamba uwezo mchezo huo wa Vita ya Kisasi beki wa kati Inonga ambaye anavaa jezi namba 29 alikuwa ni mgeni rasmi katika msako wa pointi tatu muhimu.
INONGA UWEZO WAKE BALAA

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa Inonga ni mchezaji wa viwango na jitihada zake zipo kwenye mechi zote akiwa ni mchezaji pekee ambaye timu ya taifa ya DR Congo iligotea nafasi ya nne kwenye AFCON 2023.
Mashindano ya AFCON yaliyofanyinka Misri Inonga alikuwa akivuja jasho kwenye timu ya taifa ya DR Congo akiwa ni chaguo la kwanza la benchi la ufundi jambo ambalo lilikuwa ni sababu kutajwa kuwa mgeni rasmi ndani ya kikosi cha Simba kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Simba kwenye uwezo huo ilishuhudia dakika 90 zikikamilika bila kufungwa jambo ambalo limempa furaha Kocha Mkuu wa timu hiyo mwamba Abdelhak Benchikha ambaye amesema kuwa ni kazi kubwa ilifanywa na wachezaji kiujumla.
USHINDI ULIOIPELEKA SIMBA ROBO FANALI
Ipo wazi kuwa kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 6-0 Jwaneng Galaxy ambapo Inonga alianza kikosi cha kwanza na alivuja jasho mwanzo mwisho bila kufanyiwa mabadiliko kwenye mchezo huo Simba wakiandika rekodi ya kutinga hatua ya robo fainali wakiungana na watani zao wa jadi Yanga.
Ni Saido Ntibanzokiza alifungua pazia la utupiaji dakika ya 7, Pa jobe dakika ya 14, Kibu Dennis dakika ya 22, Clatous Chama alifunga bao dakika ya 76, Ladack Chasambi aliyeanzia benchi alifunga bao dakika ya 85 na Fabrice Ngoma ilikuwa dakika ya 89.
Yanga ambayo kwenye ligi inaongoza ikiwa inadhamiwa na Kampuni ya SportPesa ina jumla ya pointi 43 na kinara wao kwenye utupiaji ni kiungo Aziz KI mwenye mabao 10 sawa na namba yake ya jezi anayovaa akiwa kwenye kutimiza majukumu ndani ya Yanga.
Rekodi zinaonyesha kwamba kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy Inonga alipiga jumla ya pasi 50 na mguu uliotoa pasi nyingi ulikuwa ni ule wa kulia huku akionyesha uwezo mkubwa kwenye kukokota mpira kuwafuata wapinzani wao kimataifa.
AYOUB LAKRED LANGONI

Kwenye mchezo huo ambapo langoni alianza Ayoub Lakred ambaye alikosekana kwenye mchezo uliopita dhidi ya ASEC Mimosas kutokana na adhabu ya kadi za njano na mbili alionyeshwa dhidi ya Wydad Casablanca.
Kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng alianza na ilikuwa kazi kubwa kwa kila mchezaji kushirikiana na wachezaji wengine kuhakikisha kwamba lango linakuwa salama na mabao mengi yanapatikana ili kuongeza nguvu ya kupata ushindi kwenye mchezo huo wakundi B.
Inonga aliokoa hatari mara sita kwenye mchezo huo ilikuwa dakika ya 8, 9, 25, 31, 58, 64 pasi yake ya kwanza kipindi cha pili alitoa dakika ya 50 alitumia mguu wake wa kulia na ilimfikia mlengwa.
Kipa Lakred yeye aliokoa hatari nne ilikuwa dakika ya 21, 23,41 na 50 na alikamilisha dakika 90 bila kuonyeshwa kadi ya njano kwenye mchezo huo sawa na Inonga ambaye naye alikamilisha dakika 90 bila kuonyeshwa kadi ya njano.
Ally amebainisha kuwa kila mchezaji ndani ya kikosi cha Simba anajituma kwa nguvu kuhakikisha kwamba wanapata matokeo chanya jambo ambalo lilidhihirika kwenye mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy.
“Tulikuwa tunahitaji ushindi kwenye mchezo wetu na ilikuwa hivyo kila mchezaji alijituma kwenye kutimiza majukumu yake sio mgeni rasmi pekee Inonga bali kila mmoja alifanya kazi yake ilionekana katika uwanja kwenye kufanya kazi ya kusaka ushindi.
“Muhimu kutinga hatua ya robo fanali na imekuwa hivyo Wanasimba wamefurahi, wachezaji wamefurahi hili ni jambo kubwa na linapaswa kuwa endelevu kila wakati. Hakuna ambaye amezimia kwa kuwa haya ni maisha yetu ambayo tunayaishi kila siku.
“Uzuri ni kwamba benchi la ufundi linatambua uimara uliopo ndani ya kikosi pamoja na malengo yaliyopo, kufika hatua ya robo fainali ikiwa ni mara ya nne hii ni rekodi kubwa ambayo hufanywa na timu kubwa,” amesema.
REKODI KUBWA ROBO FAINALI
Simba inaungana na Yanga kwenye hatua ya robo fainali wakisubiri droo kuchezwa kumtambua mpinzani wao katika hatua hiyo na mshindi atakwenda hatua ya nusu fainali.
Kutoka kundi B Simba imekusanya pointi 9 huku Yanga ikiwa na pointi 8 kutoka kundi D kinara ni Al Ahly kundi D huku ASEC Mimosas akiwa ni kinara kundi B.

