HUKU balaa la kiungo, Zouzoua Pacome wa Yanga likiendelea kuwapa shangwe mashabiki wa Yanga la ushindi mkubwa dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria juzi Jumamosi, habari njema kwao ni kuwa ushindi huo umewafanya wavune kiasi cha zaidi ya Sh2.3 bilioni kutoka Shirikisho la soka Afrika (CAF) kwa kutinga robo fainali kama sehemu ya zawadi ya kufuzu hatua hiyo.

Yanga ambao wanadhaminiwa na Kampuni ya michezo ya SportPesa juzi Jumamosi wakicheza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CR Belouizdad katika mchezo wa mkondo wanne wa kundi D la Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo wamefanikiwa kufuzu hatua hiyo huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Mpaka sasa Yanga ambao wana udhamini mono wa kampuni ya michezo ya SportPesa wanakamatia nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi D, wamesaliwa na mchezo mmoja dhidi ya Mabingwa watetezi, Al Ahly ya Misri mechi itakayopigwa Ijumaa hii.

yangasc
Kocha Mkuu YangaSc

KUHUSU PACOME, ROBO FAINALI KOCHA GAMONDI ANASEMAJE?

Kocha mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi akizungumzia ubora ulioonyeshwa na mastaa wake akiwemo Pacome na nafasi yao ya kucheza Robo Fainali amesema bado wana kazi kubwa ya kufanya, huku malengo yao yakiwa ni kuongoza kundi lao, ikumbukwe droo ya Robo fainali inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.

Gamondi amesema: “Nimefurahia kuona tumejihakikishia nafasi ya kucheza robo fainali baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Belouizdad, lakini bado tunafikiria kwenda Misri kuwafuata Al Ahly tukiwa na malengo ya kusaka ushindi.

“Tunajua kuna faida kubwa, ikiwa tutafanikiwa kumaliza kinara wa Kundi D ambapo haitakuwa na ugumu mkubwa kuelekea droo ya nani wtutakutana naye kwenye hatua ya robo fainali na ni muhimu kuanza kujifunza kuzitumia nafasi tunazotengeneza ili kupata mabao mengi, kwani hata juzi tulistahili kushinda kwa idadi kubwa zaidi.

“Kwangu bado safu ya ushambuliaji inaonekana kuwa na baadhi ya madhaifu, tunatengeneza nafasi nyingi lakini tunatumia chache lakini pia hata ukiangalia kwenye eneo la ulinzi kuna makosa madogomadogo, tunapaswa kurekebisha na naamini tukifanya hivyo tutakuwa na timu bora Afrika kwenye ushindani.

“Mimi ni kocha ninayependa kushinda wakati wote, kila mtu anajua namna ambavyo tulipambana na Ahly hapa, ni klabu kubwa na bora lakini kila kitu kinawezekana tutakwenda kujaribu kwenda kucheza kwa akili kubwa tutafute ushindi hukohuko kwao.”

PACOME AITEKA SHOW

Kiungo wa kimataifa wa Yanga inayopewa jeuri na Kampuni ya SportPesa, Zouzoua Pacome  ndiye nyota aliyefanya balaa kubwa katika pambano hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambapo staa huyo alikuwa kwenye kiwango bora na kufanikiwa kusaidia upatikanaji wa bao moja la, Kennedy Musonda kupitia asisti yake.

Pacome pia alihusika moja kwa moja kuhakikisha mabao mengine matatu ya Yanga yanapatikana na wanapata ushindi huo wa kihistoria ambao unawapeleka Yanga Robo Fainali ya mashindano hayo kwa mara ya kwanza kwenye historia ya klabu hiyo.

Mchezaji wa YangaSC Pacome,
Pacome Waarabu

SPORTPESA KUONGEZA MZIGO WA HELA KWA PACOME, YANGA

Achana na faida ya nguvu ya fedha ambayo imeipeleka Yanga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza, kama mdhamini mkuu wa Yanga, Kampuni ya SportPesa inatarajiwa kuiongezea bonus Yanga kwa kufanikiwa kutinga atua hiyo, kama sehemu ya makubaliano ya udhamini.

SportPesa kwa kushirikiana na wafadhili wengine wakiwemo GSM wanatajwa kuwaongezea wachezaji hao zaidi ya kiasi cha Shilingi Milioni 300.

Hii ina maana kuwa mastaa wa timu hiyo wakiongozwa na, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz KI, Djigui Diarra na Kennedy Musonda watazidi kuoga minoti kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo.

Imefichuka kuwa kabla ya mchezo huo mabosi wa Yanga walifanya kikao na wachezaji wao na kuweka ahadi mbalimbali kutokana na ukubwa wa ushindi ambao wataupata katika mchezo huo na ndio maana uliona juzi wachezaji wa Yanga walipofunga bao la nne ‘vibe’ liliibuka kwa wale wa ndani na wale waliokuwa benchi ambapo walikuwa wakionyesha vidole vinne.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.