Muda kimataifaMuda kimataifa

Yanga  wanalitaka jambo hili kubwa 2024

Waarabu wa Misri kukutana na balaa zito la mastaa wote

Pacome Day yaacha gumzo kila kona

YANGA wanalitaka jambo hili kubwa 2024  kwa kupata ushindi dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wao wa mwisho watakaokuwa ugenini ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kila timu kupiga hesabu kukomba pointi tatu muhimu ili waongoze kundi hilo.

Kazi kubwa ilifanyika Februari 24 wakati kiungo wa Yanga Pacome Zouzoa akiingia kwenye orodha ya wachezaji waliofanya kazi kubwa katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Waarabu wa Algeria CR Belouizdad.

Ipo wazi kuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakati timu zote zikisaka ushindi mwisho ubao ukasoma Yanga 4-0 CR Belouizdad.

YANGA HESABU KUBWA KIMATAIFA

Yanga wanapiga hesabu kubwa kimataifa baada ya kupata ushindi mkubwa kwenye anga la kimataifa chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi katika anga za kimataifa wakilipa kisasi cha mchezo wa kwanza waliocheza wakiwa ugenini.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo waliocheza ugenini nchini Algeria Yanga ambao wanadhaminiwa na kampuni ya SportPesa ndani ya Ligi Kuu Bara walipoteza kwa kufungwa jumla ya mabao 3-0.

Kwenye mchezo wa kundi D uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikuwa ni Pacome Day Kitaalamu zaidi na utaalamu ulionekana kweli kwa kila mchezaji kufanya kweli katika kusaka ushindi.

YANGA HESABU KUBWA KWENYE MABAO

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa kila kipindi ambapo kipindi cha kwanza ni bao moja pekee lilifungwa kupitia kwa mwamba Mudathir Yahya ikiwa ni hesabu kubwa zilikuwa zinapigwa kwa wawakilishi hao wa Tanzania kimataifa.

Kiungo huyo kama kawaida yake akiwa ndani ya 18 alipachika bao hilo na kuanza kushangilia kwa mtindo wa kupiga simu jambo lilipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga.

Mashabiki wa Yanga wengi walijitokeza uwanjani wakiwa wamevaa uzi wenye nembo ya SportPesa kifuani kwa kuwa hawa ni wadhamini wa Yanga na walikuwa na furaha mwanzo mwisho kutokana na burudani iliyokuwa inatolewa uwanjani.

Kipindi cha pili Gamondi alirejea uwanjani kwa mbinu tofauti kabisa kwa kushambulia haraka huku akiwashtukiza Waarabu ambao walikuwa hawaamini walichokuwa wanakiona.

Bao la Mudathir ambaye alifunga dakika ya 43 liliongezewa nguvu na kiungo mwenye balaa kwenye mapigo huru Aziz KI ilikuwa dakika ya 47 muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.

Wakati Waarabu wakiwa kwenye mwendo wa kutafuta angalau bao kwenye mchezo huo dakika ya 48 mwamba Kennedy Musonda alifanya kazi yake aipendayo kwa kufunga bao dakika ya 49 ikiwa ni muda mfupi tangu wafungwe bao moja wapinzani wao.

GUEDE ANA BALAA HUYO

Mwamba Joseph Guede ambaye ni mshambuliaji mpya wa Yanga alikamilisha Pacome Day na Yanga kutinga hatua ya robo fainali kibabe kwa bao lake la ushindi dakika ya 83. Yanga inakwenda hatua ya robo fainali ikiwa na mchezo mmoja wa kumalizia kazi dhidi ya Al Ahly.

Baada ya kumalizana na CR Belouizdad Uwanja wa Mkapa, Februari 24 kete inayofuata ni dhidi ya Al Ahly mchezo unaotarajiwa kuchezwa Machi Mosi.

Al Ahly kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ina pointi 9 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kundi D ina pointi 8 zote zimekata tiketi ya kufuzu robo fainali mchezo huo utaamua nani atamaliza akiwa ni kinara wa kundi.

Gamondi ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo wao ujao dhidi ya Al Ahly utakuwa mgumu lakni wanakwenda kwa lengo la kuonyesha ushindani na kutafuta pointi tatu muhimu ugenini.

“Mchezo utakuwa mgumu tunatambua kwamba Al Ahly ni timu imara ambacho tunakwenda kufanya ni kusaka ushindi kwa kuwa inawezekana,”.

Pacome Waarabu
KIUNGO wa Yanga Pacome akionyesha uwezo wake wa kuwaondoka wapinzani mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Uwanja wa Mkapa Source Yanga

PACOME MTAALAMU KWELIKWELI

Mwamba Pacome alionyesha utaalamu wake kwelikweli  alitumia mguu wa kulia kutoa jumla ya pasi 37, pasi tatu kwa mguu wa kushoto, alikokota mpira mara 15 na alipiga mashuti yaliyolenga lango mawili miguso kwa kichwa ilikuwa mara mbili alitoa pasi moja ya bao kwenye mchezo huo.

Katika pasi alizotoa kwa mguu wa kulia ni nne pekee hazikuwafikia walengwa aliokuwa akiwapa ndani ya uwanja alipokomba jumla ya dakika 90 kwenye mchezo huo.

Ukiweka kando Pacome mwenye mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kipa Djigui Diarra langoni aliokoa hatari saba ilikuwa dakika ya 4, 16, 45, 60,66, 85 na 88.

Pacome amesema kuwa ni furaha kwa timu kiujumla kwa malengo yao kupata ushindi pamoja na mashabiki kupata furaha waliyokuwa wakiifikiria kwa muda mrefu.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumepata kwa kilichotokea kwetu ni furaha, tunawashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu ambao ulikuwa ni muhimu kupata ushindi,”.

 

 

Share this: