Inonga na BenchikhaInonga na Benchikha

Kisasi kulipwa dhidi ya Jwaneng Galaxy iliyosababisha maumivu kwa mashabiki wa Simba 

Mashabiki waitwa kwa wingi na tiketi zimeshaanza kuuzwa 

HENOCK Inonga namba 29 mgeni rasmi kimataifa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 2 2024. Mchezo huo ni wa maamuzi kwa timu itakayokwenda hatua ya robo fainali kimataifa.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo huku wakiwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuwa sehemu ya timu hiyo siku ikitinga hatua ya robo fainali.

HENOCK INONGA MGENI RASMI

“Mgeni rasmi katika mchezo dhidi ya Jwaneng Galaxy ni Henock Inonga sababu ndio mchezaji pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ameifikisha timu yake ya taifa kwenye nafasi ya nne kwenye AFCON 2023.

“Kila mmoja anatambua ubora wake na uwezo wake lakini hakuna sababu ya kutaka kufanana na Inonga, kila mchezaji aendelee kuishi maisha yake na kuwa yeye hii ni heshima anapewa Inonga ikiwa ni maalumu kwa ajili yake kutokana na kazi yake.

YANGA KUFUZU MO ATAJWA

“Kufuzu kwa Yanga katika hatua ya robo fainali wa kushukuriwa ni Rais wa heshima wa Simba ni Mohammed Dewji na wa pili ni Simba SC.

Inonga ASEC
Inonga ASEC

“Wakati Mo anakuja kuwekeza Simba alisema vision yake ni kushinda ubingwa wa Afrika na baada ya hapo tukaanza mchakato wa kutawala soka la Afrika.

“Wakati Mohammed Dewji anatengeneza dira ya kutawala soka la Afrika vilabu vingine vilikuwa vimelala usingizi wa pono, vilikuwa haviwazi kushindana Afrika na kusumbua.

“Baada ya miaka mitano ndio na wengine wameamka na wenyewe kutaka kuanza kufanya vizuri. Kama Simba Mohammed Dewji tungeendelea kulala basi hadi sasa hakuna klabu yoyote Tanzania ingekuwa na hasira, malengo ya kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika ndio maana nasema robo fainali yao ya kwanza wa kushukuriwa ni Mohammed Dewji ndio aliwaamsha watu kutoka kwenye usingizi. Huu ndio ukweli ambao utadumu milele.

HAMASA WAO NI WATAALAMU

“Kama kawaida kutakuwa na hamasa, na sisi ndio wataalamu wa hamasa. Wiki iliyopita nimeona hamasa za kitoto. Wiki hii tutafanya hamasa kubwa mno na tutafanya kwa ubora.

“Jumatano tutafanya uzinduzi wa hamasa katika tawi la Tunawakera lililopo Keko Maduka Mawili kuanzia saa 3 asubuhi. Msafara utaanzia Keko Furniture.

“Tarehe 29 tutafanya hamasa ndani ya mabasi ya mwendokasi kuanzia saa 3 asubuhi katika kituo cha mwendokasi Gerezani muhimu uvae jezi yako ya Simba. Kutakuwa na mabasi maalumu ambayo tutazunguka mjini hapa kupiga kampeni. Hii sio mara ya kwanza kufanya kampeni kwa kutumia chombo cha moto, tulishawahi kufanya kwenye treni, tumewahi kufanya pia kwenye pantoni na muda huu ni ndani ya mwendokasi.

“Tulichobakiza kufanya ni hamasa kwenye ndege na sababu Air Tanzania ni wadhamini wetu ipo siku tutakodi ndege kwenda Dodoma tukifanya kampeni.

KUHUSU KUWAOGOPA WAPINZANI

“Sisi hatuwaogopi Jwaneng Galaxy, uoga ni kwa mtu dhaifu lakini la muhimu ni tahadhari kwa 100% ili yasije tokea ya mwaka 2021.

“Tarehe 2 ya mwezi wa tatu tunakwenda kushinda tena ushindi wa kihistoria na kwenda robo fainali. Jwaneng tunamheshimu lakini amekuja wakati mbaya. Tiketi zimeshaanza kuuzwa na niwakumbushe Wanasimba rekodi zote ambazo tuliziweka, ziliwekwa na Wanasimba wenyewe. Wakati tunamfunga AS Vita mara 2, wakati tunamfunga Horoya mabao 7 ushindi wote ulitokana na mashabiki wa Simba. Ili tumnyoe Jwaneng tunawahitaji Wanasimba.

TIKETI ZIMEANZA KUUZWA

“Kuna tiketi za Platinum kwa Tsh. 150,000. Utapata kifurushi maalumu kutoka Simba, usafiri kutoka hotelini hadi uwanjani ukiwa na escort pamoja na chakula.

“Tumeongeza kifurushi kingine kinaitwa Tanzanite, hii anayenunua anakaa pale VVIP, kama akija Infantino au Mhe. Rais Samia unakaa nae eneo moja. Hii inauzwa Tsh. 200,000. Unapata car gate pass, chakula na vinywaji. Watu wa Tanzanite na Platinum wapige simu 0742771311.

“Vilevile tuna Mnyama Package, watu kuanzia 20 ambao watanunua tiketi kwa pamoja watapewa car gate pass na kukaa sehemu moja wakiwa uwnajani. Lakini pia tuna Executive Tickets hii ni kwa ajili ya makapuni au mashirika, tutawapa na car gate pass.

“Tangu jana tiketi zinapatikana na nitoe rai kwa Wanasimba wanunue tiketi haraka iwezekanavyo. Mechi hii tunataka mashabiki waujaze Uwanja wa Mkapa, mechi hii ni muhimu na ni jukumu la kila Mwanasimba kuipeleka Simba robo fainali. Njoeni wote Simba ni yetu sote. Watu 60,000 tunawahitaji.

“Maumivu ya Oktoba 24, 2021 hakuna Mwanasimba ambaye ameyasahau na hakuna ambaye atasahau, Jwaneng Galaxy walitusababishia maumivu haya. Asante Mungu muda umefika wa kwenda kufuta haya maumivu.

“Vita ya kisasi kila mtu anatakiwa kutumia silaha yake, Mwanasimba mwenye silaha yoyote, dua yoyote afanye tukamfanye vibaya Jwaneng Galaxy. Tukishinda tutakuwa na faida tatu, moja kuingia robo fainali, ya pili kulipa kisasi na ya tatu kuingia kwenye historia kuingia robo fainali mara nne mfululizo,” .

Share this: