Muda KMCMuda KMC
  • Mwamba Mudathir ana balaa ndani ya uwanja
  • Mudathir balaa lake kwenye mabao ya usiku
  • Anaingia kwenye rekodi ya mfungaji wa kwanza Yanga

MWAMBA MUDATHIR NA BALAA LAKE

MWAMBA Mudathir ana balaa zito  Yanga kutokana na kasi yake kwenye kufunga mabao ndani ya uwanja kwenye mechi za ushindani Ligi Kuu Bara jambo ambalo limekuwa likimuongezea tabasamu yeye pamoja na mashabiki wa timu hiyo.

Ikumbukwe kwamba Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wakiwa wanaongoza ligi na pointi 43 wanadhaminiwa na kampuni ya SportPesa inayowadhamini pia Singida Fountain Gate, Namungo hizi zote zimekuwa zikifanya vizuri kwenye mechi za ushindani.

Kiungo Mudathir Yahya kwenye mechi za hivi karibuni alikuwa kwenye ubora wake akifanikisha majukumu ya klabu hiyo yenye maskani yake Jangwani kukomba pointi tatu kwenye mechi tatu mfululizo huku akifunga mabao ya usiku ndani ya mechi mbili zilizochezwa Uwanja wa Azam Complex.

MWAMBA MUDATHIR FEBRUARI KAKIMBIZA

Februari kwa nyota huyo anayeshangilia kwa mtindo wa kupokea simu kila anapofunga bao ilikuwa ni yenye furaha kwake na mashabiki wa Jangwani kutokana na kutumia nafasi alizopata kwenye mechi za Ligi Kuu Bara iwe ni nyumbani ama ugenini.

Ipo wazi kuwa Ligi Kuu Bara ina ushindani mkubwa kwa kila timu kuonyesha nia ya kusaka pointi tatu nah ii inasababishwa pia na timu ambazo zinadhamiwa na kampuni ya SportPesa kuwa na dau lao wakimaliza kwenye nafasi za juu.

Hata Yanga pia ilipotwaa ubingwa msimu wa 2022/23 ilipongezwa na SportPesa ambao ni wadhamini mkuu jambo ambalo linaongeza kasi kwa kila timu kupambana kuhakikisha malengo yanakamilika kwa wakati kwa kukusanya hesabu mapema.

Muda KMC Goal
Muda KMC Goal

Ndani ya Februari kiungo huyo mzawa alifunga mabao dakika za jioni kwenye mechi za ligi wakati mashabiki wakiamini kazi ilikuwa imeisha kutokana na ugumu waliokutana nao ndani ya dakika 80 kwa wapinzani wao.

Wakati wakihesabu kuwa ngoma ni nzito kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji hapo mwamba Mudathir aliibuka na kulainisha mambo kisha kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa aliibuka shujaa kwa mara nyingine tena.

Ipo wazi kwamba kwenye mechi hizo ambazo aliibuka shujaa alifunga mabao ya ushindi katika dakika ya 85 kwenye mechi hizo.mbili rekodi inayoonyeshwa kwamba hana jambo dogo akiwa uwanjani akishirikiana na wachezaji wengine kusaka ushindi.

Mabao aliyofunga kwenye mechi hizo mbili wakiwa nyumbani vinara hao wa ligi walikomba pointi zote tatu jumlajumla huku wapinzani wao wakiambulia patupu kwenye mchezo huo ndani ya dakika 90.

Katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Dodoma Jiji huku bao likifungwa kipindi cha pili dakika ya 85 na pointi zikabaki Jangwani.

Mchezo dhidi ya Mashujaa bao la dakika ya 85 kutoka kwa Mudathir lilitosha kuipa Yanga ushindi wakakomba pointi tatu ubao uliposoma Yanga 2-1 Mashujaa ya kutoka Kigoma.

MUDATHIR BALAA LAKE AWA WA KWANZA

Mwamba Mudathir balaa lake halijapoa kutoka mzunguko wa kwanza ameingia mzunguko wa pili na kasi ileile ya kusaka ushindi huku akifunga mabao mawili kwenye mchezo mmoja peke yake.

Nyota huyo kwenye mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya KMC ubao wa Uwanja wa Jamhuri Morogoro uliposoma KMC 0-3 Yanga alifunga mabao mawili waliposepa na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo.

Bao moja  kwenye mchezo huo lilifungwa na Pacome ambaye ni kiungo anayeaminika kucheza na kutoa maelekezo akiwa uwanjani huku kichwani utambulisho wake ukiwa ni bleach.

Wakati Mudathir akifunga mabao mawili beki wa kupanda na kushuka Nickson Kibabage yeye alitoa pasi mbili kwenye mchezo huo moja alimpa Pacome na nyingine alimpa Mudathir wakiwa ugenini kwenye mchezo huo wa ligi.

Anakuwa ni mchezaji wa kwanza kufunga bao ndani ya mzunguko wa pili katika kikosi cha Yanga huku bao la kwanza mzunguko wa kwanza likifungwa na Dickson Job.

Job ambaye ni beki alifunga bao dhidi ya KMC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 5-0 KMC hivyo kenye mechi mbili walizocheza yanga na KMC pointi zote sita zimebaki Jangwani huku mabao jumla yakifungwa 8 na wakusanya mapato wa Kinondoni safu yao ya ushambuliaji inayoongozwa na Wazir Junior haijafunga bao.

Wazir Junio aliwahi kuwa ndani ya kikosi cha Yanga kabla ya kuondoka hapo alipoibuka akitokea kikosi cha Mbao na sasa yupo KMC akiwa kwenye changamoto mpya akitimza majukumu yake na amefunga jumla ya mabao saba kwenye ligi.

Share this: