Mbeba mikoba ya Ayoub Lakred Simba ni huyu
Kusaka pointi tatu ugenini mbele ya ASEC Mimosas
Mbadala wake atajwa kamili kuanza langoni
MBEBA mikoba ya Ayoub Lakred ndani ya kikosi cha Simba ambaye alikuwa ni chaguo la kwanza katika wachezaji 11 kwenye mechi za kimataifa zilizopita kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ametajwa na uongozi wa timu hiyo inayopeperusha bendera ya Tanzania anga la kimataifa.
Kikosi cha Simba kina kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Kwa upande wa langoni mlinda mlango Aishi Manula anapewa nafasi kubwa ya kuwa mbebe mikoba ya kipa huyo aliyekuwa ni chaguo la kwanza kwenye mechi zilizopita za kimataifa nyumbani na ugenini.
Ikumbukwe kwamba Simba Mei 2022 walikabidhiwa hundi yenye thamani ya milioni 50 kutoka SportPesa hiyo ni baada ya kufuzu hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika na kwenye hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika ofisi za SportPesa zilifanyika Masaki jijini Dar es Salaam kwa sasa wanashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika wakitafuta nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali.
Miongoni mwa waliohudhuria kwenye hafla hiyo 2022 ilikuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Tarimba Abbas, Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya, kutoka Simba ni Ofisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez wakati ule kabla hajajiuzulu, Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally na Erasto Nyoni alikuwa mwakilishi upande wa wachezaji lakini kwa sasa anapata changamoto mpya Namungo.
MBEBA MIKOBA AMETAJWA
Kwenye mchezo wa leo Simba inayotafuta nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ipo kundi B itakosa huduma ya mlinda mlango Ayoub Lakred ambaye kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca uliochezwa Uwanja wa Mkapa alianza langoni.
Sababu kubwa ya kutokuwa kwenye kikosi hicho ni kutumikia adhabu ya kadi za njano jambo ambalo linamfanya akosekane. Mbali na Lakred pia Willy Onana ambaye ni kiungo mshambuliaji naye hatakuwa kwenye kikosi cha Mnyama kutokana kwa kuwa bado hajawa fiti.
Kwa mujibu wa meneja wa Simba, Mikael Igendia amesema kuwa wanatambua umuhimu wa mchezo huo huku wakiwakosa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali huku wakiwepo wengine watakaotimiza majukumu yao.
“Mchezo wetu ni muhimu kupata ushindi na tunatambua kwamba kuna baadhi ya wachezaji ambao tutawakosa kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ayoub Lakred ambaye ni mlinda mlango, John Bocco nahodha pamoja na Willy Onana.
MBEBA MIKOBA ANA BALAA HUYO
Lakred alipata kadi mbili za njano dakika ya 89 kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablanca ule wa kwanza ugenini na mchezo wa pili walipocheza Uwanja wa Mkapa. Mchezo mwingine ambao alionyeshwa kadi ya njano ilikuwa dhidi ya Power Dynamos ilikuwa dakika ya 90.
Onana anaingia kwenye rekodi ya kuwa nyota wa Simba aliyefunga mabao mawili kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Wydad Casablanca ndani ya dakika mbili.
Alifunga bao la kwanza dakika ya 35 na lilela pili alifunga dakika ya 37 ushindi ukawa ni mali ya Simba kwa kukomba pointi tatu muhimu kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa huku mashabiki wakijitokeza kwa wingi.
“Lakred yeye ana adhabu ya kadi za njano, Bocco na Onana hawa walipata maumivu hivyo wanaimarikataratibu kwa wakati huu. Kukosekana kwa Lakred ina maana wapo makipa wengine kwenye eneo hilo watakaofanya kazi kutimiza majukumu yao ikiwa ni pamoja na Aishi Manula, Hussein Abel na Ally Salim hawa wote wapo tayari,” amesema.

POINTI WALIZOKOMBA BILA YA MBEBA MIKOBA
Simba kwenye msimamo baada ya kucheza jumla ya mechi nne ndani ya kundi B imekusanya pointi tano ikiwa nafasi ya pili namba moja ni ASEC Mimosas wenye jumla ya pointi 10.
Ipo wazi kwamba baada ya kuwasili Ivory Coast wachezaji walipewa program maalumu kwa ajili ya kurejea kwenye ubora wao na kuanza mazoezi rasmi kuwakabili wapinzani wao ASEC Mimosas kwenye mechi hizo za kimataifa kipa anayetarajiwa kubeba mikoba ya Lakred hakupata nafasi ya kuanza.
MSAFARA WA SIMBA ULIOPO IVORY COAST
Aishi Manula, Ally Salim na Hussein Abel. Upande wa ulinzi ni Shomari Kapombe, Israel Mwenda, David Kameta, (Duchu), Mohamed Hussein, Henock Inonga, Che Malone, Kennedy Juma, Hussen Kazi.
Eneo la viungo kuna Babacarr Sarr, Sadio Kanoute, Fabrince Ngoma, Mzamiru Yassin, Abdallah Khamis, Saido Ntibanzokiza, Kibu Dennis, Luis Miquissone, Clatous Chama na upande wa washambuliaji ni Pa Omary Jobe na Fredy Michael.
Mchezo wa kwanza uliowakutanisha wababe hawa ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 1-1 ASEC Mimosas wakagwana pointi mojamoja.

