Dr Omari mshindi bonus

Dr. Omari Sharif Chande, wikiendi iliyopita amejishindia jumla ya Sh 10,491,465, kama Jackpot bonus, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya 13, alizocheza.

Omari ambae ni daktari kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Idara ya Afya Mkoani Arusha alianza kucheza na SportPesa mwaka 2022, baada ya kuona kuna urahisi katika kucheza ukilinganisha na kampuni nyingine aliyokuwa anacheza nayo kwa muda mrefu.

“Mimi nilianza kucheza na SportPesa mwaka jana, kwa kipindi cha nyuma nilikuwa nacheza na kampuni nyingine, lakini nikaamua kujiunga na SportPesa baada ya kuona kuna urahisi katika kucheza ukilinganisha na kampuni zingine za kubeti.”

Mkeka
 Dr.Omari aliendelea kusema, huwa haipiti siku moja bila ya yeye kubeti, na mara nyingi huwa anaweka mikeka 2 ya timu moja moja, kwenye upande wa jackpot huwa anabeti mara mbili kwa siku, na kwenye ushindi huu nilibeti mikeka 3 ya mid-week jackpot.

Akizungumzia mkeka wa ushindi, Dr. Omari anasema siku hiyo alikuwa ametoka kwenye shughuli zake za kila siku, akarudi nyumbani kupumzika. Alipofika ghafla ujumbe wa simu uliingia, kuangalia saa ilikuwa ni mida ya saa saba za usiku, alianza kujiuliza kama ule ujumbe aliopokea ulikuwa ni kweli au umekosewa.

“Kiukweli ile sms ya ushindi ilivyoingia sikuamini kama ni kweli, hivyo basi nilienda moja kwa moja kwenye akaunti yangu ya SportPesa na kujaribu kutoa hela ikashindikana, palipokucha nilienda ofisi za Airtel kwa kuwa ndio mtandao ambao nilikuwa natumia kucheza, nilipofika pale mhudumu alinieleza kuwa line yangu ya simu haikuwa na shida yoyote, hivyo niwasiliane na ofisi ya SportPesa.

Dr Omari mshindi

Niliwasiliana na huduma kwa wateja kutoka SportPesa na walinielekeza kuwa ninahitajika kuja ofisini kwao ili niweze kuhakikiwa taarifa zangu, kwakuwa nilikuwa mbali nilimuagiza ndugu yangu aende kuhakikisha na kweli walimueleza ni lazima niwepo mwenyewe, hivyo ilinibidi nifunge safari kutoka Arusha kuja Dar es salaam, na leo nimefurahi kufika hapa kwani ndio mara yangu ya kwanza.”

Kuhusu atafanyia nini kiasi alichoshinda, Dr. Omari amesema, hela hii imekuja wakati muafaka sana kwani nina majengo ya biashara ambayo ninahitaji kuyamalizia ili nianze kuyapangisha kwa watu.

Dr. Omari aliongeza kwa kusema kuwa yeye huwa anacheza michezo yote kuanzia Multibet, na jackpot zote mbili, lakini sana yeye anapendelea kucheza mid-week jackpot na anaamini ipo siku atakuja kushinda hela kubwa zaidi ya aliyoshinda, pia ninapenda kuwashauri watu kuwa wasiache kujaribu kucheza kwani hakuna kitu ambacho hapa duniani hakina manufaa, ni mtu mwenyewe anavyojipanga na anavyotulia katika michezo hii, ukijipanga  huwezi ukakosa, na hatuwezi kufanana wote kila mmoja atapata kwa kiasi chake kwa sababu akili zetu pia hazifanani, hivyo basi ninawasihi watu waendelee kucheza kwa bidii.

Akitoa neno la pongezi kwa mshindi, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Dr.Omari kwa kufanikiwa kushinda  Jackpot bonus na kumtaka aendelee kucheza ili aweze kushinda zaidi.

Nianze kwa kukupongeza kwa ushindi wako wa Jackpot ya katikati ya wiki na pia nichukue nafasi hii kuwahamasisha watanzania ambao bado hawataki kuamini SportPesa ndio baba wa Jackpot zote nchini.

Dr. Omari ni mfano mwingine kwenu, kama alivyosema alianza kucheza na SportPesa mwaka jana na leo hii amefanikiwa kushinda kiasi hiki, mbali na hapo ameshashinda pia Multibeti.

Ni juhudi yako tu ya kucheza na kutokata tamaa, ukiamini siku yako itafika, basi na wewe mtanzania utafanikiwa. Mechi za Supa Jackpot yetu ya wikii hii zimeshtoka na kiwango cha Jackpot ni 780,463,640

 

 

Share this: