Dimba la Mohammed V lililopo Jijini Casablanca nchini Morocco litakuwa mwenyeeji wa mchezo wa marudiano wa Fainali ya Klabu bingwa barani Afrika ambapo mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Wydad Athletic Club watawaalika mabingwa wa kihistoria wa CAFCL, Al Ahly ya Misri.
Mchezo huo ni wa marudiano baada ya ule wa kwanza uliopigwa katika dimba la Cairo International, Al Ahly iliibuka na ushindi wa bao 2-1.
Mabao yaliyoipa ushindi Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita yalifungwa na Percy Tau na Mahmoud Abdel Moneim ‘’Karhaba’’ akiweka la pili kambani wakati lile la kufutia machozi lilifungwa na Said Eddine Bouhra dakika ya 86 ya mchezo.
Baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza, Kocha wa Al Ahly Mswizi Marcel Koller amesema wanaweza kuimaliza kazi waliyoianza nchini Misri ingawa hautokuwa mchezo rahisi kutokana na mazingira ya mchezo wa mkondo wa kwanza.
Kikosi cha Kohller kinatakiwa kizuie kipigo cha aina yoyote nchini Morocco ili waweze kubeba taji la kumi na moja la michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya Klabu barani Afrika.
‘’Mara zote fainali haiwezi kuwa nyepesi kwakuwa inazikutanisha klabu zenye ubora ndani ya bara la Afrika. Tulicheza vizuri na tulistahili ushindi. Hatukupoteza mchezo na ni imani yangu kwa uwezo uliopo ninaiona nafasi ya kupata magoli ya ugenini siku ya Jumapili’’. Alisema Kohller.
Upande wa Kocha wa Wydad Athletic Club, Sven Vandebroeck amesema bao walilolipata ugenini lina maana kubwa kwao na tafsiri yake wao watahitaji bao moja tu kuleta tofauti katika mchezo wa fainali siku ya Jumapili.
‘’Itakuwa faida kubwa sana kwetu,tunayo furaha kwa bao la ugenini tulilolipata nadhani litatuweka kwenye njia nzuri ya kulitetea Kombe tulilotwaa msimu uliopita’’alisema Sven raia wa Ubelgiji.
Nahodha wa wa Wydad Athletic Club, Yahya Jabrane amesema ana uhakika kwamba watakuwa katika nafasi nzuri ya kulitetea taji siku ya Jumapili.
‘’Nikiwa kama nahodha wa timu ninajiona ni mtu mwenye bahati kushiriki fainali ya pili mfululizo ya Ligi ya mabingwa Afrika,ni mafanikio makubwa kwanguna ninajukumu la kuwaongoza wenzangu kushinda ili tuwape furaha mashabiki wetu , itakuwa heshima katika fainali ya tatu mfululizo tunakutana na Al Ahly na iwapo tunawafunga maana yake tutaweka heshima ya kuwasimisha kwa mara ya tatu mfululizo‘’alisema Jabrane.
Upande wa Al Ahly ,Karhaba ambaye ndiye mtambo wa mabao wa Klabu hiyo atakuwa anafukuzia rekodi nzuri ya kucheka na nyavu kwani hadi sasa amefunga bao 5 katika mashindano haya.
Karhaba alifunga bao tatu kwenye mchezo wa makundi dhidi ya Coton Sports ya Cameroon kabla ya kufunga kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Esperance ya Tunisia.
Nyota huyo ameunda utatu mtakatifu na Percy Tau mwenye bao 5 pamoja na Hussein El Shahat mwenye mabao 5.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anahitaji bao moja tu ampiku Peter Shalulile wa Mamelodi Sundown na Percy Tau ili atwae kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa mashindano.
Katika mchezo wa mkondo wa kwanza takwimu zilionyesha kwamba Ahly walipiga mashuti 12(yaliyolenga lango ni 6) wakati Wydad walipiga mashuti 13(yaliyolenga lango ni manne).
Wenyeji wa mchezo walimiliki kwa asilimia 65 wakati Wydad walimiliki kwa asilimia 35,Ahly walipiga pasi 504 wakati Wydad walipiga pasi 273,wenyeji walipiga kona 5 na wageni walipiga kona 2.
Rekodi zinaonyesha katika michezo mitano ya mwisho walizokutana kila timu imeshinda mechi 2 na sare moja.
Kwa ujumla Al Ahly imeshinda jumla ya mechi 6 wakati Wydad imeshinda mechi 3 huku sare zikijitokeza mara 4 katika mechi 13 walizokutana.
Lakini katika fainali ya msimu uliopita, Wydad waliitandika Al Ahly na kuwavua ubingwa,swali ni je Al Ahly watakubali kipigo kwa msimu wa pili mfululizo?au wao ndio watalipa kisasi ?
Ikumbukwe katika mchezo wa mkondo wa kwanza Al Ahly ilimkosa kipa wake namba moja, Mohammed El Shaanawy na huenda akarekea katika mchezo wa fainali.
Mechi hii tayari ipo kwenye tovuti yetu. Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *15087#
