Wachezaji wa Mamelodi Sundownswakipambana na wachezaji wa Wydad Athletic ClubMamelodiWydad

Leo ndio siku ambayo mpira wa Afrika, utashuhudia moja kati ya mechi bora kabisa za mpira wa miguu katika ngazi ya vilabu Afrika ikipigwa kule Africa Kusini kati ya Mamelodi Sundowns na Wydad Athletic Club, katika uwanja wa Loftus Versfeld, jijini Pretoria.

Licha ya kupoteza wachezaji wake wawili kwa kuonyeshwa kadi nyekundu ambao ni Marcelo Allende na kiungo mshambuliaji Neo Maema, mabingwa hawa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns walifanikiwa kuwasimamisha mabingwa watetezi wa Klabu bingwa Africa, Wydad Athletic Club na kutoka nao suluhu ya bila kufungana, tena wakiwa nyumbani kwao nchini Morocco, kwenye dimba la Mohammed wa tano.

Masandawana walianza vyema mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza, ambapo katika dakika 10 za mwanzo, walifanikiwa kuandika bao la kuongoza, lililowekwa kambani na mshambuliaji wao matata Peter Shalulile.

Bao hilo lililalamikiwa na wachezaji wa Wydad Athletic Club na baada ya refa kuwasiliana na wenzake kupitia marejeo ya VAR, walibaini lilikuwa goli la kuotoea.

Bahati mbaya mnamo dakika ya 43 ya mchezo Masandawana walilazimika kusalia 10 uwanjani, kufuatia kiungo wao mshambuliaji Nae Maema alionyeshwa kwa kumchezea rafu mbaya nyota wa Wydad A.C, Amine Aboulfath.

Wakati wakiendelea kuwashangaza wengi kwa kuhimili shinikizo la wenyeji huku wakiwa 10 uwanjani. Marcelo Allende ambaye alitokea benchi naye alilimwa kadi nyekundi dakika ya 90 ya mchezo na kumfanya Kocha Rhulani Mokwena kutengeneza mpango mzuri wa kujihami na kweli walifanikiwa kuondoka salama bila kuruhusu bao katika mchezo huo.

Mlinda mlango wa Mamelodi Sundowns, Ronwen Williams alikuwa na siku nzuri langoni mwake, licha ya wachezaji wa Wydad Atheletic Club kupeleka  mashambulizi makali kupitia washambuliaji kama Bouly Sambou waliojaribu mara kadhaa bila kufua dafu.

Kuwa pungufu kwa Masandawana kuliwapa nafasi Wydad kuutawala mchezo, baada ya kumiliki mchezo kwa zaidi ya (asilimia 52 dhidi ya 48 za Mamelodi). Wenyeji walijaribu kwa ari na mali na kufanikiwa kupiga mashuti mengi  (11 kwa 6 ya Mamelodi).

Kwa namna ambavyo mchezo wa awali ulivyokuwa, timu ya Wydad Athletic Club wana kazi ya kufanya ili waweze kushinda mchezo huu wa leo. Mamelodi Sundowns wanatarajiwa kubadilika na kutumia advantage ya kucheza nyumbani huku wakiwa wanasapotiwa na mashabiki wao.

Mpaka sasa Wydad Athletic wanahesabika kama mabingwa watetezi wa kikombe la klabu bingwa Africa cha walipiga pasi nyingi zaidi (389 kwa 387). Wenyeji walipata kona nyingi (7-1).  Hii ni ishara kwamba vijana wa Sven Vandebroeck, Kocha wa ki Belgiji, walinufaika na upungufu wa wachezaji wa Mamelodi Sundowns, lakini walishindwa kuweka mpira kambani.

Kipa wa Wydad Athletic Club akiwaelekeza wachezaji wenzakeSuluhu hiyo ina maanisha nini, Mamelodi Sundowns wanawasubiri Wydad kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Mei 20 huko Tshwane nchini Afrika Kusini wakihitaji ushindi na si vinginevyo,na iwapo watatoka sare isiwe ya mabao kwani wataondolewa kwa sheria ya bao la ugenini.

Mamelodi Sundowns wana rekodi nzuri hivi karibuni wanapokuwa nyumbani katika michuano ya kimataifa,hawajapoteza katika mechi 11,wakishinda 9 na sare 2,hivyo itawahitaji Wydad Athletic Club kufanya kazi ya ziada kupata matokeo chanya katika mchezo huo.

Maema na Allende wote kwa pamoja watakosekana katika mchezo huo kwa sababu watakuwa wakitumikia adhabu ya kuonyeshwa kadi nyekundu.

Tangu Mei 5,2018, Mamelodi  Sundowns wamecheza dhidi ya Wydad Athletic Club nchini Afrik Kusini mara 4, Masandawana wameshinda mara 2 na sare 2 maana yake Wydad hawajapata ushindi nchini Afrika Kusini kwa kipindi hicho.

Mara ya mwisho kukutana kwenye ardhi ya Africa Kusini,ilikuwa Jumamosi ya Mei 13,2023 katika michuano ya Klabu bingwa Africa ambapo Mamelodi Sundowns iliibuka na ushindi wa goli 1-0.

Iwapo Mamelodi watashinda mchezo huu wa leo, basi watakuwa na nafasi kubwa ya kucheza fainali na timu ya Misri iliyocheza fainali ya msimu uliopita.

Tayari Al Ahly wapo mguu mmoja ndani baada ya kushinda kwa magoli 3-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Tupe maoni yako ya matokeo ambayo unafikiri yatakuwa ndani ya dakika 90 za mchezo huu.

Tayari mchezo huu baina ya timu hizi mbili upo kwenye tovuti yetu. Kubashiri au kubeti tembelea sportpesa.co.tz au piga*150*87#

 

 

Share this: