AL AHLY vs ESPERANCE- Itakuwa maajabu Esperance Kwenda Fainali
Timu ya mpira wa miguu ya Al Ahly Cairo, leo wanashuka uwanjani kupambana na Esperance ya Tunsia katika mechi ya marudiano ya kombe la klabu bingwa Afrika, baada ya mechi ya kwanza kuisha kwa Al Ahly Cairo2, kuichapa Esperance de Tunisia kwa magoli 3-0, katika Uwanja wa Stade Olympique de Rades.
Magoli ya Al Ahly Cairo yaliyopeleka msiba kwa Esperance de Tunis yaliwekwa kambani na mshambuliaji hatari Percy Tau aliyefunga mara mbili na Mahmoud Karhaba aliyefunga bao moja.
Matokeo hayo yakaisogeza hatua moja mbele Al Ahly Cairo kuelekea fainali ya Klabu bingwa Afrika huku yakiwaacha Esperance wakitafuta mchawi ambaye aliwafanya wapoteane wakiwa nyumbani.
Baada ya kipigo hicho uongozi wat imu ya Esperance ulifanya maamuzi ya kumfuta kazi Kocha Nabil Maaloul. Maswali yanayoulizwa kwa sasa ni je katika mchezo wa marudiano nani am dhamana ya kuiongoza klabu hiyo kwenda kujaribu kupindua ubao wa matokeo.
Esperance ambao waliingia na mfumo wa 4-2-3-1 walionekana wakitawala mchezo kwa kumiliki kwa asilimia 56 dhidi ya 44 wa Al Ahly Cairo, wakipiga mashuti mengi zaidi 13 dhidi ya 10 ya Al Ahly Cairo, mashuti yaliyolenga lango yalishabihiana 4-4, wenyeji walipiga pasi 471 dhidi ya 386 za Ahly, Esperance walipata kona 10 dhidi ya 4 za Ahly lakini hawakufua dafu na hata kupata bao la kufutia machozi.
Washambuliaji watatu wa Esperance waliosimama juu kuongoza mashambulizi ambao ni Ben Hammouda, Rached Arfaoui na Mootez Zaddem walishindwa kabisa kufuruka mbele ya ukuta wa Al Ahly Cairo uliokuwa ukiongozwa na miamba Ali Maaloul, Mohamed Abdelmonem, Yasser Ibrahim na Mohammed Hany huku kiungo mkata umeme Aliou Dieng akiimarisha ulinzi huo.
Kocha wa Al Ahly Cairo, Marcel Koller raia wa Uswizi anaonekana kuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wa leo katika dimba la Cairo International, pahala ambapo huwa wanajivunia uwepo wa mashabiki na wapenzi wao ambao wana mizuka ya kushangilia dakika zote za mchezo .
Ndani ya msimu huu, Al Ahly Cairo haijapoteza mchezo kwenye michuano ya kimataifa, wametoka sare ya magoli mawili dhidi ya Mamelodi Sundown, lakini mechi zote zilizosalia walishinda 3-0 dhidi ya Al Hilal Omrduman.
Hawakuishia hapo wakainyuka 3-0 timu ya Cotton Sport ya Cameroon, kabla ya kuisambaratisha Raja Casablanca, katika mechi ya robo fainali , kwa mabao 2-0. hivyo Esperance wanayo kazi ya ziada kuwasimamisha mapharaoh hao.
Timu hii ya Esperance ina matokeo mchanganyiko ugenini msimu huu. Walinyukwa na Plateau ya Nigeria mabao 2-1, wakatandikwa na timu ya Zamalek ya Misri kwa bao 3-1.
Baada ya hapo walitoka sare michezo miwili dhidi ya Al Merrikh na kushinda miwili bao 1-0 dhidi ya CR Belouzdad na 1-0 dhidi ya JS Kabylie kwenye mchezo wa robo fainali.
Mara ya mwisho kukanyaga ardhi ya Misri msimu huu ilikuwa machi 7,2023, ambapo kwenye hatua ya makundi walisambaratishwa kwa magoli 3-1, na leo wanarejea kwenye ardhi hiyo. Je watachomoka?
Ukitazama safari yao msimu huu, Esperance wamecheza michezo mingi dhidi ya wapinzani kutoka ukanda wao wa Kaskazini na sasa wanaendelea kupita kwenye njia hiyo ngumu.
Uzuri ni kwamba timu hizi zote ni mabingwa wa michuano hii, Esperance ni mabingwa mara 4 wakati Al Ahly Cairo wao ni mabingwa mara 10 hivyo bado haijaisha ingawa tofauti ya idadi ya mabao ni kubwa sana.
Wababe hawa wa soka la Afrika wamekutana mara 17 kwenye historia yao,Al Ahly Cairo imeshinda mara nyingi zaidi (10),Esperance wameshinda (3) na sare 4 .
Mbaya zaidi kwa Esperance wameshindwa kufurukuta mbele ya Al Ahly Cairo katika mechi 5 za mwisho walizokutana ambapo wamepoteza zote,takwimu ambazo sio za kuvutia kuelekea mchezo huo wa marudiano.
Rekodi ngumu zaidi kwa Esperance ni kwamba hawajawahi kuifunga Al Ahly Cairo katika ardhi yao ya nyumbani, lakini wamebahatika kupata sare mara 4, hivyo iwapo watashinda itakuwa si kufuzu pekee bali ni kuingia kwenye vitabu vyao vya kumbukumbu kwa kushinda kwa mara ya kwanza nchini Misri dhidi ya Mapharaoh.
Timu hizi zote zipo kwenye kiwango bora katika Ligi zao za nyumbani, Esperance ni vinara kwao na hawajapoteza katika michezo mitano na sare moja nao Al Ahly Cairo nao wameshinda mitano na sare mmoja, hivyo kati ya michezo 6 hawajapoteza hata mmoja.
Unasubiri nini kuweka mkeka wako kwenye mechii ya wakali wa kaskazini mwa Africa. Tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#