Wachezaji wawili wanaocheza michezo ya Jackpot ya SportPesa, wamejishindia vitita vinono vya Jackpot bonus ya kati kati ya wiki, almaarufu kama Mid Week na Supa Jackpot baada ya kupatia kwa usahihi mechi za Jackpot walizocheza, hivyo kujipatia bonus kama zawadi za kifuta jasho.
Wakizungumza katika ofisi za SportPesa baada ya uhakiki na makabidhiano wa mfano wa hundi wachezaji hao walisema wamefurahi kushinda Jackpot bonas na kwamba ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kushinda viwango vya zawadi ya Jackpot ambavyo hawajawahi kushinda tangu wameanza kubashiri na SportPesa.
Wa kwanza ni Jumanne Iddi Mwanja, mkazi wa kata ya kituntu, Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida. Yeye alishinda Tsh 5,382,603 katika Jackpot Bonus ya Mid-Week.
Jumanne alianza kucheza na SportPesa kuanzia Mwaka 2022, Mwezi wa tatu, baada ya kuwa anaona kupitia mitandao na magazeti, habari na washindiwa SportPesa, ambao walikuwa wakitangazwa baada ya kushinda.
‘’Mimi nilianza kucheza SportPesa Mwaka jana. Nakumbuka ilikuwa Mwezi wa tatu baada ya kuwa naona washindi mbali mbali wakitangazwa. Pia kulitokea msukumo mwingine kwani pale ninapoishi kulitokea washindi mbali mbali ambao nilikuwa nawafahamu’’.
Anaendnelea kwa kusema baada ya kuhamasika ilibidi aombe msaada wa kueleweshwa namna ya kujisajili, kuweka pes ana kucheza.
Pale ninapokaa kuna vijana wa kawaida na wengine naweza kuwaita vijana wa makamo ambao bado hawajafika umri wangu. Sasa mimi niliwatumia wale vijana kupata kujifunza namna ya kutumia simu hizi kucheza SportPesa.
Kwa mara ya kwanza nilianza kwa kuweka Tsh 500 na Tshs 300 ambazo zilikuwa zinabaki kama vichenji kwenye simu yangu. Sasa Mungu si Athumani nilishinda Tsh 29,300 na baada ya muda kupita siku nyingine nilishinda 9000’’. Alisema….
Naye Husseni Marangwi, mshindi mwingine wa Supa Jackpot bonus na mkazi wa Gongo la mboto Ulongoni B. Yeye ameshinda kitita cha Tsh4,697,457.
Husseni alianza kucheza na SportPesa mwaka jana 2022. Anaeleza kwamba aliifahamu SportPesa siku nyingi kupitia jezi za Simba kwa kuwa yeye ni mpenzi wat imu hiyo kindaki ndaki na huwa ananunua jezi kila msimu.
‘’Mimi niliifahamu SportPesa wakati ikiwa bado inaidhamini Simba miaka kama minne nyuma. Lakini kwa kucheza nimeanza mwaka jana. Unajua mwaka jana baada ya Simba kuachana na SportPesa lile vugugvugu la kuhamia kwa mdhamini mwingine lilinifanya niifuatilie SportPesa kwa undani.
Nilipowafuatilia nilibaini ni kampuni ya ubashiri na imekuwa ikitangaza washindi mara kwa mara ambao niliwaona kwenye mitandao ya kijamii’’.
Anaendelea kwa kusema wakati anaanza alikuwa anacheza Tsh 300 mechi kuanzia 12 mpaka 15. Katika kipindi hicho baada ya kujifunza namna ya kucheza.
‘’Namshukuru Mungu wakati naanza mwaka jana nilipata bahati ya kushinda hela nyingi kidogo kulinganisha na kiwango nilichokuwa naweka kama dau la kila mkeka niliokuwa nacheza. Najua huwezi amini lakini mara ya kwanza mimi kushinda ilikuwa katika mkeka wa multibet.
Niliweka dau la Tshs 300 na kucheza mkeka wa mechi 12 na kushinda Tsh 700,000. Nilishinda tena 500,000 kwa 1000 katika mkeka wa mechi za kawaida. Hapa unaweza kuona mtiririko wa ushindi wangu ulivyo kuwa.
Bahati yangu haikuishia hapo nilikuja kushinda tena Tsh 200,000 baada ya kuweka Tsh 500 kwenye mkeka wa mechi 7.”
Kuhusu mikeka yao ya Jackpot waliyoshinda anasema yeye kwanza huwa na kawaida ya kuchambua mikeka kwa siku mbili kabla hajaiweka rasmi.
‘’Mimi mara nyingi huwa nakaa na kuchambua timu kwa siu mbili kwa sababu siku hizi nacheza zaidi Jackpot ya kati kati ya wiki na Supa jackpot hivyo huwa najipa muda kuangalia timu na mwenendo wa timu husika.
“Kwa kifupi mkeka huu ulioshinda nilikuwa nimeweka jumla ya mikeka mitatu kwenye hii Jackpot. Mkeka wa kwanza ulikufa mapema. Wa pili nao halikadhalika ulikufa siku ya kwanza. Sasa huu ulioshinda siku ya kwanza nilipata mechi 8.
Siku ya Jumapili nilipata mechi tatu za kwanza na baada ya hapo nilifanikiwa kupata mechi tatu ngumu ambazo zote niliweka sare. Mechi hizo ni Stuttgart VS Bayer Leverkusen, Monaco VS Lille na Bologna VS As Roma. Baada ya hapo sikuendelea kuangalia matokeo kwa kuwa nilikuwa na uhakika wa bonus.”
Baada ya mechi kwisha nilikuja kupata sms ya hongera kutoka SportPesa ikinitaarifu kuhusu kushinda Supa Jackpot bonus ya ….
Naye mshindi wa Jackpot bonus ya kati kati ya wiki anasema yeye ana kawaida ya kuchambua timu kwa kuangalia odds zaidi Pamoja na madhaifu ya timu husika.
‘’Kwanza niseme hii ni moja ya sababu nilivutiwa na SportPesa ni kuwa mechi za Jackpot huwa zinawekwa odds zinazoonekana. Hii inanipa mimi urahisi wa kufanya ulinganifu na tathmini kwa kina na kwa urahisi.
Pili kwa wastani katika kila Jackpot za SportPesa ninazocheza huwa naweka wastani wa mikeka mitatu. Sasa katika mkeka huu niliyoshinda niliweka mikeka mitatu. Mmoja kwenye namba ya Tigo, mwingine kwenye namba ya Vodacom na wa tatu kwenye namba ya Airtel.
Mikeka miwili wa Tigo na wa airtel ilichanika mapema tu. Huu wa Vodacom ndio ulioshinda. Baada ya mechi kwisha nilipata SMS ya hongera, ingawaje muda sms inaingia simu ilikuwa kwenye chaja.
Nilipoisoma SMS ile baada ya kuchukua simu kutoka kwenye chaja nilifurahi sana, lakini furaha yangu ilikatishwa baada ya mimi kujaribu kutoa pesa kutoka kwenye akaunti yangu ya SportPesa kuja akaunti yangu ya M-pesa.
Jaribio la kuhamisha pesa lilifeli na ikanibidi nitafute namna ya kuwasilianan na Sportpesa kujua kulikoni. Nilishauriana na mwanangu na yeye alinipa simu yake na mimi nilipiga simu na kuelekezwa ni kawaida kwa akaunti kufungwa ili mteja aje kwa ajili ya uhakiki na makabidhiano ya mfano wa hundi.
Hii ndio sababu nipo hapa leo.
Wakimalizia washindi wote wawili wanawashauri watanzania kuiamini na kucheza na SportPesa ili waweze na wao kushinda zawadi kama ambavyo wao wameweza kushinda bonus za Mid-Week na Supa Jackpot.
Wakimalizia ….anasema kiasi alichoshinda atawekeza kiasi kwenye nyumba yake ambayo anasema inahitaji maboresho na kiasi kingine atawekeza kwenye biashara yake ya Spea.
Kwa yeye anasema sehemu ya pesa yake itakwenda kwenye nyumba yake na nyingine atawekeza kwa wanae ambao bado wanasoma mmoja akiwa chou cha UDSM na wengine bado wanasoma elimu ya upili.
Naye mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya SportPesa Sabrina Msuya aliwapongeza washindi wote wawili kwa ushindi wao na kuwataka waendelee kucheza ili weze kuja kushinda Jackpot yenyewe katika siku za mbeleni.
‘’Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza kwa kushinda Mid-Week Jackpot bonus na Supa Jackpot bonus na pia nawapenda kuwaasa endeleeni kucheza kwani ushindi hauna mwenyewe, ni juhudu yako kucheza kila mara utakapopata nafasi na hauwezi jua mnaweza kurudi tena kukabidhiwa Jackpot kamili.
Kwa watanzania nawaomba waendelee kucheza na Sportpesa kwani kila wiki washindi wa viwango mbali mbali wanapatikana’’. Alisema Sabrina.
Wiki hii Jackpot ya kati kati ya wiki imesimamia 583,071,860.

