NI SIMBA vs RUVU SHOOTING KMC vs SINGIDA BIG STARS NBC PL

SimbaRuvu KMCSimbaRuvuSimbaRuvu

 

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania, NBC Premier League bara inaendelea leo Ijumaa kwa mechi kati ya Simba SC dhidi ya Ruvu shooting, wakati KMC watawavaa Singida Big Stars.

Mchezo wa mapema utapigwa saa 10.00 Jioni kwenye dimba la Uhuru ambapo wakusanya mapato wa KMC watakuwa wakijiuliza mbele ya matajiri wa mafuta ya Alizeti Singida Big Stars ambao tayari wanayo tiketi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.

Wakusanya mapato hao hawapo vizuri kwenye msimamo wa ligi ya NBC Premier League na hadi sasa wanakamata nafasi ya 14 kati ya timu 16 wakiwa na jumla ya alama 26.

Hadi sasa timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni, wameshinda mechi 6 pekee katika michezo 27 waliyocheza katika Ligi Kuu ,wamepoteza 13 na sare 8,wameruhusu bao 30 huku wao wakifunga bao 22 tu.

Kutokana na mwenendo huo kwa muda mrefu, KMC waliamua kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi, kwa kuwaondoa kocha Thiery Hitimana na kumpa kibarua kocha Jamhuri Kihwelu.

Hata hivyo kocha Jamhuri Kihwelu hakuanza vizuri kibarua chake na mambo bado yamezidi kumwendea kombo ambapo katika michezo yake miwili ya kujaribu kuikoa timu hiyo amejikuta akipoteza dhidi ya Dodoma Jiji na Geita Gold.

Wakati huo huo timu timu hiyo imeruhusu mabao matatu na vile vile kushindwa kupata bao hata moja katika michezo miwili ambayo wamecheza chini ya kocha huyo.

 

Ili kujiweka katika mazingira mazuri timu ya KMC inahitaji kushinda mechi 3 zilizosalia ili wafikishe alama 35 ambazo angalau zinaweza kuwaweka Katika mazingira rafiki ya kutetea nafasi yao ya kusalia kwenye Ligi Kuu Tanzania.

Wanakutana na Singida Big Stars ambayo imeshajikusanyia alama 51 wapo nafasi ya 4, na wanahitaji kushinda ili kujaribu kuiondoa Azam iliyo katika nafasi ya 3 na alama zao 53 wakiwa wamecheza michezo 27.

Hans Van Pluijm na Vijana wake wanapambana ili kuipiku Azam huku kiungo wao Bruno Gomes mwenye bao 10 katika Ligi Kuu akihitaji kuongeza takwimu bora ambazo pengine zitamuongezea  nafasi ya kuwania tuzo ya kiungo bora msimu huu.

 

Singida Big Stars wameshinda mechi 15 katika Ligi Kuu,maana yake ni nusu ya mechi zote za Ligi, wamepoteza 6 na sare 6,wamefunga mabao 32 na kuruhusu 22,wana msimu bora kabisa tangu wapande Ligi Kuu..

Katika mechi tano za mwisho,KMC imepoteza 4 na kushinda 1,wakati Singida wao wameshinda 2,wamepoteza 1 na sare 2,na mchezo wa mwisho wamepoteza dhidi ya Yanga katika dimba la Liti.

Rekodi inaonyesha timu hizi zimekutana mara moja katika Ligi Kuu na Singida United iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Medie Kagere je, ni Singida wataendelea ubabe au KMC wataokoa jahazi lao linaloonekana linaelekea kuzama?

KMC ina nyota mahiri kama Keny Ally Mwambungu, Masoud Kabaye, Baraka Majogoro ,Daruweshi Saliboko, kitasa Ibrahim Ame, Kelvin Kijiri na hata Matheo Anthony ambaye alikuwa na wastani mzuri wa kufunga mabao mwanzo mwa msimu huu. wakati Singida Big Star ina mastaa kama Deusi Kaseke,Said Ndemla,Nickson Kibabage ambao wanao uzoefu mkubwa katika soka la Tanzania.

Kwingineko ni katika dimba la Azam Complex lililopo Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam, ambapo wekundu wa msimbazi Simba SC wakiwa hawana wanachogombea, watakuwa wakijaribu kuwafariji mashabiki na wapenzi wao baada ya kutupwa nje ya kinyang’anyiro cha mataji yote msimu huu, na kuwakaribisha Ruvu Shooting kutoka Pwani.

Simba wameondoshwa katika michuano ya klabu bingwa hatua ya robo fainali, pia wakatupwa nje ya michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup. Katika msimu huu Simba wameshindwa kutwaa ngao ya jamii na pia michuano ya Mapinduzi.

Kitu pekee wanachohitaji ambacho ni cha faraja kwao ni kushinda mechi zao zote tatu zilizosalia, wakianzia na huu mchezo dhidi ya Ruvu Shooting huku wakiwaombea dua mbaya Yanga wapoteze mechi zao tatu zilizosalia.

Iwapo Simba watashinda mechi zote watafikisha alama 73 na Yanga wakipoteza mechi zote watasalia na alama zao 71 na hapo ndipo wana msimbazi wanaweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu. Hizi ni hesabu kali sana zilizopo akilini mwao, jambo ambalo linaonekana haliwezekani lakini katika mpira wa miguu huwa yanatokea.

Mnyama anakutana na Ruvu Shooting, ambayo ipo mkiani katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa na alama 20 tu, baada ya michezo 27.  Ikumbukwe maafande hawa walimuondoa Kocha Charles Boniface Mkwasa na kumkabidhi kibarua kocha Mbwana Makata ili awanusuru na janga la kushuka daraja lakini hadi sasa mambo ni magumu zaidi.

 

Mchezaji wa KMC akipasha kujiandaa kuwakabili Sindida Big Stars.Maafande hao ni miongoni mwa timu mbili ambazo zimeshinda mechi chache zaidi katika Ligi Kuu msimu huu sawa na Polisi Tanzania (5) na ndio timu iliyopoteza mechi nyingi zaidi katika Ligi Kuu (17),ndio timu iliyofunga mabao machache zaidi kuliko timu yeyote katika Ligi Kuu(18),ni timu ya nneambayo imeruhusu bao nyingi zaidi(36) hivyo takwimu zao zinaonyesha ni wadhaifu.

Wakiwa na takwimu hizo mbaya,wanakutana na Klabu yenye takwimu bora zaidi katika kufunga mabao kuliko hata vinara wa Ligi hiyo,Simba ndio vinara kwa kufunga mabao (63) na ndio timu iliyopoteza mchezo mmoja pekee katika Ligi kuliko timu yeyote(1),ndio timu ya pili kwa kuruhusu bao chache katika Ligi(15),timu ya pili kwa kushinda mechi nyingi (19),hivyo Mbwana Makata na vijana wake wana kazi kubwa ya kufanya kuwazuia Simba.

Inaweza ikawa ni mechi ambayo inachagiza takwimu bora hata kwa wachezaji wa Simba mfano ni Jean Baleke ambaye ana mwenendo mzuri wa kupachika mabao,akiwa amefunga 8 katika mechi 7 za Ligi Kuu,lakini pia mchezaji kama Saido Ntibazonkiza mwenye bao 10 na pasi za mabao 10 atakuwa anaboresha takwimu zake kuelekea kwenye usiku wa tuzo za msimu.

Katika mechi 5 za mwisho Simba imeshinda 3 na sare 2, wakati Ruvu Shooting wameshinda 1 na kupoteza 4.

Mchezaji wa Ruvu Shooting akijiandaa kwa mechi na SimbaKatika mechi 5 za mwisho walizokutana,Simba imeshinda mara 4 wakati Ruvu Shooting wameshinda mara moja tu,je Simba watarejesha tabasabu kwa wapenzi na mashabiki wake au Ruvu Shooting watafufua matumaini ya kusalia Ligi Kuu?

Kama ilivyo ada yetu sportpesa mechi hizi tayari zipo kwenye tovuti yetu. Ili ubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

 

Share this: