Wachezaji wa Juventus wakishangiliaJuventusSevilla

Usiku wa Ulaya unaendelea leo hii kwa michezo miwili ya mkondo wa kwanza nusu fainali ya kombe la UEFA Europa kupigwa nchini Italia baina ya Juventus VS Sevilla na As Roma VS Bayer Leverkusen.

Huko Allianz Stadium, kibibi kizee cha Turin, Juventus watakuwa na kibarua dhidi ya Sevilla kutoka Uhispania, ikiwa ni kumbukizi ya michezo minne waliyokutana miaka kadhaa iliyopita katika mashindano ya Ulaya.

Ili kufika hapa walipo, Juventus na Sevilla zote zilijikuta zinadondokea kwenye michuano ya Europa baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya mwanzoni mwa msimu huu wa 2022/2023.

Tukianza kuwatazama Juventus, wao baada ya kuondoshwa katika Uefa Champions League walipangwa kucheza mtoano na timu ya Nantes ya Ufaransa.

Baada ya kuichapa Nantes kwa jumla ya mabao 4-0, kisha walikutana na Freiburg ya Ujerumani, kwenye 16 bora, ambapo Juve waliibuka kidedea kwa ushindi wa jumla wa bao 3-0.

Juventus walifanikiwa kuvuka kigingi cha hatua ya makundi na mtoano na kutinga hatua ya robo fainali na kufanikiwa kuwatupa nje timu ya Sporting CP ya Ureno kwa jumla ya mabao 2-1.

Sevilla kwa upande wao hadi kufikia hii ya kucheza mechi ya nusu fainali waliwatupa nje PSV Eindhoven ya Uholanzi, kwenye hatua ya mtoano kwa mikwaju ya penati 5-3.

Hapo awali timu hizo yaani Sevilla na PSV zilitoka sare ya mabao 5-5, baada ya michezo miwili. Timu ya Sevilla iliendeleza makali yake na walipofika hatua ya 16 bora walicheza na Fernabance ya Uturuki na kufanikiwa kuwafunga kwa magoli 2-1, kabla ya kukutana na Man United na kuwatoa kwa jumla ya mabao 5-3 kwenye hatua ya robo fainali.

Kwa ujumla Juventus hadi wanafikia hatua hii, wamecheza jumla ya michezo 6, wameshinda mara 4, hawajapoteza mchezo hata mmoja na wamefunga mabao 9, huku wakiruhusu mabao mawili tu.

Mchezaji wa Bayer Leverkusen akijindaa na mechi dhidi ya AS RomaSevilla ambao wanaonolewa na Kocha Jose Luis Mendibar, wamecheza jumla ya michezo 6, wameshinda 3, wamepoteza 2 na sare 1, wamefunga jumla ya mabao 10, wameruhusu mabao 5.

Ni dhahiri kwa takwimu hizi Juventus wanadhihirisha walikuwa na matokeo bora zaidi.

Juventus iliyo chini ya kocha Maximilliano Allegri, imekuwa na mwenendo usio ridhisha katika msimu huu, lakini hivi sasa nafasi waliyopo ni kama ya kushangaza hata katika Ligi Kuu ya Italia.

Juventus wanakamata nafasi ya pili baada ya kurejeshewa alama 15 walizopokwa kufuatia masuala ya udanganyifu ya ripoti za matumizi ya fedha.

Upande wa Sevilla wao katika La Liga wapo nafasi ya 11 na hawana nafasi kubwa ya kucheza kwenye mashindano ya Ulaya hivyo njia rahisi ya kufuzu ni kuhakikisha wanatwaa taji la Europa na wanapaswa kuwaondoa Juventus katika nusu fainali.

Timu hizi zimekutana mara 4 katika historia yao huku Juventus ikishinda mara 2, Sevilla mara 1 na sare 1.

Juventus wana silaha wanazozitegemea kama Leandro Paredes, Dusan Vhalovic, Angel Di Maria, Federico Chiesa huku Sevilla ikiwa na mastaa kama Alex Telles, Erik Lamela, Jesus Navas na hata Lucas Ocampos.

Kwa mechi 5 za mwisho, Juventus imeshinda 2, sare 2 na kupoteza 1 wakati Sevilla wao wameshinda 4 na kupoteza 1.

Tukihamia katika dimba la Olimpico, As Roma inayonolewa na Jose Mourinho watakuwa wenyeji wa Vijana wa Kocha Xabi Alonso, nawazungumzia Bayer 04 Leverkusen ya Ujerumani.

As Roma wao walianzia katika michuano hii tangu mwanzo na ndio maana wao wamecheza mechi 10, wameshinda 6, wamepoteza minne tofauti na Bayern Leverkusen ambao walidondokea Europa walitokea Klabu bingwa Ulaya.

Bayer Leverkusen wao wamecheza mechi 6, wameshinda 4, sare 1 na kupoteza 1, kwa kifupi AS Roma ndio timu pekee iliyosalia katika michuano hii ambayo ilianza tangu mwanzo.

Wachezaji wa AS RomaKatika hatua ya mtoano As Roma iliwaondoa Salzburg kwa bao 2-1, hatua ya 16 bora wakiichapa Real Sociedad kwa bao 2-0 kabla ya kuwasambaratisha Feyernoord ya Uholanzi kwa bao 5-2 na sasa wapo nusu fainali.

Bayer Leverkusen wao waliwatupa nje Monaco ya Ufaransa kwa penati 5-3 baada ya sare ha bao 5.

Hatua ya 16 bora, Leverkusen waliwaondoa Ferencvaros kwa bao 4-0 kabla ya kuwatandika vilivyo Union SG kwa bao 5-2.

Leverkusen wao nao nguvu kubwa ipo kwenye michuano hii, baada ya kuonekana nafasi yao ya kucheza Ligi ya mabingwa kupitia Bundesilga ni ngumu.

Kwa sasa wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi wakiwa na alama 48 huku mechi zimesalia 3 tu na walio juu yao wana alama 56 kila mmoja.

As Roma wana wachezaji wazuri wa kuchungwa kama Paulo Dyabala, Andrea Belotti, Nemanja Matic, wakati Bayer Leverkusen wanaye Patrick Schik, Mousa Diaby, Karim Bellarabi, Hin Capiye Frimpong na Palacious.

Duru za kimichezo zinatuarifu kuwa timu hizi zimekutana mara tatu katika historia yao na kila timu imeshinda mara moja na kutoka sare moja.

Kwa mechi za karibuni As Roma imecheza mechi 5, imeshinda 1, imepoteza 2 na sare 2, nayo Leverkusen katika mechi 5 za mwisho imeshinda 2, sare 2 na kupoteza 1.

Ni matumani yetu uchambuzi huu utatumika kama chachu ya kuongeza maarifa kwa wale wadau wetu wanaopenda kubashiri. Tayari zote mbili zipo kwenye tovuti yetu, na ukitaka kuweka mkeka wako tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

Share this: