YANGA VS MARUMO- Muda Wa Yanga Kungára Africa.
Patashika nguo kuchanika ya kipute cha nusu fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kinashika kasi ambapo kesho Jumatano kuanzia majira ya Saa 10 Jioni, Klabu ya Wananchi Yanga (Tanzania), watakuwa wenyeji wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini ikiwa huo ni mchezo wa raundi ya kwanza kwa hatua ya nusu fainali.
Mchezo huo wa kesho kwa Yanga, ni mechi ya kihistoria ambayo wanataka kuiandikisha kwa kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele, kabla ya kwenda kuimalizia safari yao ya matumaini nchini Afrika Kusini katika mechi ya marudiano.
Na kwa kuzingatia kuwa ni mchezo wa kihistoria, Yanga wamekuja na Kauli mbiu isemayo ‘’Our Team Our Time’’ wakimaanisha Timu yetu, Wakati wetu, wakijihamasisha kuhakikisha wanaibuka na ushindi.
Yanga na Marumo zimetinga hatua hiyo si kwa kubahatisha licha ya kutopewa nafasi hapo mwanzoni lakini kadri muda ulivyokuwa unasogea,wakadhihirisha kuwa wana ubora mkubwa na kulithibitisha hilo walimaliza vinara kwenye hatua ya makundi ya michuano hii ya Kombe la Shirikisho.
Timu hizi zinakutana zikiwa na safari ya kushangaza , Yanga ambayo ilidondokea katika michuano hii baada ya kutupwa nje ya Klabu bingwa Afrika,hawakupewa nafasi kubwa ya kufikia hatua hii lakini hivi sasa wanaonekana kuwa ni timu hatari zaidi na wanapewa nafasi ya kucheza fainali.
Upande wa Marumo waliongoza Kundi A wakiwa na alama 12 wakafuatiwa na USM Alger ambao wao waliondolewa hatua ya robo fainali na FAR Rabbat na wa Algeria hawa walikusanya alama 11,Saint Eloi Lupopo ya Congo DR walimaliza na alama 5 wakati Akhdar walimaliza mkiani wakiwa na alama 5 .
Yanga kutoka mitaa ya Jangwani ambao wao waliangukai kwenye michuano ya Shirikisho baada ya kutupwa nje na Al Hilal ya Sudan kwenye hatua ya awali ya Klabu bingwa,wao walifanikiwa kumaliza vinara wa kundi D ambao wao walikusanya alama 13,wakafuatiwa na US Monastir waliomaliza na alama 13, Real Bamako walikusanya alama 5 huku TP Mazembe walimaliza na alama 3.
Hatua ya robo fainali Marumo waliwasambaratisha matajiri kutoka Misri, Pyramids tena wakiwalazimisha sare huko Cairo kabla ya kuwanyuka bao 1-0 huko Afrika Kusini wakati Yanga wao waliwabwaga Rivers United kwa ushindi wa bao 2-0 baada ya michezo yote miwili.
Tukirejea kuzitazama timu hizi ndani ya msimu huu,tuanze na Marumo Gallants ambao kwenye Ligi yao ya nyumbani PSL waliuanza vibaya na hadi mwanzoni mwa Januari 2023 walikuwa wapo mkiani baada ya michezo 8 bila ushindi na hadi kipindi hicho walikuwa wameshinda mechi 2 tu.
Kufuatia matokeo hayo Marumo walimtambulisha Kocha wa zamani wa Simba,Dyllan Kerr ambaye alitua na bahati kwani walicheza mechi 8 bila kupoteza huku wakishinda mechi 4 za mwanzo na kuondoka mkiani mwa msimamo lakini jambo zuri ndiye amewafikisha nusu fainali ya Kombe la Shirikishoo.
Kabla ya kupoteza wikiendi iliyopita dhidi ya Mamelodi Sundown,Marumo walicheza michezo 8 katika mashindano yote bila kupoteza,wakishinda minne na sare minne jambo linaloashiria wapo katika kiwang bora kwa siku za karibuni.
Jambo la kuvutia kutoka kwa wakali hao wa Afrika Kusini wanajivunia rekodi yao ya kutopoteza mchezo katika michuano ya Kombe la Shirikisho kwenye dimba lake la nyumbani ,ambapo wamecheza michezo 9,wameshinda mara 8 na sare moja,hivyo Yanga wanapaswa kulazimisha ushindi kwenye uwanja wa Mkapa katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali.
Upande wa Yanga,wao wana msimu mzuri katika Ligi Kuu ya Tanzania bara kwakuwa ndio vinara na wanahitaji alama tatu pekee kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu, vilevile wapo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la TFF,na wapo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika,ukiwatazama wapo katika kinyang’anyiro cha mataji matatu msimu huu.
Chini ya kocha Nassredine Nabi ,Yanga imeimarika kwani hadi wanafikia hatua hii,wamepoteza mechi moja pekee ambayo ilikuwa ni ya kwanza hatua ya makundi dhidi ya US Monastir kwa bao 2-0,lakini tangu hapo wameendeleza ushindi na sare katika michuani hii.
Yanga wana rekodi nzuri kwa Mkapa msimu huu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho, wametoka sare mara moja dhidi ya Rivers United kwenye hatua ya robo fainali,lakini wameshinda mechi zote tena ikifunga kuanzia bao 2 katika kila mchezo.
Kinachochagiza mchezo huu ni uwepo wa washambuliaji wawili ambao ndio vinara kwenye kupachika mabao, kwa Marumo Gallants wanaye Ranga Chivaviro na Fiston Mayele ambao kila mmoja amefunga mabao matano.
Stori nyingine inayotawala mchezo huo ni uwepo wa kocha Dyllan Kerr ambaye alifanya kazi katika Klabu ya Simba msimu wa 2015/16, na wengi wakiamini kwakuwa anaujua utamaduni wa Tanzania huenda akawa na picha halisi ya mchezo huo ingawa ni muda mrefu tangu aondoke na mambo mengi ya mebadilia kwa Wanajangwani.
Kuelekea mchezo huu imetolewa taarifa kutoka Kamati ya nidhamu ya CAF ambayo imeipiga faini Klabu ya Yanga, Jumla ya dola za Kimarekani elfu 35 (Milioni 80.5) za kitanzania kwa makosa makubwa mawili.
1-Matumizi ya fataki kwenye mchezo dhidi ya Rivers United ya Nigeria faini yake ni dola 1000.
2-Tukio la basi la timu kuvamiwa na kuibiwa pesa dola 5200 na kuwapulizia harufu mbaya inayosemekana kuwa sumu, faini yake ni dola 25,000.
Aidha Yanga kwakuwa kwao kwenye nusu fainali ya CAFCC wanapaswa kuhakikisga usalama wa timu pinzani (Marumo Gallants.
Inawezeka taarifa hii ikawa sehemu ya kuwaondoa mchezoni Marumo wakifahamu kuwa kwa Mkapa si pahala salama na ikawa faida kwa Yanga .
Ni matumaini yetu kwamba uchambuzi huu ambao umeletwa kupitia blog hii utakupa ahueni ya kubashiri mchezo huu ambao unategemewa kuchezwa hapo kesho majira ya jioni..
Tayari mechi hii ipo kwenye tovuti, kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#