Patashika ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) imefikia hatua ya nusu fainali ambazo zinahusisha vilabu vinavyoshiriki ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC, Simba SC, Yanga SC na singida Big Stars, ambazo zinatarajiwa kuanza kushuka dimbani kuanzia siku ya Jumapili.
Stori ya kuvutia ni kwamba timu zilizotinga hatua hiyo zote ndizo zilizopo juu kwenye msimamo wa ligi kuu ambapo vinara ni Yanga, Simba, ambao wapo nafasi ya kwanza na ya pili, Singida Big Stars yupo nafasi ya tatu na Azam wanashika nafasi ya nne na wote wameshafuzu kucheza michuano ya kimataifa msimu ujao.
Azam FC ilifuzu kwa kuitandika Mtibwa Sugar bao 2-0 wakati Singida Big Stars waliwalaza Mbeya City kwa bao 4-1, Mabingwa watetezi Yanga, walikata tiketi baada ya kuwacharaza Geita Gold kwa bao 1-0 wakati watani zao Simba walitoa kipigo cha aina yake dhidi ya Ihefu cha bao 5-1 katika hatua ya robo fainali ya ASFC.
Jambo la kufurahisha ni namna droo ya nusu fainali ya ASFC ilivyojipanga. Azam Fc wataumana na Simba ikiwa ni kumbukumbu ya mchezo uliopigwa mnamo juni 27,2021 mkoani Ruvuma ambapo Simba iliitandika Azam Fc kwa bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa katika dimba la Majimaji Mkoani Ruvuma.
Mara zote mechi za aina hii huwa zina wachezaji ambao wamekuwa na kiwango cha kushangaza kama ambavyo upande wa Azam,mshambuliaji Prince Dube ambaye alifunga bao dhidi ya Simba katika mchezo wa mwisho ambao wanalambalamba na wana msimbazi walitoka sare.
Licha ya Azam kuwa na matokeo mazuri dhidi ya Simba msimu huu kwa kutopoteza, lakini haijawa na wachezaji wenye takwimu bora, lakini wana nyota ambao kwa siku za karibuni wamekuwa na kiwango kizuri kama Abdul Seleman Sopu ambaye ana mchango mzuri katika mechi za hivi karibuni.
Upande wa Simba bila shaka Jean Baleke ambaye alifunga mabao matatu dhidi ya Ihefu katika mchezo wa robo fainali ndiye nyota wa kuchungwa katika mchezo huo.
Mtanange mwingine wa kukata na shoka ni baina ya Singida Big Stars ambao watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi wa michuano hiyo Klabu ya Yanga, mchezo utakaopigwa katika dimba la Liti mkoani Singida
Singida inajivunia kiungo wake Bruno Gomes ambaye kafunga mabao 9 katika Ligi Kuu msimu huu lakini upande wa Yanga,Fiston Mayele na Clement Mzize bila kusahau Aziz Ki wamekuwa ndio vinara wa mabao katika klabu hiyo msimu huu.
Kulingana na droo hiyo upo uwezekano wa kuwashuhudia wababe wa soka hapa nchini wakakutana katika mchezo wa Fainali na wakaturejesha kwenye kumbukumbu ya Julai 25 2021, ambapo Simba ilitwaa ubingwa mbele ya Yanga kwa ushindi wa bao 1-0 katika Fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.
Vilevile timu hizi zilikutana katika hatua ya nusu fainali msimu uliopita ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Simba na Yanga tayari zimeshacheza mechi ya Derby ya Ligi Kuu Tarehe April 16,2023 na Yanga kuchapwa magoli 2-0 na Simba huku magoli yakifungwa na Inonga na Denis Kibu.
Tafsiri ya haraka katika nusu fainali hii ni kwamba upo uwezekano mkubwa wa kuishuhudia dabi ya pili ya timu za Kariakoo kabla ya msimu huu kumalizika. Hilo linawezekana kutokana na namna fomu ya timu zote mbili zilivyo kwa sasa.
Pamoja na kuwa dalili zote zinaonyesha timu za Simba na Yanga zina nafasi kubwa ya kwenda hatua ya fainali, kwa upande mwingine timu ya Azam na Singida United nazo zinatarajiwa kutoa upinzani mkali dhidi ya wababe hawa wa Kariakoo ili na wao waweze kupata japo kombe la kufutia machozi, baada ya kutokuwa na uhakika wa kombe la ligi kuu ya NBC.
Tunategemea mechi hizi za nusu fainali ambazo zitachezwa kuanzia kesho kuamsha ari ya ushindani baina ya timu zote nne ambazo zinachauana kwenye msimamo wa ligi kuu ya Tanzania NBC. SportPesa tukiwa kama wadau wa michezo, hasa hasa mpira wa miguu tayari tumeshakuwekea mechi kati ya Azam VS Simba katika tovuti yetu.
Mpaka muda tunaandika makala hii, mechi ya Yanga iliombwa kusogezwa mbele kutokana na ushiriki wa timu hiyo ya Jangwani katika mechi za hatua ya nusu fainali katika kombe la shirikisho barani Africa, ambapo Yanga anategemewa kucheza na Mallumo gallants siku ya Jumatano Tarehe 10, 2023.
Tayari TFF jana wameusogeza mbele mchezo huo mpaka tarehe ambayo itatangazwa mbeleni na mechi ya Azam dhidi ya Simba
Kubashiri tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

