Timu ya Brighton Hove Albion leo usiku inashuka dimbani katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu ya Uingereza, almaarufu kama EPL. Licha ya kufanya vizuri ndani ya msimu huu imeendelea kuwa kiboko ya baadhi ya vigogo katika EPL. Sasa leo wanakipiga na mashetani wekundu Manchester United, katika uwanja wa American Express Community Stadium.
Ubora wa Brighton &Hove Albion ulianza kudhihirika ilipokuwa chini ya Graham Potter ambaye aling’arisha vilivyo huku vijana kadhaa wakionyesha umahiri jambo ambalo liliwavuta Chelsea kumchukua Kocha huyo pamoja na beki Cucurella, lakini kama haitoshi Arsenal nayo ikavamia shamba lao na kumnyakua Leandro Trossard kwenye dirisha dogo la usajili.
Pamoja na kuondokewa na kocha wao pamoja na nyota wake bado Brighton wakaonyesha umahiri wa kumpa kibarua Roberto De Zerbi ambaye alijiunga nao Septemba 18,2022 akitokea Shakhtar Donetsk ya Ukraine na ameifanya Klabu hiyo kuwa moto wa kuotea mbali.
Kocha huyo ameiongoza Brighton katika michezo 25 ya EPL, ameshinda mechi 11, sare 6 na akapoteza michezo 8, huku kikosi chake kikifunga mabao 50. Mchezo wake wa kwanza wa EPL ulikuwa dhidi ya Liverpool pale Anfield walipotoka sare ya bao 3-3 ambapo Leandro Trossard akawa nyota wa kwanza wa Brighton kufunga Hat Trick katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Si chini ya kocha De Zerbi pekee, lakini hata wakati wa kocha Potter, Brighton walidhihirisha kuwa wao ni kiboko ya vigogo katika michezo waliyocheza kwenye michuano ya kombe la ligi wakiwatupa nje Arsenal, kwa kuwapa kipigo cha mabao 3-0, katika uwanja wa Emirates, na kwa kudhihirisha ubabe wao, waliowaondosha Liverpool kwenye michuano ya kombe la FA kwa kuwafunga magoli 2-1.
Katika Ligi Kuu EPL, Brighton waliwacharaza Chelsea bao 4-1,wakatoka sare ya bao 3-3 na Liverpool,waliinyuka Leicester City bao 5-2,waliwatandika Manchester United katika dimba lao la Old Traford kwa bao 2-1,wakawashikilia Newcastle United kwa kutoka nao suluhu,ni Man City na Tottenham Hotspurs pekee ambazo zipo juu yao katika msimamo ndio zilizowafunga wagumu hao.
Mashetani wekundu wanakutana wa wakali hawa wakiwa na kumbukumbu ya kushindwa kuwafunga katika michezo mitatu mfululizo iliyopita. Miwili ikiwa katika ligi kuu ya EPL ambayo walifungwa kwa bao 4-1 na 2-1 kabla ya kutoka nao suluhu kwenye nusu fainali ya FA ambapo The Red Devils walishinda kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza.
Kwa maana hiyo mchezo wa leo una tafsiri pana kwa Kocha Erik Ten Hag ambaye mchezo wake wa kwanza katika EPL ulikuwa ni dhidi ya Brighton ambapo walichapika kwa mabao ya Pascal Glob na Dany Welbeck.
Manchester United watakuwa wanahitaji kulipa kisasi lakini kuimarisha mbio zao za kumaliza ndani ya nne bora ambayo itawarejesha kwenye michuano ya klabu bingwa barani ulaya msimu ujao.
Ten Haag na vijana wake wapo nafasi ya 4 kwenye msimamo wa EPL, wakiwa na alama 63, baada ya michezo 32, wanahitaji kushinda ili waketi kwenye nafasi ya 3 ambapo watakuwa wamewashusha Newcastle United wenye alama 65 lakini The Magpies wao wamecheza mchezo mmoja zaidi ya The Red Devils.
Ushindi kwa Man United utakuwa na faida zaidi kwa kuwatoroka Liverpool ambao nao wameanza kuja kwa kasi baada ya ushindi wao dhidi ya Tottenham Hotspurs na sasa wapo nafasi ya 5 wakiwa na alama 56 baada ya michezo 33.
Brighton kwa sasa wapo katika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa EPL, wakiwa na alama 52, baada ya michezo 31. Wameshinda michezo15, kutoa sare 7 na kupoteza michezo 9. Wamefunga jumla ya mabao 61 na kuruhusu kufungwa magoli 40. Takwimu hizi zinaonyesha wameimarika sana msimu huu.
Iwapo Brighton watashinda mechi ya leo, basi watafikisha alama 55 na watawashusha Tottenham Hotspurs na Aston Villa waliopo katika nafasi za 6 na 7 wakiwa na alama 54 kila mmoja. Timu hizo mbili nazungumzia Aston Villa na Tottenham wamecheza michezo mitatu zaidi ya Brighton, hivyo hesabu za kocha wao Di Zerbi zinaweza kuwa nzuri iwapo watashinda mechi zao za viporo ambavyo vinaweza kuwasogeza kwenye mbio za kuwania nafasi ya nne bora.
Kuelekea mtanange huu wa leo utakaopigwa katika dimba la American Express Community Stadium, Brighton watashuka katika dimba lao wakiwa na motisha ya ushindi walioupata katika mchezo uliopita dhidi ya Wolves pale Amex Stadium ambapo waliibuka kidedea kwa bao 6-0 shukrani za dhati kwa mabao ya Dany Welbeck, Pascal Gross na Denis Undav na kuwafanya wafikishe alama nyingi zaidi katika EPL kwenye historia yao (52).
Ikumbukwe katika mchezo huo Kocha Di Zerbi aliamua kuwapunzisha nyota wake muhimu kwenye kikosi chake ambao ni Moises Caicedo, Alexis Mac Allister, Kaoru Mitoma lakini wakapata ushindi ambao uliibua hisia za wengi kuwa Kocha huyo ana kitu kikubwa katika EPL.
Ijapokuwa yeye amekwepa sifa hizo na kumtaja Pep Guardiola wa Man City na kusema kwamba yeye ndiye amejenga daraja la juu la ubora.
Kuwapumzisha Caicedo, Mac Allister na Mitoma kunaleta tafsiri ya kwamba nyota hawa wanarejea wakiwa na nguvu nzuri katika mchezo wa leo dhidi ya Manchester United.
Upande wa Man United ambayo nayo imetoka kuwacharaza wagumu wengine katika EPL Aston Villa, timu ambayo ilikuwa imecheza mechi 10 bila kupoteza.
Kikosi cha kocha Unai Emery kilifunga katika kila mechi kati ya hizo 10, hivyo kushindwa kufunga dhidi ya The Red Levils kulidhihirisha waliongeza kitu katika mchezo huo.
Baada ya ushindi dhidi ya Villa, Kocha wa Man United Erik Ten Hag alipongeza kiwango cha mabeki Victor Lindelof ambaye meonyesha kiwango kizuri akiungana na Luke Shaw katika idara ya ulinzi ya kati ambayo itawakosa Lissandro Martinez na Raphael Varane ambao ni majeruhi hadi mwisho wa msimu.
Lindelof ambaye alionekana kuzuia hatari mara nne kwenye mchezo wa Man U dhidi ya Spurs,ameaminiwa kucheza kwenye nafasi ya ulinzi dhidi ya nahodha Harry Maguire ambaye hajawa na msimu mzuri hadi sasa.
Takwimu za wachezaji kwa timu zote mbili zinapaswa kuzingatiwa tukianza na wenyeji ambao ni Brighton wana washambuliaji vinara kama Pascal Gross na Alexis Mac Allister ambao kila mmoja amepachika mabao 8. Mchezaji Kaoru Mitoma ana mabao 7, huku Solly March akiwa amepachika mabao 6.
Vinara wa pasi za mabao ni Solly March (7), akifuatiwa na Pascal Gross (6), wakati Kauri Mitoma anazo pasi za mabao 5.
Takwimu nyingine ni za nyota vinara kwa kupiga mashuti ya kulenga lango kwa Brightoni ni Alexis Mac Allister (29), Solly March (25), Dany Welbeck (19) na Kaoru Mitoma (17.
Upande wa Manchester United kinara wa kupachika mabao ni Marcus Rashford (16),akifuatiwa na Bruno Fernandes (6) na Jadon Sancho (5).
Vinara wa kutoa pasi za mabao ni Bruno Fernandes (8),akifuatiwa na Christian Eriksen (7) na Marcus Rashford(5).
Wakali wa kupiga mashuti yaliyolenga lango kwa Man United ni Marcus Rashford (41), Bruno Fernandes (27) na Antony Martial(21).
Rekodi zinaonyesha kwenye mechi 5 za mwisho za Brighton& Hove Albion,imeshinda mara 2 na kupoteza 3 huku Man United wao wameshinda 3 ,wamepiteza 1 na sare 1.
Tangu msimu wa 202/21, Klabu hizi zimekutana maa 5 katika EPL,Manchester United imeshinda michezo mitatu huku Brighton ikishinda mara mbili .
Kupitia takwimu na historia zinaweza kukuongoza katika ubashiri wako kupitia tovuti ya sportpesa ujishindia mara dufu zaidi.
Mechi ipo tayari kwenye tovuti yetu. Kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*187#

